CHEKA TARATIBU...

Koplo wa kambi moja ya jeshi iliyoko Dar es Salaam alikuwa kwenye mihangaiko yake ya kusaka chakula kwa ajili ya mifugo yake nyumbani. Kutokana na haraka aliyokuwa nayo alipotoka kazini, akabadili suruali tu na juu akasahau na kuvaa sare ya jeshi iliyosomeka wazi JWTZ. Akiwa njiani kurudi nyumbani akakutana na afande mwenye cheo cha meja. Akamsimamisha na kumuuliza, “Aroo, mbona umevaa sare za cheshi kwenye shughuli zako pinafsi?” Yule Koplo huku akichuruzika jasho na mzigo wake begani akajibu, “Hapana afande hii sio sare ya jeshi.” Afande kwa ukali akasema, “Inamaana unanifanya kipofu, si hapo imeandikwa JWTZ?” Koplo akajibu, “Ooh, hiki ni kifupisho cha majina yangu. Naitwa Januari Wendere Tanslausi Zakaria.” Yule afande akabaki mdomo mwaaaa…

No comments: