Aunty Ezekiel. |
Mfanyabiashara Ivony Maximilian, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka ya kumjeruhi muigizaji wa filamu Aunty Ezekiel kwa chupa wakiwa klabu Bilicanas.
Ivony (22), alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka yake, mbele ya Hakimu Mkazi Sundi.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, inadaiwa Ivony alitenda kosa hilo, Agosti 18, mwaka huu, katika klabu Bilicanas, iliyopo mtaa wa Makunganya, wilayani Ilala.
Iliendelea kudaiwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa huyo alimjeruhi muigizaji huyo kwa chupa katika mkono wa kushoto na kumsababishia majeraha.
Ivony anayetetewa na Wakili Majura Magafu, alikana shitaka hilo, ambapo mshitakiwa huyo yupo nje kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaofanya kazi katika taasisi zinazotambuliwa kisheria. Kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 21, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment