Monday, July 1, 2013

CHEKA TARATIBU...

Vibaka wawili waliiba viroba vya maembe na kwa bahati mbaya wakaingia navyo kwenye chumba cha maiti. Wakati wanaingia ndani wakadondosha embe mbili mlangoni.
Wakiwa ndani wakaanza kugawana: "Hii yangu! Hii yangu!" Mlinzi bila kujua kama kuna watu wameingia wakati akiwa msalani, akatimua mbio na kwenda kumwita dokta. "Dokta, kuna malaika wanagawana roho kwenye chumba cha maiti!" Dokta na yule mlinzi wakaenda kushuhudia kilichokuwa kikiendelea mle ndani. Walipofika mlangoni wakasikia sauti kutoka ndani zikisema: "Kuna nyingine mbili pale nje!" Kusikia vile, dokta na mlinzi wakatimua mbio huku wakipiga kelele za kuomba msaada. Kasheshe...

No comments: