Sunday, September 29, 2013

DADA WA FREEMAN MBOWE ALIYEHAMIA CCM AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI...

Grace Mbowe (kushoto) alipokuwa akikabidhiwa kadi ya uanachama wa CCM na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Hassan Mtenga, baada ya kukihama CHADEMA kwa kile alichodai hakuna jambo jipya.
Habari zilizotufikia zinasema kwamba Grace Mbowe na dereva wake, Abrahman Lukindo wamefariki dunia katika ajali mbaya ya gari iliyotokea leo mchana mkoani Tanga.
Grace, ni dada wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.
Kwa mujibu wa mashuhuda, Grace na dereva wake huyo walifariki dunia eneo la tukio kufuatia majeraha makubwa hasa sehemu za kichwani.
Hivi karibuni, Grace alizua gumzo pale alipoamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho ni mpinzani mkubwa wa Chadema kinachoongozwa na kaka yake.
Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.
Taarifa zaidi endelea kuperuzi ziro99blog.

No comments: