![]() |
| Miss World 2013, Megan Young mara baada ya kutangazwa mshindi. |
![]() |
| Miss World 2013, Megan Young akiwa na Marine Lorphelin (kushoto) aliyeshika nafasi ya Pili na Carranzar Naa Okailey Shooter aliyeshika nafasi ya tatu. |
Megan amerithi taji hilo kutoka kwa mrembo wa China, Yu Wenxia aliyefanya hivyo mwaka jana.
Katika shindano hilo lililofanyika mjini Jakarta, Indonesia na kumalizika muda mfupi uliopita, mrembo kutoka Ufaransa, Marine Lorphelin alishika nafasi ya tatu.
Tanzania kama kawaida yake, haikuweza kabisa kufua dafu baada ya mshiriki wake, Brigitte Lyimo kushindwa kufurukuta katika mtanange huo mkali na unaobeba hisia kubwa miongoni mwa wadau wake duniani kote.
Dalili za Miss Ghana kung'ara katika shindano hilo zilizidi kuongezeka hasa kutokana na umahiri wake katika kujibu swali na kujiamini.



No comments:
Post a Comment