POLISI WADAI KUKUTA COCAINE CHUMBANI KWA WHITNEY...


Kizungumkuti cha kifo cha mwanamuziki Whitney Houston kimeendelea baada ya jana polisi kuibuka na kutoa taarifa kwamba walikuta dawa za kulevya chumbani alimopanga mwanamuziki huyo kwenye Hoteli ya Beverly Hills, imefahamika.
Taarifa hizo zimekuja siku chache baada tya taarifa nyingine kudai kuwa askari upelelezi hawakufanikiwa kukuta dawa zozote chumbani humo na kwamba hata mashuka yaliondolewa mara baada ya kifo cha Whitney.
Kuhusu kiasi cha dawa za kulevya aina ya cocaine kilichokutwa, nyaraka rasmi zinaonesha mojawapo ya vitu vilivyokutwa chumbani ni “unga fulani mweupe kama poda.” Vyanzo vya habari vimesema poda hiyo ilipimwa na kugundulika kuwa dawa za kulevya aina ya cocaine.
Imeelezwa kuwa wapelelezi wa Beverly Hills hawachunguzi tetesi za kwamba kuna mtu ameondoa dawa za kulevya chumbani, sababu wanaamini kuwa hazikuondolewa.
Vyanzo vya habari vinavyoshirikishwa kwenye uchunguzi huo vilisema hapo kabla…hakuna dawa zozote zilizokatazwa kisheria zimekutwa chumbani.
Lakini baadaye vyanzo hivyo vikaeleza kuwa hawakujua kama dawa hizo za kulevya zilikuwemo chumbani humo wakati wakifanya  uchunguzi mwanzoni.
Kwa sasa askari wako katika hatua za mwisho za uchunguzi wao, lakini hawalengi kuchunguza mtu anayewezekana kuwa aliondoa dawa za kulevya, sababu vitu hivyo kwa sasa viko katika himaya yao.

No comments: