RUBANI WA NDEGE YA ABIRIA 180 ASHITAKIWA KWA KULEWA WAKATI WA SAFARI...

Moja ya ndege za shirika hilo ikiwa safarini.
Rubani wa ndege anatarajiwa kupandishwa kizimbani leo baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kuwa amelewa wakati akijiandaa kuongoza ndege hiyo.

Kapteni huyo wa ndege ya Shirika la Ndege la Kimataifa la Pakistani, iliyokuwa ikitarajia kuruka kutoka Uwanja wa ndege wa Leeds Bradford kwenda Islamabad usiku wa Jumatano, atafikishwa mbele ya hakimu wa Leeds asubuhi hii.
Rubani huyo mwenye miaka 54, kutoka Pakistani, alikamatwa majira ya Saa 4 usiku wa juzi, wakati akifanya ukaguzi kabla ya kuruka katika chumba cha marubani cha ndege aina ya Airbus 310.
Abiria wote 180 waliokuwa kwenye ndege hiyo wakati huo walilazimika kushushwa na kukodishiwa hoteli kwa usiku huo.
Msemaji wa Polisi wa West Yorkshire alisema: "Takribani Saa 4 usiku wa jana polisi waliitwa kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Leeds Bradford ambako walimkamata rubani wa ndege kwa tuhuma za kufanya vitendo visivyokubalika katika shughuli za usafiri wa anga vilivyotokana na ulevi.
"Rubani huyo kwa sasa anashikiliwa na polisi."
Irfan Faiz, miaka 54, kutoka Pakistan, anafikishwa mbele ya hakimu mjini Leeds asubuhi hii akishitakiwa kwa kufanya vitendo visivyokubalika katika shughuli za usafiri wa anga vilivyotokana na ulevi.

No comments: