Friday, September 27, 2013

MWANDISHI WA GAZETI LA MWANANCHI AFARIKI DUNIA...

Marehemu Venance George.
Mwandishi wa habari  wa gazeti la Mwananchi mkoani Morogoro, Venance George aliyekuwa amelazwa kwa muda katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro amefariki dunia.

Mwandishi huyo alifariki dunia jana alasiri.
Baba wa marehemu, George Mhangilwa, amesema taratibu za maziko zinasubiri ndugu zake walio nje ya Morogoro.
Waandishi wa habari kadhaa mjini Morogoro wakiwemo na wadau wa habari walikusanyika katika jengo la wodi ya daraja la kwanza alasiri hiyo baada ya kupata taarifa ya kifo hicho na walisubiri hadi saa 11 jioni wakati mwili wake ulipotolewa kwenda kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Msiba huo upo nyumbani kwa marehemu mtaa wa Tubuyu, nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro.

No comments: