Monday, September 30, 2013

CHANZO CHA AJALI ILIYOKATISHA UHAI WA DADA WA MBOWE CHATAJWA...

Majeruhi wa ajali hiyo, Zedii Mzuke  na mtoto wake wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Magunga wilayani Korogwe kwa matibabu.
Familia ya Mwenyekiti Chadema Taifa, Freeman Mbowe, imepata pigo baada ya dada wa mwenyekiti huyo, Grace Mbowe, kufariki katika ajali ya gari.

UNYAMA ZAIDI WA MAGAIDI WA AL-SHABAAB WAFICHULIWA WESTGATE SHOPPING MALL...

Mmoja wa magaidi hao akiwaelekezea mtutu wa bunduki wateja kwenye kaunta ya benki ya Diamond Trust ndani ya jengo hilo.
Ilikuwa ni mitutu ya bunduki kila kona ya jengo hilo kama wanavyoonekana magaidi hao wakifanya.
Hili ni tukio la kutisha mmoja wa magaidi  kwenye kituo cha biashara cha Kenya akielekeza mtutu kwa mateka, tayari kwa kuwaua.

MAHAKAMA YA ICC YADAIWA KUPOTEZA HESHIMA BARANI AFRIKA...

Jengo la Makao Makuu ya ICC yaliyoko The Hague, Uholanzi.
Rais Jakaya Kikwete amesema mwenendo wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kuhusu Bara la Afrika na viongozi wake, unainyima Mahakama hiyo nafasi ya kuungwa mkono na bara la Afrika.

JICHO LA TATU...


UMOJA WA MATAIFA WAJIVUNIA UWEZO WA WANAJESHI WA TANZANIA...

Baadhi ya wanajeshi wa Tanzania walioko kwenye majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki moon amemwambia Rais Jakaya Kikwete, kuwa Umoja  huo unajivunia mchango na ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika Brigedi ya Kimataifa ya Kutuliza Hali (FIB) katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Sunday, September 29, 2013

DADA WA FREEMAN MBOWE ALIYEHAMIA CCM AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI...

Grace Mbowe (kushoto) alipokuwa akikabidhiwa kadi ya uanachama wa CCM na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Hassan Mtenga, baada ya kukihama CHADEMA kwa kile alichodai hakuna jambo jipya.
Habari zilizotufikia zinasema kwamba Grace Mbowe na dereva wake, Abrahman Lukindo wamefariki dunia katika ajali mbaya ya gari iliyotokea leo mchana mkoani Tanga.
Grace, ni dada wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.

RUBANI NA MSAIDIZI WAKE WAKIRI KULALA USINGIZI HADI DAKIKA CHACHE KABLA YA KUTUA...

Marubani wakiwa kazini katika chumba chao.
Rubani mmoja jana amekiri kwamba yeye na ofisa wake wa kwanza walilala usingizi wakiwa ndani ya ndege ya mizigo angani - na kuamka dakika chache kabla ya kutua.

KILICHOYAPONZA MAGAZETI YA "MWANANCHI" NA "MTANZANIA" HIKI HAPA...

Assah Mwambene.
Serikali imeyafungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania kutokana na kuandika habari na makala za uchochezi.

MAWAZIRI WANNE KENYA WALIPUUZIA ONYO LA MAGAIDI WA AL SHABAAB...

Moshi ukifuka kwenye jengo la Westgate Shopping Mall, mjini Nairobi.
Mawaziri wanne na Mkuu wa Majeshi wa serikali ya Kenya walionywa kuwa kundi la kigaidi la al-Shabaab linapanga kufanya mashambulizi jijini Nairobi ambapo watavamia jengo na kushikilia  watu mateka.

MSAKO WA WAHAMIAJI HARAMU WAGUNDUA KIJIJI CHA WARUNDI 600...

Issa Machibya.
Kampeni ya kitaifa ya kuondoa wahamiaji haramu nchini iliyopewa jina la Operesheni Kimbunga, imefanikiwa kusambaratisha kijiji cha wahamiaji haramu wa Burundi waliokuwa wamejitengenezea dola yao nchini, kiasi cha hata kutumia sarafu ya Burundi ilihali wakiwa Tanzania.

VICHWA SITA VYA BINADAMU WALIOCHINJWA VYAOKOTWA MTAANI...

Walinzi wakikagua moja ya magari mjini humo.
Vichwa sita vilivyochinjwa vya binadamu vimepatikana kwa zaidi ya siku mbili katika mji mmoja nchini Mexico ambako wakazi wa mjini humo wameunda vikosi vya kujilinda dhidi ya magenge ya matajiri wa dawa za kulevya.

JICHO LA TATU...


Saturday, September 28, 2013

WATUHUMIWA FEDHA ZA EPA WAFUNGWA MIAKA SABA JELA...

Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imewahukumu kifungo cha kati ya mwaka na nusu na saba jela baadhi ya washitakiwa wa wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

SERIKALI YAFUNGIA MAGAZETI YA MWANANCHI NA MTANZANIA...

Serikali imetangaza kuyafungia magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia Septemba 27, mwaka huu kwa kuandika na kuchapisha habari na makala za uchochezi.

MREMBO WA GHANA AFANYA KWELI MISS WORLD 2013, TANZANIA YALE YALE...

Miss World 2013, Megan Young mara baada ya kutangazwa mshindi.
Miss World 2013, Megan Young akiwa na Marine Lorphelin (kushoto) aliyeshika nafasi ya Pili na Carranzar Naa Okailey Shooter aliyeshika nafasi ya tatu.
Wakati mrembo kutoka Philippines, Megan Young akiibuka kidedea Shindano la Miss World 2013, mrembo kutoka Afrika, Miss Ghana Carranzar Naa Okailey Shooter amechomoza kati ya warembo 130 na kushika nafasi ya tatu.

UNYAMA WESTGATE MALL! MATEKA WATOBOLEWA MACHO, WANG'OLEWA PUA NA KUNYOFOLEWA VIDOLE KWA KOLEO..

Askari wa Kenya akijipanga namna ya kutoka...
Ghorofa ya juu ya Westgate Mall baada ya kupigwa kombora na vikosi vya Kenya...
Ghorofa tatu zilizobomolewa kwa kombora...
Uharibifu mkubwa baada ya ghorofa kulipuliwa kwa kombora...
Baadhi ya magari baada ya kuteketea kwa moto juu ya jengo la Westgate Mall...
Sehemu ya maegesho ya magari ndani ya jengo hilo baada ya kupigwa kombira...
Mwili wa mmoja wa waathirika ukiwa umetelekezwa ndani ya jengo hilo.
Askari wamesimulia mateso makali ya kutisha yaliyofanywa na magaidi kwenye jengo la Westgate mjini Nairobi juzi wakidai kuwa mateka walikatwa viungo, macho yao kutobolewa na kutelekezwa wakiwa wamening'inizwa katika vishikizo darini.

JICHO LA TATU...


Friday, September 27, 2013

MTANGAZAJI WA KIKE ASIMULIA ALIVYOJIFANYA AMEKUFA KUWAKWEPA MAGAIDI WESTGATE...

Sneha Kothari Mashru.
Mtangazaji wa kituo cha redio jana ameeleza jinsi alivyonusurika katika shambulio la umwagaji damu nchini Kenya kwa kujigubika katika damu za kijana mmoja ili aonekane kuwa amekufa.

MAGAIDI WALIOTEKA WESTGATE WATUPA SILAHA WASIJULIKANE NA KUTOROKA...

Ghorofa mbili za jengo la Westgate zikiwa zimebomolewa kwa ndani baada ya mlipuko mkubwa uliofuatiwa na moshi mzito.
Maofisa Usalama wa nchi za Magharibi wanahofia kuwa huenda watekaji wengi waliokuwa wakishikilia kituo cha biashara cha Westgate, walitoroka muda mfupi baada ya shambulio, kwa kutupa bunduki zao na kujifanya wateja wa duka hilo, imefahamika.

AJALI ZIWA TANGANYIKA YAUA WATU 16, WAMO WATOTO 13...

Ziwa Tanganyika.
Watu 16, wakiwamo watoto 13 wenye umri chini  ya  miaka mitano, wamekufa maji baada ya mtumbwi  waliokuwa wakisafiria kuzama katika Ziwa Tanganyika.

SAFARI YA ABIRIA WA FASTJET KWENDA SAUZI YAOTA MBAWA...

Moja ya ndege za FastJet.
Abiria waliokuwa wasafiri leo kwa ndege ya Kampuni ya FastJet kwenda Afrika Kusini, wamepigwa na butwaa baada ya safari hiyo kufutwa jana.

BALAA! WASICHANA 55,000 WATIMULIWA SHULENI KWA MIMBA...

Watoto wa kike zaidi ya 55,000 Tanzania Bara, walifukuzwa shule na kutengwa na jamii, baada ya kupata  mimba wakiwa shuleni katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, hatua iliyowaharibia kwa kiasi kikubwa ndoto zao za baadaye.

MWANDISHI WA GAZETI LA MWANANCHI AFARIKI DUNIA...

Marehemu Venance George.
Mwandishi wa habari  wa gazeti la Mwananchi mkoani Morogoro, Venance George aliyekuwa amelazwa kwa muda katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro amefariki dunia.

JICHO LA TATU...


TUME YA KATIBA YAONYA WANASIASA KUSHINIKIZA MASLAHI BINAFSI...

Jaji Joseph Warioba.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ameonya vyama vya siasa kwa kushinikiza maslahi yao kwenye mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya.

Thursday, September 26, 2013

MWANAMKE ANUSURIKA BAADA YA KUMIMINIWA RISASI NA GAIDI WESTGATE SHOPPING MALL...

Patashika katika jengo la Westgate Shopping Mall mjini Nairobi.
Wakati Serikali ya Kenya ikitangaza kukamilisha kazi ya kupambana na magaidi walioteka kituo cha biashara cha Westgate, Nairobi na kufanikiwa kuwaangamiza, mfanyakazi wa moja ya maduka ya kituo hicho, amesema mwanamke anayefanana na Samantha Lewthwaite alimmiminia risasi siku ya tukio.

SENSA 2012 YAFICHUA IDADI KUBWA YA WATANZANIA NI WATOTO...

Baadhi ya watoto wa Kitanzania wakiwa darasani.
Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 inaonesha kuwa sehemu kubwa ya idadi ya watu  nchini ni watoto wenye umri wa chini ya miaka 15 na vijana.

WANAOPINGA MUSWADA WA MABADILIKO YA KATIBA WASHAURIWA KURUDI MEZANI...

Peter Mziray.
Vyama vya siasa vinavyopinga Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba vimeshauriwa kurudi kwenye meza ya mazungumzo vikiaswa kuwa malumbano katika majukwaa ya kisiasa hayawezi kuleta suluhu.

Wednesday, September 25, 2013

MHAMIAJI HARAMU AKUTWA NA LESENI NA KITAMBULISHO CHA KUPIGIA KURA...

Leseni ya udereva.
Baadhi ya wahamiaji haramu, wamekuwa wakitumia mbinu ya kupiga picha na viongozi wa juu wa Serikali na kuzitumia kama ‘kibali’ cha kukaa nchini.

MJANE GAIDI WA UINGEREZA AHOFIWA KUFA UTEKAJI WESTGATE SHOPPING MALL...

Samantha Lewthwaite.
'Mjane Mweupe' Samantha Lewthwaite anawezekana kuwa ameuawa katika utekaji nyara wa Nairobi.

JICHO LA TATU...


MWANAUME AIBA MAITI YA BABA YAKE KWA IMANI AKIMWOMBEA ATAFUFUKA...

KUSHOTO: Vincent Bright. KULIA: Jeneza hilo likiwa nyuma ya gari la Bright baada ya kukamatwa na polisi.
Mtu mmoja aliyeiba maiti ya baba yake kutoka makaburi ya Detroit amewekwa chini ya uangalizi jana na kuamriwa kuhudhuria tiba ya akili ama atafungwa jela.

Tuesday, September 24, 2013

MAPYA YAIBUKA UTEKAJI WESTGATE SHOPPING MALL, MJANE WA KIINGEREZA AHUSIKA...

KUSHOTO: Samantha Lewthwaite. KULIA: Jinsi ilivyokuwa.
Shambulio la kigaidi kwenye kituo cha kibiashara Kenya lililosababisha vifo vya watu 69 liliongozwa na mjane mweupe wa Kiingereza wa mlipuaji mabomu ya 7/7, imedaiwa juzi usiku.
**Serikali jana ilirekebisha taarifa za vifo kwa kusema waliokufa ni 62 na kwamba wengine 63 hawajulikani waliko.**

KANISA LALIPULIWA NA KUUA WAKRISTO 75 NA KUJERUHI 110...

Waumini wakiwa hawajui la kufanya baada ya shambulio hilo kanisani hapo.
Wauaji wawili wa kujitoa mhanga wamelipua mabomu yao nje ya kanisa la kihistoria nchini Pakistan jana na kuua watu 75 kwenye shambulio baya zaidi kuwahi kutokea kwa Wakristo walio wachache wa nchini humo.

JICHO LA TATU...


WASIMULIA MKASA MZIMA WA UTEKAJI WESTGATE SHOPPINGA MALL...

Jengo la Wesgate Shopping Mall mjini Nairobi.
Manusura katika shambulizi la kigaidi katika duka kubwa la Westgate jijini Nairobi, Kenya, wamesimulia mkasa mzima na kusema walivyoshuhudia wateja wenzao katika duka hilo wakiuawa baada ya kubainika kutokuwa Waislamu.

CHAMA MBADALA CHA WALIMU TANZANIA CHAUNGWA MKONO...

Makao Makuu ya Chama cha Walimu Tanzania.
Chama mbadala wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mtandao wa Walimu Tanzania (TTN), ambacho kimesajiliwa, kimeungwa mkono na Kamati ya Taifa ya Wanachama wa CWT.

Monday, September 23, 2013

MAGAIDI WAHOFIWA KUJILIPUA NDANI YA WESTGATE SHOPPING MALL...

Moshi mzito ukifuka ndani ya jengo la Westgate Shopping Mall.
Habari zilizopatikana hivi punde zinasema inahofiwa kuwa magaidi wa Kiislamu wamejilipua wenyewe ndani ya jengo la Westgate Shopping Mall kufuatia mapigano makali.

AL-SHABAAB WATISHIA KUUA MATEKA WOTE WALIOBAKI WESTGATE SHOPPING MALL...

Jengo ambalo mateka hao bado wanashikiliwa ndani yake.
Magaidi wa Kiislamu ambao wameliteka jengo la Westgate Shopping Mall mapema leo wametishia kuua mateka wao wote waliobakia huku vikosi maalumu vikiingia ndani ya jengo hilo kumaliza utekaji huo wa siku mbili ambao umesababisha vifo vya watu 69.