Monday, September 23, 2013

JICHO LA TATU...


SHULE KONGWE SASA KUREJESHEWA KIDATO CHA KWANZA...

Mizengo Pinda.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema Serikali inashughulikia utaratibu wa kurejesha utoaji wa elimu ya kidato cha kwanza hadi kidato cha nne, katika baadhi ya shule kongwe, ili kurudisha ufaulu uliokuwepo na kuimarisha malezi ya watoto kuanzia elimu ya chini. 

Sunday, September 22, 2013

WALIOKUFA WESTGATE SHOPPING MALL SASA WAFIKIA 59, WENGINE 175 WAJERUHIWA...

Mwanajeshi akilinda usalama nje ya jengo hilo.
Vikosi vya usalama vikiwa tayari kwa mapambano ndani ya jengo hilo.
Habari tulizopata muda mfupi uliopita zinasema jumla ya watu 59 wamethibitishwa kufariki hadi sasa kufuatia mashambulizi kwenye jengo la Westgate Shopping Mall mjini Nairobi.

WALIOJERUHIWA SHAMBULIO LA KENYA SASA WAFIKIA 162, AL-SHABAAB YAKIRI KUHUSIKA...

Askari wa Jeshi la Kenya wakiwa wamejipanga nje ya jengo hilo.
Mmoja wa majeruhi akipatiwa msaada na wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu.
Habari zilizopatikana muda mfupi uliopita zinasema idadi ya majeruhi katika shambulio la uvamizi wa jengo la maduka la Westgate nchini Kenya imefikia zaidi ya 162 huku kundi la al-Shabaab lilitangaza kuhusika na tukio hilo.
Wakati idadi ya majeruhi ikifikia hapo, watu waliokufa mpaka sasa inaaminika kufikia zaidi ya 40.
Polisi na wanajeshi nchini humo wameweza kudhibiti ghorofa ya kwanza na ya pili kwenye jengo hilo, huku wito ukitolewa na mamlaka husika kwa watu kujitokeza kwenda kuchangia damu kwa ajili ya majeruhi wa tukio hilo.
Inaaminika bado kuna mamia ya watu wa mataifa mbalimbali waoshikiliwa mateka ndani ya jengo hilo wakati milio ya risasi imeendelea kusikika ndani ya jengo hilo.
Rais Uhuru Kenyatta amewataka wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki na kuahidi askari wake watawashinda wavamizi hao ndani ya kipindi kifupi kijacho.
Tayari serikali ya Canada imethibitisha vifo vya raia wake wawili akiwamo mfanyakazi wa Ubalozi wake nchini Kenya.

SHAMBULIO LILILOUA WATU 39 KENYA LILIWALENGA WASIOKUWA WAISLAMU...

KUSHOTO: Askari wa Kenya akijiandaa kukabiliana na wavamizi hao jana. JUU NA CHINI: Baadhi ya majeruhi wakisaidiwa kutoka kwenye jengo hilo.
Takribani watu 39 wameripotiwa kufa na zaidi ya 50 kujeruhiwa wakati polisi walipotupishiana risasi na watu wenye silaha katika eneo moja la maduka kwenye mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

MISS TANZANIA 2013 APATIKANA, NI HAPPINESS WATIMANYWA...

Happiness Watimanywa.
Taji la urembo wa Tanzania mwaka 2013 limepata mwenyewe na safari hii limekwenda mkoani Dodoma.

FAMILIA YAUAWA KIKATILI KWA KUNYONGWA NA KUCHINJWA...

Sehemu ya Jiji la Mwanza.
Watu watatu wa familia moja akiwemo mtoto wa mwaka mmoja wameuawa kikatili kwa kuchinjwa na wawili kunyongwa katika Mtaa wa Ihila, Kata ya Buhongwa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

KANISA LAJENGWA KUMUENZI HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE...

Askofu Telesphor Mkude.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Telesphor Mkude, amesema ili amani iendelee kudumu ni vema kila mtu akajua haki na mipaka yake kwenye jamii ili kuepuka mifarakano isiyo ya lazima.

JICHO LA TATU...


ALIYEMJERUHI MWIGIZAJI AUNTY EZEKIEL APANDISHWA KIZIMBANI...

Aunty Ezekiel.
Mfanyabiashara Ivony Maximilian, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka ya  kumjeruhi muigizaji wa filamu Aunty Ezekiel kwa chupa wakiwa klabu Bilicanas.

WACHIMBAJI TANZANITE WAFA KWA KUKOSA HEWA MGODINI USIKU...

Eneo la machimbo ya Tanzanite.
Watu wawili ambao ni wachimbaji wadogo wa madini ya tanzanite katika Mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro, Manyara wamekufa wakiwa ndani ya mgodi baada ya kukosa hewa.

Saturday, September 21, 2013

HATIMAYE MASOGANGE AACHIWA HURU, ALIMWA FAINI SHILINGI MILIONI TANO...

Agnes Gerald 'Masogange'.
Habari zilizotufikia zinasema kwamba msanii Agnes Gerald 'Masogange' aliyekuwa amekamatwa nchini Afrika Kusini kwa tuhuma za kukamatwa akisafirisha dawa za kulevya, ameachiwa huru jana.

HUYU NDIYE DAKTARI FEKI ALIYENASWA HOSPITALI YA MUHIMBILI...

Dismas John Macha baada ya kukamatwa jana.
Daktari anayedaiwa kuwa bandia amekamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akiwa na vitambulisho bandia vya mwanafunzi wa  Chuo Kikuu cha Muhimbili cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) akisomea Shahada ya Pili.

JICHO LA TATU...


BINTI APIGWA HADI KUFA, MCHUMBA WAKE AKATWA KICHWA KWA KULAZIMISHA KUOANA...

Moja ya miili ya wapenzi hao.
Msichana mmoja wa India ambaye alipigwa hadi kufa na ndugu wa familia yake na rafiki yake wa kiume kukatwa kichwa katika mauaji ya kutisha ya heshima baada ya kuwa wameshawishiwa kurejea kijijini kwao wakifikiri wataruhusiwa kuoana.

Friday, September 20, 2013

MNIGERIA ATWAA TAJI LA SHINDANO LA MREMBO WA KIISLAMU DUNIANI...

Obabiyi Aishah Ajibola (kushoto) akivikwa taji hilo mara baada ya kutangazwa mshindi nchini Indonesia.
Mwanamke wa Nigeria amevishwa taji la Mrembo wa Kiislamu Duniani katika fainali ya shindano hilo la urembo lililoandaliwa na kundi la wanawake kupinga mwenendo wa Miss World kwenye shindano lililofanyika nchini Indonesia.

WATANZANIA WATAKIWA KUOMBA KUSHIRIKI UCHIMBAJI GESI...

Moja ya mitambo ya uchimbaji gesi.
Wizara ya Nishati na Madini imefikia mwafaka na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) katika suala la ugawaji vitalu vya gesi asilia na kukubalika Watanzania washiriki kila hatua na ambao wanataka kuwekeza kwenye sekta hiyo wajitokeze.

RUBANI WA NDEGE YA ABIRIA 180 ASHITAKIWA KWA KULEWA WAKATI WA SAFARI...

Moja ya ndege za shirika hilo ikiwa safarini.
Rubani wa ndege anatarajiwa kupandishwa kizimbani leo baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kuwa amelewa wakati akijiandaa kuongoza ndege hiyo.

JICHO LA TATU...


RAIS KIKWETE KUSAINI MUSWADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA....

Rais Jakaya Kikwete.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, amesema Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013, utasainiwa na Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa uliwasilishwa na kupitishwa bungeni kwa kufuata taratibu na kanuni zinazotakiwa.

Thursday, September 19, 2013

MWANAFUNZI AMCHINJA MWALIMU WAKE DARASANI...

KUSHOTO: Mwalimu Sun Wakang. KULIA: Damu ikiwa imetapakaa darasani muda mfupi baada ya tukio hilo.
Mwanafunzi wa China amemchinja mwalimu wake katika kulipiza kisasi baada ya simu yake ya mkononi kutaifishwa.

MOTO WA UPINZANI WAZIDI KUSHAMIRI NDANI YA CHAMA CHA WALIMU...

Gratian Mukoba.
Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kinazidi kupata upinzani kutoka kwa wanachama wake hasa wa shule za msingi, ambapo sasa imeundwa  Kamati ya Taifa ya Wanachama wa chama hicho ya kudai haki za walimu.

SHAHIDI ADAI BASIL MRAMBA HAKUITAFUTA KAMPUNI YA ALEX STEWART...

Basil Mramba.
Aliyekuwa mfanyakazi wa Benki Kuu (BoT), Kesisia Mbatia (61) ameieleza Mahakama kuwa Waziri wa zamani wa Wizara ya Fedha, Basil Mramba hakuhusika katika mchakato wa kuitafuta kampuni ya kukagua migodi ya madini ya Alex Stewart.

JICHO LA TATU...


Wednesday, September 18, 2013

WATUHUMIWA WALIOINGIZA MABOMU YALIYOTUPWA ARUSHA WAKAMATWA...

Baadhi ya majeruhi wa bomu kwenye mkutano wa hadhara wa Chadema huko Arusha.
Watuhumiwa walioingiza mabomu ya kurushwa kwa mkono yaliyotupwa Arusha Mei na Juni katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti na kwenye mkutano wa wa hadhara wa Chadema, Soweto mkoani Arusha, wamekamatwa.

MWALIMU AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME NDANI YA DARASA...

Diane Krish-Veeramany na wenzake watatu mara baada ya kujifungua salama mtoto wa kiume darasani.
Mwalimu wa shule ya msingi alilazimika kujifungulia ndani ya darasa pale mtoto wake alipotokeza kabla ya wakati, huku wenzake wakifanya kazi kama wakunga.

MCHUNGAJI APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUHIFADHI WAHAMIAJI HARAMU...

Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam.
Mchungaji wa Kanisa la Life Change Chapel lililopo Sinza, Blessing Dangana (36) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kuwahifadhi Raia wa Nigeria waliokuwa wanaishi nchini bila kibali.

WAPANGA KUJIVUA UANACHAMA CWT, KUANZISHA CHAMA KINGINE...

Makao Makuu ya Chama cha Walimu Tanzania.
Walimu wa shule za msingi wilayani Ukerewe, wanajiandaa kuanzisha chama kingine, ili wajitoe uanachama wao katika Chama cha Walimu Tanzania (CWT).

JICHO LA TATU...


Tuesday, September 17, 2013

BALAA!! WAKAMATWA WAKIWA NA LITA 29 ZA TINDIKALI ZANZIBAR...

Kamishna Mkuu, Mussa Ali Mussa.
Siku chache baada ya Padri wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Machui, Anselmo Mwang'amba kumwagiwa tindikali Zanzibar, Polisi  visiwani hapa imekamata  lita 29 za tindikali kwenye magaloni ya ujazo tofauti.