Friday, March 30, 2012

KUTANA NA MBWA AJIZOLEA UMAARUFU KWENYE INTANETI...

Video hapo juu inamuonesha mbwa Chuck the Boxer alipompa mapokezi mazito bosi wake.

Mbwa anayefahamika kwa jina la Chuck the Boxer kwa haraka amekuwa nyota kwenye intaneti baada ya video yake ya pili kumuonesha akimkaribisha nyumbani  mmiliki wake.
Huku ikitazamwa zaidi ya mara 1,600,000 tangu ibandikwe kwenye mtandao Machi 22, mbwa huyo mwenye rangi ya kahawia na mabaka meupe alionekana kufanya kile kilichotafrsiriwa kama kumpokea rafiki yake mkubwa.
Gari lenye namba zinazoanzia na BB, iliashiria kwamba tukio hilo lilitokea mji wa Böblingen, Ujerumani jirani na Makao Makuu ya Jeshi la Ulaya.
Yakisikika maneno, "Baba karudi nyumbani!", kutoka kwa mke wa askari huyo, Katie, mbwa huyo kwa haraka akagungua kinachoendelea na kwa kasi ya ajabu akaruka kutoka kwenye gari na kumkimbilia bosi wake, Nick.
Baada ya hapo, akabaki akimtazama kwa takribani sekunde 59 huku mbwa akionyesha wazo furaha ya kumwona tena nyumbani bosi wake nyumbani baada ya majukumu ya kijeshi.
"Ni miezi minane," alisema Katie.
Katika moja ya vituko hapo, mbwa huyo alithibitisha jina lake la Boxer (Bondia) baada ya kugonga miwani ya jua ya Nick kwa kutumia pua yake.
Katika kuonesha wivu kwa jinsi mbwa alivyopewa umuhimu mkubwa, mke wa askari huyo alitania kwa kusema, "Amekupa mapokezi ya muda mrefu kuliko nilivyofanya mimi."
Lakini nani wa kumlaumu Nick kwa kutumia muda wake mwingi kucheza wakati  mbwa waliyetengana naye akionesha furaha kubwa ya kumuona tena bosi wake?
Hii si mara ya kwanza kwa mbwa huyo kuwa kufanya vituko kwenye video zinazovuta hisia.
Mwaka jana, mbwa huyo alipata umaarufu mkubwa kwa mara ya kwanza baada ya kumpa mapokezi Nick Februari, 2011.

No comments: