Mmoja ni mweusi mwenye macho ya kahawia. Mwingine ni mweupe mwenye macho ya bluu.
Wana aina moja ya tabasamu, lakini ukiwatazama kwa umakini kuna tofauti ndogo sana. Ila wanafanana.
Ukweli ni kwamba, Kian na Remee ni mapacha, wamezaliwa wakipishana dakika moja tu.
Uzao wa mapacha wa aina hii hutokea mara moja kati ya milioni ya mseto wa chembechembe wa wazazi wao.
Mama Kylee Hodgson na baba Remi Horder wote wamezaliwa kwenye mchanganyiko wa mama weupe na baba weusi.
Mchanganyiko huo ndio uliozalisha seti ya mabinti wawili wazuri.
Kwa mara ya kwanza waliweza kuvuta hisia za watu mbalimbali duniani pale walipotikea kwenye gazeti la Mail wakiwa na umri wa chini ya mwaka mmoja.
Sasa wakiwa wanakaribia kutimiza miaka saba, hawajawahi kuhoji kwanini hawafanani rangi wala hawajawahi kukwaruzana.
“Wamekuwa ni mfano wa inavyotakiwa kuwa,” anasema mama yao. “Imekuwa haiwasumbui kuona hawafanani rangi zao za ngozi. Limekuwa sio jambo kubwa kwani kila mmoja anachukulia kama ilivyo.
Kian na mwenzake aliyezaliwa sekunde 60 baadaye walizaliwa Aprili, 2005 kwa oparesheni.
Mama yao, Kylee mwenye miaka 25 sasa anakumbukia alipowaona kwa mara ya kwanza. “Niligundua kuwa wote wana macho mazuri ya bluu,” alisema.
“Lakini nywele za Remee zilikuwa nyeupe, za Kian zilikuwa nyeusi na ngozi yake pia ilikuwa nyeusi. Kwangu mimi, walikuwa ni watoto wangu na walikuwa kawaida tu. Nilifikiri watafanana hivyo kadri wanavyoendelea kukua.
Punde, hata hivyo, tofauti zao zikaanza kujitokeza. Macho ya Kian yakabadilika rangi na ngozi yake ikazidi kuwa nyeusi. Mchanganyiko wa Remee ukazidi kuwa angavu huku nywele zake zikaendelea kuwa nyeupe.
“Watu wanaweza kuuliza kwanini nawavalisha mavazi yanayofanana,” anasema Kylee. “Ninawajibu: Sababu ni mapacha,” na kuwaachia watu wafanyie kazi. Ilinitatiza mara ya kwanza, lakini kila mtu eneo ninaloishi anaelewa walikuwa mapacha na kukubali hilo. Ni wageni ama watu kutoka mbali ndio hawakufahamu hilo.”
Licha ya kuchangia vitu vingi, mapacha hao wameshaanza kuwa na maamuzi yao binafsi kwa kila mmoja kufanya kitu vile anavyopenda mwenyewe.
No comments:
Post a Comment