Bao la dakika ya 2 ya mchezo lililowekwa kimiani na mchezaji anayevalia jezi namba 9, Fred limekuwa bao la kwanza dhidi ya Hispania baada ya miaka 27.
Fred alifunga bao hilo katika mchezo wa Kombe la Mabara uliowakutanisha miamba hao kwenye Uwanja wa Maracana, Brazil usiku wa kuamkia leo.
Hadi tunarusha habari hii wakati wa mapumziko, Brazil ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-0 kufuatia lile la Neymar alilofunga dakika ya 44.
Mara ya mwisho kwa Brazil kufunga bao dhidi ya miamba hao wa Ulaya ilikuwa mwaka 1986 pale mshambuliaji Socrates alipofunga bao katika michuano ya Kombe la Dunia.
Katika mechi nyingine, Italia imefanikiwa kupunguza machungu kwa kushika nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo baada ya kuifunga Uruguay kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya mabao 2-2 katika dakika 120 za mchezo huo.

No comments:
Post a Comment