AL-SHABAAB WATISHIA KUUA MATEKA WOTE WALIOBAKI WESTGATE SHOPPING MALL...

Jengo ambalo mateka hao bado wanashikiliwa ndani yake.
Magaidi wa Kiislamu ambao wameliteka jengo la Westgate Shopping Mall mapema leo wametishia kuua mateka wao wote waliobakia huku vikosi maalumu vikiingia ndani ya jengo hilo kumaliza utekaji huo wa siku mbili ambao umesababisha vifo vya watu 69.
Mashuhuda walisema walisikia milipuko kadhaa mikubwa ndani ya Westgate Shopping Centre mjini Nairobi na kumekuwa na ripoti za kuwapo milio ya risasi mitaani nje ya jengo hilo.
Moshi mzito mweusi ulionekana baadaye ukifoka kutoka kwenye jengo hilo.
Asubuhi ya leo ilibainika kwamba raia wa Uingereza alipoteza mke na binti yake katika mauaji hayo ya halaiki wakati msanifu majengo aliyeshinda tuzo, mwenye uraia wa Uingereza na Australia naye pia alikuwa miongoni mwa waliokufa.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza ilithibitisha leo kwamba Waingereza wanne sasa wameuawa katika shambulio hilo.
Ross Langdon, miaka 33, aliuawa sambamba na mkewe mjamzito raia wa Uholanzi Elif Yavuz. Mtaalamu huyo wa malaria alikuwa amekabisha wiki mbili tu ajifungue.
Vikosi vya Kenya vimevamia jengo hilo kumaliza utekaji huo lakini msemaji wa kundi hilo la kigaidi al Shabaab, Ali Mohamud Rage alisema katika taarifa iliyotumwa kwenye tovuti ya Kiislamu kwamba wote wanaoshikiliwa ndani 'watahusika na pigo kuu la shinikizo lolote' litakalofanywa na askari dhidi ya wanamgambo hao.
Taarifa hiyo ilisomeka: "Tunawapa mamlaka mujahidina ndani ya jengo hilo kuchukua hatua dhidi ya wafungwa hao watakavyo kwa kadri wanavyobanwa.
"Tunawaambia Wakristo kujisalimisha kwa mujahidina kupata msamaha kwa ajili ya wafungwa wao ambao watapata pigo kuu kutokana na shinikizo lililoelekezwa dhidi ya mujahidina."
Kundi hilo linalohusishwa na Al-Qaeda lilidai kuwa na mawasiliano na wapiganaji waliomo ndani ya jengo hilo na kusema wanamgambo hao walikuwa wakipambana na wote Wakenya na vikosi vya Israeli.

No comments: