![]() |
| Mmoja wa magaidi hao akiwaelekezea mtutu wa bunduki wateja kwenye kaunta ya benki ya Diamond Trust ndani ya jengo hilo. |
![]() |
| Ilikuwa ni mitutu ya bunduki kila kona ya jengo hilo kama wanavyoonekana magaidi hao wakifanya. |
Hili ni tukio la kutisha mmoja wa magaidi kwenye kituo cha biashara cha Kenya akielekeza mtutu kwa mateka, tayari kwa kuwaua.
Mshambulizi huyo, aliyevalia jaketi la maua na kujifunika uso, anaelekeza bunduki yake kwa wateja ndani ya benki moja wakiwa wamelala katika kaunta huku mikono yao ikiwa vichwani.
Picha hizo za kamera ya CCTV zilipigwa ndani ya Benki ya Diamond Trust katika ghorofa ya chini ya jengo la Westgate Shopping Mall katika hatua za awali za balaa la utekaji nyara.
Picha nyingine inaonesha wapiganaji watatu wakionesha silaha zao kwenye lango la kuingilia katika kituo hicho cha biashara, mmoja wao akiwa amevalia vazi la utamaduni wa Kiislamu na kuonesha.....pointing at a figure cowering in the corner.
Katika picha nyingine, wanawake na watoto wanaoneshwa kwenye dari la jengo hilo miongoni mwa miili iliyotapakaa damu ya waliokufa na majeruhi.
Kundi hilo linadhaniwa kujumuisha familia ambazo zilikuwa zinahudhuria maonesho ya mapishi yaliyokuwa yakifanywa na mpishi wa kwenye televisheni Ruhila Adatia-Sood, ambaye alikuwa na mimba ya miezi sita na alifariki katika shambulio hilo.
Waliokolewa baadaye na wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu, ambao waliwasili wakiwa na vitanda vya magurudumu wakati magaidi walipoingia ndani ya jengo hilo.
Kwa wengi ni desturi yao sehemu za maficho ambazo zinatofautisha kati ya kifo na kupona. Baadhi ya picha za kamera za usalama zinaonesha watu hao wenyewe silaha wakipiga risasi kwa bunduki vijichumba vya choo, mara baada ya kubaini kwamba watu walikuwa wamejificha ndani.
Washambulizi wengine walitumia muda wao kuwagawa Waislamu kutoka kwa wasio-Waislamu baada ya kutaka baadhi kukariri Shahada, weledi wa imani ya Kiislamu.
Mtu aliyenaswa ndani ya kituo hicho cha biashara alieleza aliweza kumwona bayana mwanamke akitia tahabibu bunduki ya kudungulia.
Achebe Odida, miaka 42, alielezea jinsi alivyojificha chini ya kaunta ya duka la simu za mkononi wakati mapigano yalipoanza na kuinua kichwa chake dirishani kutazama nje.
"Nilimwona mwanamke aliyevalia kilemba cheusi na shali jeusi juu ya kizibao cha pinki na suruali nyeusi," alisema.
"Wakati wateja wakikimbia na kupiga kelele kote katika jengo hilo, alisogea taratibu na kwa umakini kujibanza nyuma ya nguzo. Alionekana kama mwanamke wa Kisomali, mrefu na mwembamba mwenye ngozi nyeusi."
Alimwona akiweka sawa bunduki yake hiyo kana kwamba anajiandaa kufyatua, lakini hakumwona akimfyatulia risasi yeyote.
Kenya mpaka sasa haijatangaza magaidi wangapi walihusika katika utekaji huo. Wanasema watano waliuawa katika kituo hicho cha biashara na haikufahamika kama watu hao wanane ambao kwa sasa wamekamatwa walishikwa katika eneo la tukio au kwingineko.
Utekaji huo ulivuka mipaka na kugeuka ushikiliaji mateka huku Al-Shabaab wakidai wananchi walikuwa wanashikiliwa lakini kama kulikuwa na mateka, haijafahamika nini kilichowatokea.
Mamlaka za nchini Kenya zimesisitiza kwamba wote waliokufa wamehesabiwa, ingawa Msalaba Mwekundu wanasema inazo ripoti za watu 71 ambao hawajapatikana, pamoja na idadi rasmi ya watu 67.


No comments:
Post a Comment