Saturday, June 29, 2013

ALIYEMBAKA BIBI MSTAAFU MIAKA 16 ILIYOPITA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA...

KUSHOTO: Wendell Baker. KULIA: Hazel Backwell enzi za uhai wake.
Mtu aliyembaka mstaafu chumbani kwake miaka 16 iliyopita amehukumiwa kifungo cha maisha jela kufuatia kurejewa tena kwa hukumu chini ya sheria hatarishi.

Wendell Baker, mwenye miaka 56, hapo awali aliachiwa huru mahakamani pale alipopandishwa kizimbani mwaka 1999 kwa kumshambulia mstaafu mwenye miaka 66, Hazel Backwell sababu jaji alitupilia mbali ushahidi wa DNA.
Lakini alirejeshwa tena kwenye kesi mwaka huu baada ya vipimo vya DNA vinavyofanana kugundulika kwenye 'mpangilio mmoja kati ya bilioni'.
Baker, ambaye alipatikana na hatia na wazee wa mahakama baada ya kujadiliana kwa zaidi ya saa moja Jumanne, aligoma kutoka kwenye selo yake kwenda kusikiliza hukumu yake katika mahakama ya Old Bailey.
Jaji Peter Rook alisema atatumikia kifungo cha miaka 10 na miezi sita kabla ya kufikiriwa kupewa kifungo cha nje.
Bibi Hazel, ambaye alifariki dunia mwaka 2002, alisumbuliwa na 'mateso ya kutisha' pale Baker alipovamia nyumbani kwake huko Stratford, mashariki mwa London, wakati akiwa amelala mnamo Januari 1997.
Baker alimfunga mikono yake nyuma, akampiga na kumbaka, kisha kupekua nyumba yake kabla ya kumtelekeza na kumfungia ndani ya kabati.
Bibi huyo alikutwa kwa bahati tu na jirani yake George Walpole jioni ya siku iliyofuata, 'akaogopa' na kufikiri bibi huyo alikuwa akikaribia kufa.
Shambulio hilo lilimwacha bibi huyo akiwa mwenye hofu kubwa kuendelea kuishi peke yake au kutoka nje mwenyewe na 'akafariki akiwa mnyonge na aliyekata tamaa', familia yake ilisema.
Baker alikamatwa mnamo Oktoba 1998 kwa tuhuma za ubakaji na kuchukuliwa vipimo vya DNA ambavyo vilifanana na vile vilivyochukuliwa kwa bibi Hazel.
Hapo kabla alikwishachukuliwa vipimo vya DNA Januari 1998 ambavyo pia vilifanana na vile vilivyochukuliwa kwa bibi Hazel.
Lakini Baker aliachiwa huru mahakamani baada ya jaji huyo kuamua kusitisha kesi hiyo kufuatia malumbano ya kisheria wakati wa kuanza kwa kesi ya msingi mwaka 1999.
Mabadiliko katika sheria mwaka 2005 yaliruhusu mtu aliyefutiwa mashitaka ya makosa mazito kupandishwa tena mahakamani kwa mazingira fulani, lakini pale kesi hiyo ilipopitiwa upya mwaka 2007, ilionekana kwamba sehemu kubwa ya ushahidi ilipotea ama kuharibiwa.
"Mama yangu kwa huzuni alifariki dunia akiwa mpweke, akiwa amekata tamaa na jinamizi la tukio hilo, na hakuweza kushuhudia mtu aliyemsababishia maumivu makubwa akihukumiwa kifungo kwa kile alichofanya."
Kesi hiyo kisha ikafunguliwa upya mwaka 2009 na Baker, anayetokea Walthamstow, kaskazini mashariki mwa London, lakini asiye na makazi ya kudumu, alikamatwa mwaka 2011.
Baker ambaye ni mzaliwa wa Jamaica alikana kumbaka bibi Hazel, akiieleza mahakama hiyo alibambikiwa kesi hiyo na polisi, ambao alidai walikuwa wakimuwinda kwa miaka mingi.
Mahakama ilielezwa kwamba Baker alikuwa akifunga na kuachiwa gerezani tangu miaka ya 1970 kwa makosa mbalimbali yakiwamo ya uporaji, wizi na kudhuru mwili.
Jana mtoto wa bibi huyo, David Backwell alikuwa mahakamani kushuhudia mshambulizi wa mama yake akihukumiwa.

No comments: