Moja ya miili ya wapenzi hao. |
Msichana mmoja wa India ambaye alipigwa hadi kufa na ndugu wa familia yake na rafiki yake wa kiume kukatwa kichwa katika mauaji ya kutisha ya heshima baada ya kuwa wameshawishiwa kurejea kijijini kwao wakifikiri wataruhusiwa kuoana.
Nidhi Barak, miaka 20, mwanafunzi wa sanaa ya uchoraji, na Dharmender Barak, miaka 23, ambaye alikuwa akisoma katika chuo cha ufundi, waliuawa juzi usiku huku wakazi katika kijiji cha Gharnavati kwenye jimbo ya Haryana nchini India wakishuhudia.
Wawili hao walikuwa wametorokea karibu na Delhi Jumanne sababu familia zao hazikuridhia mahusiano yao.
Lakini walishawishiwa kurejea kwa ahadi kwamba hawatadhuriwa na mwishowe wataruhusiwa kuoana.
Wazazi wa Nidhi na mjomba wamekamatwa na polisi sasa wanajaribu kumsaka kaka yake na wanafamilia wengine ambao wamejificha kusikojulikana tangu uhalifu huo.
Kwa mujibu wa polisi wawili hao waliteswa kwa masaa kadhaa nyumbani kwa Nidhi kabla ya kupigwa hadi kufa mbele ya halaiki ya watu.
Dharmender Barak alipigwa na mikono yake na miguu kuvunjwa, kabla ya kukatwa kichwa. Mwili wake ulidaiwa kutekelezwa karibu na nyumba ya familia yao kijijini hapo.
Polisi, ambao walitaarifiwa na mwanakijiji mmoja, waliripotiwa kuikamata familia ya Nidhi ikichoma mwili wake katika kimbwi.
Mwili wake uliochomwa nusu na ule wa Dharmender Barak ilichukuliwa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.
Mkuu wa polisi wa eneo hilo Anil Kumar alisema: "Licha ya kumuua mvulana huyo pia walimkata kichwa.
"Tumewakamata baba yake, mama na mjomba na tunamsaka kaka yake, rafiki yake na dereva wa gari ambalo liliwarejesha nyumbani wawili hao huko kijijini Gharnavati.
"Wote ni wenyeji wa kijiji hicho na ukoo mmoja. Ni mauaji ya heshima lakini mauaji hayo hayakupata baraka za jamii."
India kwa miaka mingi imeshuhudia mauaji yanayolenga wapenzi wenye umri mdogo ambao wana mahusiano ambayo familia zao, ukoo au jamii, hususani katika maeneo ya kimila vijijini, yanakatazwa.
Sababu za kukataliwa ni nyingi, lakini wakati fulani inahusisha kuwa na mahusiano nje ya ukoo wao au dini.
Mauaji hayo hufanywa na ndugu kulinda heshima ya familia na fahari.
Polisi huko Haryana wamekuwa wakifanya kampeni dhidi ya mauaji ya heshima katika jimbo hilo, ambako uwiano wa jinsia ni pungufu kwa wanaume sababu ya sheria zilizopitwa na wakati lakini bado kuna utamaduni wa wanawake kuua watoto wachanga.
"Tunafanya semina na maofisa wetu wa kike kutembelea vijiji lakini silaha kuu shidi ya mauaji haya ya heshima ni (zaidi) elimu," alisema Kumar.
Mahakama Kuu ya India ilisema mwaka 2010 kwamba adhabu ya kifo itatolewa kwa watakaopatikana na hatia ya mauaji ya heshima, akiita uhalifu huo ushenzi 'aibu' kwa taifa hilo.
Hakuna idadi rasmi za matukio ya mauaji ya heshima nchini India, lakini asasi ya All India Democratic Women's Association inasema uchunguzi wake unaonesha kuna takribani matukio 1,000 ya aina hiyo kote nchini humo.
No comments:
Post a Comment