Tuesday, July 2, 2013

JICHO LA TATU...


BINTI AKATWA MKONO KWA KUSHUHUDIA MDOGO WAKE AKITEKWA...

Mji lilikotokea shambulio hilo.
Genge moja nchini India limekata mkono wa binti mmoja mwenye miaka minane kwa kutumia fyekeo huku familia yake ikijaribu kuhakikisha kuachiwa kwa kaka yake aliyetekwa nyara.

Monday, July 1, 2013

OBAMA AWASILI DAR, APANGA KUKUTANA NA BUSH UBALOZINI KESHO...

Rais Barack Obama akishindwa kujizuia na kusakata moja ya ngoma za asili mbele ya mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam Terminal 1 mapema leo.
Rais Barack Obama akifurahia ngoma ya kabila la Wamanda alipowasili Uwanja wa Ndege Dar es Salaam mapema leo.
Rais Barack Obama amewasili jijini Dar es Salaam mapema leo kuhitimisha ziara yake barani Afrika - na wakati akiwa hapa anatarajiwa kukaribishwa na sura anayoifahamu.

BRAZIL YAFUNGA BAO LAKE LA KWANZA DHIDI YA HISPANIA BAADA YA MIAKA 27...

Mchezaji wa Brazil, Fred (9) akishangilia na wenzake bao lake la kwanza alilofunga dhidi ya Hispania kwenye mechi ya michuano ya Kombe la Mabara iliyofanyika Uwanja wa Maracanam Brazil. Juu kulia ni Neymar ambaye alifunga bao la pili.
Bao la dakika ya 2 ya mchezo lililowekwa kimiani na mchezaji anayevalia jezi namba 9, Fred limekuwa bao la kwanza dhidi ya Hispania baada ya miaka 27.

KASHFA MPYA! MICHAEL JACKSON ALITUMIA BILIONI 56 KUNYAMAZISHA WATOTO ALIOWADHALILISHA...

Mfalme wa Pop, Marehemu Michael Jackson.
Michael Jackson 'Wacko Jacko' alilipa Dola za Marekani milioni 35 (Sawa na Shilingi za Tanzania zaidi ya bilioni 56) kama pesa za kunyamazisha wavulana wadogo zaidi ya 20 ambao aliwadhalilisha kijinsia kwa kipindi cha zaidi ya miaka 15, imedaiwa.

CHEKA TARATIBU...

Vibaka wawili waliiba viroba vya maembe na kwa bahati mbaya wakaingia navyo kwenye chumba cha maiti. Wakati wanaingia ndani wakadondosha embe mbili mlangoni.

BARABARA YA NYERERE YAFUNGWA KUPISHA UJIO WA OBAMA LEO...

Barabara ya Nyerere kama inavyoonekana pichani (kushoto).
Rais Barack Obama leo anaanza ziara ya siku mbili nchini akitokea Afrika Kusini ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuzuru Bara la Afrika.

ABIRIA 164 WA NDEGE WAKWAMA MASAA 30 KWENYE JOTO KALI LINALOUNGUZA...

Abiria wakiwamo wanawake wajawazito, watoto na wastaafu waliachwa wakiwa hawajui la kufanya kwa masaa 30 katika joto linalounguza baada ya ndege moja ya easyJet kutoka Misri kwenda Uingereza kuchelewa.

JICHO LA TATU...


RAIS OBAMA AITANGAZIA TANZANIA NEEMA YA MRADI MKUBWA WA UMEME...

Rais Barack Obama.
Ili kukabiliana na matatizo ya ukosefu wa umeme katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Marekani imeamua kuanzisha miradi kwa ajili hiyo.

Sunday, June 30, 2013

MZEE MANDELA AANDIKA WOSIA NA KUTAJA MAHALI ANAPOTAKA KUZIKWA...

KUSHOTO: Mzee Nelson Mandela. KULIA: Eneo walilozikwa mababu wa Mandela ambalo naye anataka akazikwe atakapofariki.
Mzee Nelson Mandela ameandika wosia kwenye karatasi moja ya ukubwa wa A4 ambamo ameagiza azikwe katika milima iliyojitenga nyumbani kwa mababu zake huko Qunu, imebainika.

WAPENZI WADONDOKA NA KUFA WAKATI WAKIFANYA MAPENZI DIRISHANI...

Wapelelezi wakifunika miili ya wapenzi hao eneo la tukio.
Wapenzi wameanguka na kufa baada ya dirisha walipokuwa wakifanyia mapenzi kufunguka ghafla nchini China.

WINNIE MANDELA AZUNGUMZIA HALI YA MUMEWE WA ZAMANI...

Winnie Mandela akizungumza na vyombo vya habari.
Nelson Mandela anaonesha 'maendeleo makubwa' katika afya yake tangu siku chache zilizopita, mkewe wa zamani alisema jana.

MWANAMKE ALIYEMKATA UUME MUMEWE AFUNGWA MAISHA GEREZANI...

Catherine Kieu.
Mwanamke mmoja wa California ambaye alituhumiwa kukata uume wa mumewe kabla ya kuutupa kwenye mashine ya kusagia taka amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

CHEKA TARATIBU...

Jamaa kaenda baa na mke wake wa ndoa. Wakati wakiendelea kupata vinywaji pale, ghafla akatokea changudoa mmoja na kwenda moja kwa moja kwa mke wa jamaa na kumnong'oneza sikioni: "Akulipe kabisa kabla hujaenda kulala naye, jamaa mgumu sana kulipa!!" Duh, kasheshe...

UVUMILIVU WAMSHINDA OBAMA, SASA AWAJIBU WAKENYA...

Rais Barack Obama.
Wakati Rais wa Marekani, Barack Obama amesema asingeweza kufanya ziara Kenya kutokana na Rais wake, Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Rutto kukabiliwa na mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC), pia amehadharisha Afrika kuhakikisha kuwa kampuni za kigeni zinaajiri wafanyakazi wazalendo ili wawekeze nchini mwao.

JICHO LA TATU...


MAITI AZIKWA MARA MBILI MWANZA...

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwili wa kijana umezikwa mara mbili,  baada ya maziko ya kwanza kufanywa na wanakijiji cha Mwalubungwe Kata ya Hungumalwa  Kwimba, Mwanza, baada ya kumuua wakidhani jambazi na kumzika bila nguo wala sanda.

Saturday, June 29, 2013

ALIYEMBAKA BIBI MSTAAFU MIAKA 16 ILIYOPITA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA...

KUSHOTO: Wendell Baker. KULIA: Hazel Backwell enzi za uhai wake.
Mtu aliyembaka mstaafu chumbani kwake miaka 16 iliyopita amehukumiwa kifungo cha maisha jela kufuatia kurejewa tena kwa hukumu chini ya sheria hatarishi.

KODI YA PETROLI YASHUSHWA, USHURU WA SIMU ZA MKONONI WAFUTWA...

Mfumo mpya wa Bunge kuanza na bajeti za kisekta na kumalizia na Bajeti ya Serikali pamoja na uundwaji wa Kamati ya Bajeti, umeonesha makali yake kiasi na kuilazimisha Serikali, kushusha kodi ya petroli na kufuta ushuru wa kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu.

OBAMA AWASILI AFRIKA KUSINI, KUTOKWENDA KUMTEMBELEA MZEE MANDELA...

Rais Barack Obama akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili nchini Afrika Kusini jana jioni.
Rais Barack Obama amewasili Afrika Kusini jana jioni, lakini sasa hatamtembelea kinara wa kupinga ubaguzi wa rangi, Mzee Nelson Mandela hospitalini alikolazwa mjini Pretoria katika kituo chake cha pili cha ziara yake ya nchi tatu za Afrika.

JICHO LA TATU...


PINDA AHITIMISHA BUNGE LA BAJETI KWA KUTOA ONYO KALI...

Mizengo Pinda.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, jana alihitimisha mjadala wa Bunge la 10 lililojadili na kupitisha Bajeti ya Serikali na bajeti za wizara mbalimbali, huku akisisitiza umuhimu wa kila mbunge kuwajibika kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani na utulivu.

MWANAUME ADAI KUISHI MIAKA MITANO BILA KULA CHAKULA...

Kirby de Lanerolle.
Mwanaume mmoja nchini Sri Lanka anadai ameweza kuishi bila kula chakula kwa miaka mitano iliyopita.
Ingawa wataalamu wanaamini wanadamu wanaweza tu kuishi kwa miezi miwili bila kula, Kirby de Lanerolle anasisitiza alikuwa akihitaji tu hewa safi kama kirutubisho.

Friday, June 28, 2013

WAGANGA WA JADI AFRIKA KUSINI WAMFANYIA TAMBIKO MZEE MANDELA...

Waganga wa Jadi nchini Afrika Kusini.
Sasa ni dhahiri kuwa maisha ya kiongozi wa zamani wa nchi hii, Nelson Mandela yamo hatarini kutokana na kwamba anaishi kwa msaada wa mashine, imethibitishwa na mmoja wa wazee wa ukoo wa kiongozi huyo.

JICHO LA TATU EXTRA...


SABABU ZA OBAMA KUTOKWENDA KENYA, NIGERIA ZAANIKWA...

Rais Barack Obama.
Rais Barack Obama amepongeza hatua zilizopigwa na Afrika katika kujenga demokrasia, imeelezwa kutoka Dakar, Senegal.

CHEKA TARATIBU...

Mke kamwomba mumewe pesa ya kununulia nyama kwakuwa aliitamani sana. Mume akamshika mkono mkewe na kwenda naye hadi kwenye kioo kisha akatoa Shilingi elfu tano na kusema:

UNENE ULIOKITHIRI WAMWOKOA BIBI ASIPANDISHWE KIZIMBANI...

Rita Astbury akionesha picha aliyopiga na wajukuu zake.
Mwanamke aliyenenepeana amekwepa kupandishwa kizimbani sababu maofisa waliamua kuwa kumtoa kwenye nyumba yake ingekuwa hatari.

MARAIS WA MAREKANI WAIBEBA TANZANIA...

Balozi Ombeni Sefue.
Tanzania imetajwa kuwa nchi pekee Afrika iliyobahatika kutembelewa na marais watatu wa Marekani wakiwa madarakani.