Picha mbalimbali za Fabrice Muamba akiwa uwanjani kabla ya matatizo kumkumba.
Nyota wa zamani wa timu ya soka ya Arsenal, Thierry Henry wiki iliyopita alifanya kile alichokusudia kwa kumtembelea Fabrice Muamba kwa masaa kadhaa hospitalini kwa siri. Henry alitumia mlango wa nyuma kuingia Hospitali ya Kifua ya London kumuona rafiki yake wa karibu na mchezaji mwenzake wa zamani Arsenal na kisha kupanda tena ndege kurejea Marekani.Saturday, March 31, 2012
MAPACHA WA RANGI TOFAUTI WAFIKISHA MIAKA SABA...
Mmoja ni mweusi mwenye macho ya kahawia. Mwingine ni mweupe mwenye macho ya bluu.
Wana aina moja ya tabasamu, lakini ukiwatazama kwa umakini kuna tofauti ndogo sana. Ila wanafanana.
Ukweli ni kwamba, Kian na Remee ni mapacha, wamezaliwa wakipishana dakika moja tu.
Uzao wa mapacha wa aina hii hutokea mara moja kati ya milioni ya mseto wa chembechembe wa wazazi wao.
Mama Kylee Hodgson na baba Remi Horder wote wamezaliwa kwenye mchanganyiko wa mama weupe na baba weusi.
Mchanganyiko huo ndio uliozalisha seti ya mabinti wawili wazuri.
Kwa mara ya kwanza waliweza kuvuta hisia za watu mbalimbali duniani pale walipotikea kwenye gazeti la Mail wakiwa na umri wa chini ya mwaka mmoja.
Sasa wakiwa wanakaribia kutimiza miaka saba, hawajawahi kuhoji kwanini hawafanani rangi wala hawajawahi kukwaruzana.
“Wamekuwa ni mfano wa inavyotakiwa kuwa,” anasema mama yao. “Imekuwa haiwasumbui kuona hawafanani rangi zao za ngozi. Limekuwa sio jambo kubwa kwani kila mmoja anachukulia kama ilivyo.
Kian na mwenzake aliyezaliwa sekunde 60 baadaye walizaliwa Aprili, 2005 kwa oparesheni.
Mama yao, Kylee mwenye miaka 25 sasa anakumbukia alipowaona kwa mara ya kwanza. “Niligundua kuwa wote wana macho mazuri ya bluu,” alisema.
“Lakini nywele za Remee zilikuwa nyeupe, za Kian zilikuwa nyeusi na ngozi yake pia ilikuwa nyeusi. Kwangu mimi, walikuwa ni watoto wangu na walikuwa kawaida tu. Nilifikiri watafanana hivyo kadri wanavyoendelea kukua.
Punde, hata hivyo, tofauti zao zikaanza kujitokeza. Macho ya Kian yakabadilika rangi na ngozi yake ikazidi kuwa nyeusi. Mchanganyiko wa Remee ukazidi kuwa angavu huku nywele zake zikaendelea kuwa nyeupe.
“Watu wanaweza kuuliza kwanini nawavalisha mavazi yanayofanana,” anasema Kylee. “Ninawajibu: Sababu ni mapacha,” na kuwaachia watu wafanyie kazi. Ilinitatiza mara ya kwanza, lakini kila mtu eneo ninaloishi anaelewa walikuwa mapacha na kukubali hilo. Ni wageni ama watu kutoka mbali ndio hawakufahamu hilo.”
Licha ya kuchangia vitu vingi, mapacha hao wameshaanza kuwa na maamuzi yao binafsi kwa kila mmoja kufanya kitu vile anavyopenda mwenyewe.
CHEKA TARATIBU...
Koplo wa kambi moja ya jeshi iliyoko Dar es Salaam alikuwa kwenye mihangaiko yake ya kusaka chakula kwa ajili ya mifugo yake nyumbani. Kutokana na haraka aliyokuwa nayo alipotoka kazini, akabadili suruali tu na juu akasahau na kuvaa sare ya jeshi iliyosomeka wazi JWTZ. Akiwa njiani kurudi nyumbani akakutana na afande mwenye cheo cha meja. Akamsimamisha na kumuuliza, “Aroo, mbona umevaa sare za cheshi kwenye shughuli zako pinafsi?” Yule Koplo huku akichuruzika jasho na mzigo wake begani akajibu, “Hapana afande hii sio sare ya jeshi.” Afande kwa ukali akasema, “Inamaana unanifanya kipofu, si hapo imeandikwa JWTZ?” Koplo akajibu, “Ooh, hiki ni kifupisho cha majina yangu. Naitwa Januari Wendere Tanslausi Zakaria.” Yule afande akabaki mdomo mwaaaa…
FABRICE MUAMBA ATUMA PICHA "KUTOKA KUZIMU"
PICHA YA JUU: Fabrice Muamba akiwa amekaa kitandani hospitalini. CHINI: Ujumbe mbalimbali wa kumtakia afya njema Muamba. Ujumbe wa kushoto unasomeka "Tunashukutu kwa msaada wako kwa Fabrice" na ule wa kulia inasomeka "Tunaungana kwa ajili ya Fabrice"
Ni picha ambayo dunia nzima ilikuwa ikingoja kwa hamu kuiona.
Fabrice Muamba ameketi kwenye kitanda chake hospitalini akiwa ameachia tabasamu tamu takribani wiki mbili tangu aanguke uwanjani muda mfupi kabla ya mapumziko.
Mchumba wa mchezaji huyo, Shauna Magunda ametuma picha kwenye mtandao wa Twitter jana kuwashukuru mamilioni ya mashabiki ambao waliungana naye kumwombea Muamba ambaye moyo wake ulikuwa ukikaribia kuacha kufanya kazi.
Picha inamuonesha nyota huyo wa Bolton akiwa amevalia jaketi la bluu huku akiwa ameegemea kitanda chake hospitalini hapo. Tabasamu lake linaashiria maendeleo mazuri ya afya yake tangu siku ya mechi Machi 17.
Shauna aliandika pembeni ya picha: “Fab amenitaka niwatumie wote picha hii na kwa niaba yake nawashukuru sana kwa msaada wenu.”
Picha hiyo imevuta hisia kali kutoka kwa mashabiki kwenye mtandao huo wa kijamii.
Shabiki mmoja aliandika: “Mungu akubariki Fabrice. Endelea kupambana, kijana. Nakuombea upone haraka.”
Moyo wa Muamba ulisimama kufanya kazi kwa zaidi ya saa moja wakati madaktari akiwamo mtaalamu wa magonjwa ya moyo aliyeingia uwanjani kujitahidi kupigania uhai wa mchezaji huyo.
Alikimbizwa Hospitali ya Kifua ya mjini London, ambako alitembelewa na wachezaji wenzake wa Bolton na makundi ya wapenzi wa soka.
Baadaye ilibainika kuwa baada ya kushituliwa kwa mashine maalumu mara 15, mchezaji huyo ndipo akaanza kuonesha dalili za uhai.
Tukio hilo limeistusha jamii ya wapenda soka na wengineo ambao wameonesha kuguswa yaliyomsibu mchezaji huyo mwenye miaka 23, huku familia yake ikiwaomba mashabiki wamuombee.
Picha hiyo itakuwa faraja kubwa kwa jamii ya wapenda soka ambao wamekuwa wakifuatia kwa ukaribu maendeleo ya afya ya kijana huyo. Anaonekana atachukua muda mrefu kuwa nje ya uwanja kwa ajili ya matibabu kabla hajarudi kucheza tena.
Wakati huohuo, mwanafunzi aliyetuma ujumbe wa kuchekelea ‘kifo’ cha Muamba kwenye mtandaio wa Twitter, ameshindwa rufani yake na hivyo anakwenda lupango kutumikia adhabu yake ya kifungo cha siku 56 jela.
Liam Stacey mwenye miaka 21, pia anakabiliwa na adhabu ya kufukuzwa chuo kutokana na ubaguzi wake huo aliofanya dhidi ya Muamba. Alikuwa mwaka wa mwisho Chuo Kikuu cha Swansea akisomea digrii ya baiolojia.
POLISI WADAI KUKUTA COCAINE CHUMBANI KWA WHITNEY...
Kizungumkuti cha kifo cha mwanamuziki Whitney Houston kimeendelea baada ya jana polisi kuibuka na kutoa taarifa kwamba walikuta dawa za kulevya chumbani alimopanga mwanamuziki huyo kwenye Hoteli ya Beverly Hills, imefahamika.
Taarifa hizo zimekuja siku chache baada tya taarifa nyingine kudai kuwa askari upelelezi hawakufanikiwa kukuta dawa zozote chumbani humo na kwamba hata mashuka yaliondolewa mara baada ya kifo cha Whitney.
Kuhusu kiasi cha dawa za kulevya aina ya cocaine kilichokutwa, nyaraka rasmi zinaonesha mojawapo ya vitu vilivyokutwa chumbani ni “unga fulani mweupe kama poda.” Vyanzo vya habari vimesema poda hiyo ilipimwa na kugundulika kuwa dawa za kulevya aina ya cocaine.
Imeelezwa kuwa wapelelezi wa Beverly Hills hawachunguzi tetesi za kwamba kuna mtu ameondoa dawa za kulevya chumbani, sababu wanaamini kuwa hazikuondolewa.
Vyanzo vya habari vinavyoshirikishwa kwenye uchunguzi huo vilisema hapo kabla…hakuna dawa zozote zilizokatazwa kisheria zimekutwa chumbani.
Lakini baadaye vyanzo hivyo vikaeleza kuwa hawakujua kama dawa hizo za kulevya zilikuwemo chumbani humo wakati wakifanya uchunguzi mwanzoni.
Kwa sasa askari wako katika hatua za mwisho za uchunguzi wao, lakini hawalengi kuchunguza mtu anayewezekana kuwa aliondoa dawa za kulevya, sababu vitu hivyo kwa sasa viko katika himaya yao.
Kwa sasa askari wako katika hatua za mwisho za uchunguzi wao, lakini hawalengi kuchunguza mtu anayewezekana kuwa aliondoa dawa za kulevya, sababu vitu hivyo kwa sasa viko katika himaya yao.
Friday, March 30, 2012
SIPATI PICHA IKITOKEA AJALI YA MOTO HAPA...
Nyumba zikiwa zimesongamana kwenye maeneo ya bonde la Kinondoni Mkwajuni bila kufikiria siku moja inaweza kutokea ajali ya moto ama kupata mgonjwa wa ghafla na hivyo gari kukosa njia ya kufika kwa urahisi. Siamini kama wakazi hawa walipimiwa viwanja hivi. Jamani hata kama kujenga, basi acheni nafasi ya kupita magari! Ni mtazamo tu, msinikasirikie! (Picha na ziro99blog).
FOLENI DAR ES SALAAM JIONI YA LEO ILIKUWA HIVI...
Magari yakiwa yamesongamana kwenye Barabara ya Nyerere maeneo ya Banda la Ngozi kutokea Uwanja wa Ndege kuelekea katikati ya Jiji jioni hii.
Msururu mrefu wa magari kama unavyoonekana pichani yakiwa yamekwama kwenye Barabara ya Kawawa eneo la bonde la Mkwajuni yakitokea Magomeni kuelekea Kinondoni muda mfupi uliopita. (Picha zote na ziro99blog)
Msururu mrefu wa magari kama unavyoonekana pichani yakiwa yamekwama kwenye Barabara ya Kawawa eneo la bonde la Mkwajuni yakitokea Magomeni kuelekea Kinondoni muda mfupi uliopita. (Picha zote na ziro99blog)
UHABA WA PETROLI SIO KWETU TU, HATA UINGEREZA LIPO...
SIJUI NAO WANAFICHA MAFUTA? Moja ya vituo vha mafuta nchini Uingereza kikiwa kimewekwa matangazo yanayosema, "Samahani, Hakuna Dizeli. Tunasubiri Mafuta" na lingine "Samahani, Hakuna Petroli. Tunasubiri Mafuta".
KAMA BONGO! Hata vituo vichache vilivyokuwa na mafuta, kulikuwa na msongamano mkubwa sana wa magari.
KAAZI KWELI KWELI! Misururu ya magari ikisubiri huduma ya mafuta kwenye moja ya vituo vilivyobahatika kuwa na bidhaa hiyo nchini Uingereza.
KAMA HUKO HALI HIVI, HUKU JE? Kituo cha Mafuta cha ESSO nacho kikiweka tangazo la kwamba wanasubiria mzigo wa mafuta.
KAMA BONGO! Hata vituo vichache vilivyokuwa na mafuta, kulikuwa na msongamano mkubwa sana wa magari.
KAAZI KWELI KWELI! Misururu ya magari ikisubiri huduma ya mafuta kwenye moja ya vituo vilivyobahatika kuwa na bidhaa hiyo nchini Uingereza.
KAMA HUKO HALI HIVI, HUKU JE? Kituo cha Mafuta cha ESSO nacho kikiweka tangazo la kwamba wanasubiria mzigo wa mafuta.
KUTANA NA MBWA AJIZOLEA UMAARUFU KWENYE INTANETI...
Video hapo juu inamuonesha mbwa Chuck the Boxer alipompa mapokezi mazito bosi wake.
Mbwa anayefahamika kwa jina la Chuck the Boxer kwa haraka amekuwa nyota kwenye intaneti baada ya video yake ya pili kumuonesha akimkaribisha nyumbani mmiliki wake.
Huku ikitazamwa zaidi ya mara 1,600,000 tangu ibandikwe kwenye mtandao Machi 22, mbwa huyo mwenye rangi ya kahawia na mabaka meupe alionekana kufanya kile kilichotafrsiriwa kama kumpokea rafiki yake mkubwa.
Gari lenye namba zinazoanzia na BB, iliashiria kwamba tukio hilo lilitokea mji wa Böblingen, Ujerumani jirani na Makao Makuu ya Jeshi la Ulaya.
Yakisikika maneno, "Baba karudi nyumbani!", kutoka kwa mke wa askari huyo, Katie, mbwa huyo kwa haraka akagungua kinachoendelea na kwa kasi ya ajabu akaruka kutoka kwenye gari na kumkimbilia bosi wake, Nick.
Baada ya hapo, akabaki akimtazama kwa takribani sekunde 59 huku mbwa akionyesha wazo furaha ya kumwona tena nyumbani bosi wake nyumbani baada ya majukumu ya kijeshi.
"Ni miezi minane," alisema Katie.
Katika moja ya vituko hapo, mbwa huyo alithibitisha jina lake la Boxer (Bondia) baada ya kugonga miwani ya jua ya Nick kwa kutumia pua yake.
Katika kuonesha wivu kwa jinsi mbwa alivyopewa umuhimu mkubwa, mke wa askari huyo alitania kwa kusema, "Amekupa mapokezi ya muda mrefu kuliko nilivyofanya mimi."
Lakini nani wa kumlaumu Nick kwa kutumia muda wake mwingi kucheza wakati mbwa waliyetengana naye akionesha furaha kubwa ya kumuona tena bosi wake?
Hii si mara ya kwanza kwa mbwa huyo kuwa kufanya vituko kwenye video zinazovuta hisia.
Mwaka jana, mbwa huyo alipata umaarufu mkubwa kwa mara ya kwanza baada ya kumpa mapokezi Nick Februari, 2011.
USAFIRI KAFIRI...
Abiria wakisubiri usafiri wa kuelekea mjini kwenye kituo cha mabasi yanayoelekea upande mwingine eneo la Buguruni Sokoni, Dar es Salaam leo asubuhi. Kutokana na shida ya usafiri wa kwenda katikati ya jiji, abiria hulazimika kusimama ng'ambo ya barabara na kuvizia mabasi yanapogeuka kurudi mjini jambo ambalo ni la hatari kwa usalama wao. (Picha na ziro99blog).
KAZI KAPATA, USALAMA WAKE JE...?
Mama huyu anayefanya kazi ya kufagia barabara akijiandaa kuvuka Barabara ya Kawawa leo asubuhi maeneo ya Ilala Bomba jirani na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Ni kweli kazi amepata, lakini usalama wake uko mashakani kutokana na kukosa vifaa muhimu vya kazi. Hana buti, vifaa vya kujikinga na vumbi na hata vikombe maalumu vya alama ya barabarani kumkinga na magari wakati akitekeleza majukumu yake. Wahusika mpooo...? (Picha na ziro99blog).
TAKA ZINAPOBEBWA NA 'TAKA'...
Hivi nani kasema gari la kusomba taka lazima liwe chakavu? Pichani, lori linalofanya kazi ya kuzoa taka likikatiza enero la Kinondoni Mkwajuni, Dar es Salaam leo asubuhi katika safari zake za kawaida za kubeba taka. Pata picha lilivyochoka na mzigo lililobeba ndio maana nashawishika kusema, "Taka zimebebwa na Taka". (Picha na ziro99blog).
"BORA PUNDA AFE MZIGO UFIKE..."
Akinamama wakipita na vifurushi kichwani mbele ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam leo asubuhi baada ya kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali kwenye soko la Ilala.
Mwendesha baiskeli ya miguu mitatu maarufu kama guta akipita katikati ya barabara maeneo ya Amana, Ilala, Dar es Salaam leo asubuhi. Usafiri huu umekuwa maarufu sana kwa kubeba mizigo kama inavyoonekana pichani.
Waendesha baiskeli aina ya guta wakisukuma baiskeli hizo kutokana na mzigo mzito waliobeba kutokea soko la Ilala leo asubuhi. Uendeshaji huu wa baiskeli haukubaliki kwa usalama barabarani kwa umekuwa kero kwa watumiaji wengine wa barabara na moja ya chanzo cha foleni kubwa za magari.
Jamaa hawa wakiwa wamestarehe kwenye masofa yaliyopakiwa kwenye pikipiki ya miguu mitatu aina ya Toyo kwenye Barabara ya Kawawa maeneo ya Msimbazi Center leo asubuhi. Usalama wao je? (Picha zote na ziro99blog).
Mwendesha baiskeli ya miguu mitatu maarufu kama guta akipita katikati ya barabara maeneo ya Amana, Ilala, Dar es Salaam leo asubuhi. Usafiri huu umekuwa maarufu sana kwa kubeba mizigo kama inavyoonekana pichani.
Waendesha baiskeli aina ya guta wakisukuma baiskeli hizo kutokana na mzigo mzito waliobeba kutokea soko la Ilala leo asubuhi. Uendeshaji huu wa baiskeli haukubaliki kwa usalama barabarani kwa umekuwa kero kwa watumiaji wengine wa barabara na moja ya chanzo cha foleni kubwa za magari.
Jamaa hawa wakiwa wamestarehe kwenye masofa yaliyopakiwa kwenye pikipiki ya miguu mitatu aina ya Toyo kwenye Barabara ya Kawawa maeneo ya Msimbazi Center leo asubuhi. Usalama wao je? (Picha zote na ziro99blog).
AJIFYATULIA RISASI USONI NA KUSAMBARATISHA KILA KITU...
Richard Norris alivyokuwa kabla na baada ya tukio (picha ya chini). Picha kubwa ni madaktari wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Mwanaume mwenye miaka 37 aliyejijeruhi vibaya kwa bunduki mwaka 1997 amepatiwa sura mpya, meno, ulimi na taya katika kile madaktari walichokiita upasuaji mgumu kabisa wa upandikizaji sura mpya kuwahi kufanyika.
Maofisa kutoka kituo cha tiba cha Chuo Kikuu cha Maryland wametangaza juzi kuwa Richard Lee Norris anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji uliochukua saa 36 wiki iliyopita.
Ameanza kupata hisia kwenye uso wake na tayari ameanza kupiga mswaki na hata kunyoa ndevu.
Pia ameanza kuhisi harufu, kitu ambacho alikuwa akishindwa kufanya mara baada ya ajali hiyo.
Kwa miaka 15, Norris amekuwa akiishi kwa shida huku akificha uso wake kwa kuvaa kinyago na kutoka nje nyakati za usiku tu.
Upandikizaji huo utamrejeshea hamu ya kuishi, amesema Dk. Eduardo Rodriguez, kiongozi wa jopo la madaktari waliofanya zoezi hilo la upasuaji.
“Inashangaza unapomuangalia. Ni vigumu kuamini.
“Kabla, watu walikuwa wakimshangaa Norris sababu amevaa kinyago na walikuwa na hamu ya kuona anachoficha,” anasema Rodriguez.
“Sasa, wana sababu nyingine ya kumshangaa, na hakika inashangaza.”
Wapasuaji wanaita ni upandikizaji sura endelevu duniani ambao umemuwezesha mwanaume huyo wa Virginia kuvua kinyago baada ya miaka 15 na kutembea kwa kujiamini.
Wakati alipojipiga risasi mwenyewe usoni mwaka 1997, aling’oa pua yake, midomo na kila kitu mdomoni mwake. Alilazimika kupata jitihada za ziada kuokoa maisha yake, lakini hakuna iliyofanikiwa kama hii ya sasa.
Alipatiwa sura mpya kutoka kwa mchangiaji asiyefahamika wiki iliyopita ambaye viungo vyake vimesaidia maisha ya wagonjwa wengine watano siku hiyohiyo.
Siku sita baada ya upasuaji huo, anaweza kuchezesha ulimi wake, kufumba na kufumbua macho na afya yake inaimarika kwa kasi kuliko madaktari walivyotarajia.
“Hakika kwa sasa anajitazama kwenye kioo akinyoa na kupiga mswaki meno yake, jambo ambalo hatukulitegemea,” anasema Dk. Eduardo Rodriguez, Profesa Shule ya Tiba katika Chuo Kikuu cha Maryland na kiongozi wa jopo la madaktari waliofanya upasuaji huyo, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Wakati Norris alipofungua macho yake siku ya tatu baada ya upasuaji huku familia yake ikiwa imemzunguka kitandani, alitaka ajitazame kwenye kioo.
“Akaweka kioo chini na kunishukuru huku akinikumbatia,” anasema Dk. Rodriguez.
Upandikizaji sura kwa Norris unaonekana kuwa ni wa mafanikio zaidi kwa sasa kufuatia picha na video zilizosambazwa kwa vyombo vya habari katika mkutano huo. Anaendelea kupata nafuu na bado yuko hospitalini hivyo hakuweza kuhudhuria mkutano huo.
Kuhakikisha Norris anafanya shughuli zote kama kawaida, madaktari wamempatia ulimi utakaomuwezesha kutamka maneno, kula na kumung’unya, mpangilio sahihi wa meno, na kuunganisha mishipa yake ya fahamu itakayomuwezesha kutabasamu.
Upandikizaji sura kwa Norris umekuwa wenye mafanikio zaidi kuwahi kutokea kwenye miji ya Forth Worth, Texas na Boston, Massachusetts mwaka jana.
Amekuwa wa kwanza kufanyiwa upandikizaji wa sura nzima katika Marekani na kuweza kuendelea kuona bila matatizo.
Operesheni ya kwanza ya kupandikiza sura nzima ulifanyika Ufaransa mwaka 2005 kwa mwanamke aliyeng’atwa na mbwa wake. Kliniki ya Cleverland ilifanya upandikizaji sura nzima wa kwanza katika Marekani mwaka 2008.
Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo imekuwa ikifadhili sura na upasuaji mikono wenye lengo la kusaidia wanajeshi wake wanaojeruhiwa vitani.
Zaidi ya askari 1,000 wamepoteza mkono au mguu nchini Afghanistan ama Irak, na serikali inakadiria zaidi ya askari 200 watalazimika kupandikiziwa sura.
Subscribe to:
Posts (Atom)