KUSHOTO: Vincent Bright. KULIA: Jeneza hilo likiwa nyuma ya gari la Bright baada ya kukamatwa na polisi. |
Mtu mmoja aliyeiba maiti ya baba yake kutoka makaburi ya Detroit amewekwa chini ya uangalizi jana na kuamriwa kuhudhuria tiba ya akili ama atafungwa jela.
Vincent Bright, miaka 49, alinusurika hukumu ya kifungo jela. Alipatikana na hatia Agosti ya kufukua mwili huo.
Bright lazima aendelee kupatiwa tiba ya afya ya akili na kumwonesha ofisa wake uangalizi kwamba anatumia dawa, Jaji wa Mahakama ya Wayne County James Chylinski alisema.
"Kama hufanyi hivyo, nitalazimika kukufunga jela," alisema jaji huyo.
Mnamo Januari, mwili wa Clarence Bright mwenye umri wa miaka 93 ulitoweka kutoka kwenye makaburi ya Gethsemane, muda mfupi baada ya msiba wake lakini kabla jeneza halijafukiwa.
Wanafamilia waliwaongoza polisi kuelekea kwenye mwili huo katika jokofu nyumbani kwa Vincent Bright huko Detroit.
Bright alikamatwa pale polisi walipomkamata ndani ya gari akiwa na jeneza tupu nyuma ya gari hilo.
Polisi wakati huo walisema Bright alikuwa mfuasi wa dini na alikuwa na matumaini baba yake atafufuka na kuishi tena kutokana na maombi.
Aligundulika hakuwa na akili timamu kuweza kukabili mashitaka, lakini afya yake ya kiakili ikaimarika baada ya wiki kadhaa za matibabu na uchunguzi kwenye hospitali za serikali.
"Alipitia kipindi kibaya, misongo mingi ya mawazo. ...Anaendelea vema. Yuko kwenye matibabu," wakili anayemtetea Gerald Karafa alisema nje ya mahakama, akizungumzia vifo vya wazazi wa Bright.
Alisema ilikuwa 'ushahidi binafsi' ambao afya ya kiakili ya Bright ilitawala katika wizi huo.
Bright alikataa kuzungumzia suala hilo nje ya mahakama. Baada ya kukamatwa kwake, alitumikia siku 225 jela au mahabusu katika hospitali za serikali.
Dhamana yake ilipangwa kuwa Dola za Marekani 75,000 hivyo mchanganuo wa afya ya akili unaweza kukamilika, ambao utaweka kumkuta akiwa tayari kukabili mashitaka.
Endapo atapatikana na hatia ya kufukua mwili, Vincent Bright anaweza kukabiliwa na kifungo cha hadi miaka 10 jela, kama hangekuwa amewekwa chini ya uangalizi kwa matatizo ya akili.
No comments:
Post a Comment