MAGAIDI WAHOFIWA KUJILIPUA NDANI YA WESTGATE SHOPPING MALL...

Moshi mzito ukifuka ndani ya jengo la Westgate Shopping Mall.
Habari zilizopatikana hivi punde zinasema inahofiwa kuwa magaidi wa Kiislamu wamejilipua wenyewe ndani ya jengo la Westgate Shopping Mall kufuatia mapigano makali.
Vikosi maalumu vimevamia jengo hilo na kuweza kuingia ndani kupitia kwenye paa ili kujaribu kumaliza utekaji huo wa siku tatu, japo waziri mmoja wa serikali ya Kenya alisema kwamba wanamgambo hao wamechoma moto mashuka kadhaa ndani ya duka moja kama mtego.
Muda mfupi uliopita, vikosi hivyo vinasemekana kujikita kwenye mapigano kufa au kupona dhidi ya magaidi hao ambao wameng'ang'ania ndani ya jengo la Westgate Shopping Mall wakiwashikilia mateka zaidi ya 40 tangu Jumamosi.
Mashuhuda wameeleza kusikia milipuko minne mikubwa kutoka kwenye jengo hilo na kufuatiwa na mirindimo ya risasi baada ya jeshi kuvamia humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani Joseph Ole Lenku alisema kwamba magaidi wawili kati ya hao wameuawa na kwamba wengi wa mateka sasa wameachiwa huru. Wanamgambo wote ni wanaume, aliongeza, ingawa baadhi yao walikuwa wamevalia kama wanawake.
Mpaka sasa, watu 69 wamethibitishwa kufa. Takribani watu 175 wamejeruhiwa, wakiwamo watoto.
Moshi mzito mweusi umeonekana kutoka kwenye jengo hilo kufuatia mfululizo wa milipuko mikubwa na majibizano makali ya risasi.
Eneo hilo kuzunguka Westgate Mall lilikuwa limezingirwa na wanajeshi na askari wenye silaha, huku wafanyakazi wa dharura na waandishi walielezwa kujificha.
Mkuu wa Polisi David Kimaiyo alisema baadahi ya mateka wameachiwa huru. Hatahivyo, kundi moja linalodai kuwakilisha magaidi wa Al-Shabaab lilisema bado wanaendelea kupambana ndani ya jengo hilo.

No comments: