Monday, July 1, 2013

ABIRIA 164 WA NDEGE WAKWAMA MASAA 30 KWENYE JOTO KALI LINALOUNGUZA...

Abiria wakiwamo wanawake wajawazito, watoto na wastaafu waliachwa wakiwa hawajui la kufanya kwa masaa 30 katika joto linalounguza baada ya ndege moja ya easyJet kutoka Misri kwenda Uingereza kuchelewa.

Wasafiri wenye hasira wanaofikia 164, wengi wao wakiwa Waingereza, walielezwa kubaki ndani ya ndege kwa masaa matano licha ya ndege hiyo kupangwa kuruka Saa 11 jioni siku ya Alhamisi.
Abiria hao hatimaye waliruhusiwa kushuka na kupelekwa kwenye hoteli moja lakini ndege hiyo iliendelea kusukumwa kwenda nyuma.
Hatimaye walitua Uwanja wa Ndege wa Gatwick juzi Saa 10 alfajiri.
Abiria Luke Gayle, mwenye miaka 20, kutoka Croydon, kusini mwa London, alieleza: "Ilikuwa fedheha. Watu walikuwa wakilia na kupoteza uvumilivu wao wakati tulipokuwa tumenaswa kwenye joto kali.
"Mwanamke mwenye ujauzito wa miezi sita alijilaza kwenye viti vitatu. Lilikuwa ni joto la kuchoma na hakukuwa na chakula."
Kwa mujibu wa Luke, hakuna walioruhusiwa kupiga simu za bure kuwasiliana na familia zao.
Msemaji wa easyJet alisema: "Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote na kwa uchelewaji wowote kwa abiria wakiwa wameelezwa wanaweza kupiga simu hadi mbili za bure."

No comments: