Mwanajeshi akilinda usalama nje ya jengo hilo. |
Vikosi vya usalama vikiwa tayari kwa mapambano ndani ya jengo hilo. |
Habari tulizopata muda mfupi uliopita zinasema jumla ya watu 59 wamethibitishwa kufariki hadi sasa kufuatia mashambulizi kwenye jengo la Westgate Shopping Mall mjini Nairobi.
Wakati idadi ya vifo ikiongezeka kiasi hicho, watu waliojeruhiwa sasa wamefikia 175 ambapo Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine wa juu wakienda kuwatembelea katika Hospitali za Aga Khan na MP Shah.
Mamlaka husika zimewaamuru waandishi wa habari kuondoka ndani ya jengo hilo kwa usalama wao, huku ikibainishwa kwamba kuna wanamgambo kati ya 10 na 15 wanaowashikilia mateka ndani ya jengo hilo.
Nje ya jengo hilo, polisi wamelazimika kutupa mabomu ya machozi kwa sababu za kiusalama kuwatawanya watu waliokusanyika kwa wingi kushuhudia sakata hilo.
Maduka ya Nakumatt katika jengo hilo la Westgate yameendelea kufungwa kwa siku ya pili mfululizo kutokana na mashambulizi hayo.
No comments:
Post a Comment