Saturday, October 5, 2013

ZITTO AWASILISHA MUSWADA BINAFSI KUFUTA SHERIA YA MAGAZETI...

Kabwe Zitto.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto amewasilisha kwa Katibu wa Bunge muswada binafsi kufuta Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976.

HOTUBA KAMILI YA RAIS KIKWETE KWA WANANCHI - OKTOBA 4, 2013...

Ndugu Wananchi;
Namshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kumaliza mwezi Septemba salama na kuwasiliana kwa kutumia utaratibu wetu huu mzuri.  Naomba radhi kuzungumza nanyi siku ya leo kwa sababu nilikuwa safari na nilirejea jioni ya tarehe 30 Septemba, 2013.   Awali nilifikiria nisiseme, nisubiri mwisho wa mwezi wa Oktoba.  Lakini, baada ya kupata taarifa ya yaliyojiri, nimeshauriwa na nimekubali angalau niyasemee baadhi ya mambo huenda itasaidia.  Niwieni radhi nisipoyasemea baadhi ya mambo siyo kwa kuyapuuza, bali kwa kuepuka hotuba kuwa ndefu mno.  Nitayatafutia mahali pengine pa kuyasemea.

MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA DADA WA FREEMAN MBOWE...

Marehemu Grace Mbowe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu wa Bunge, William Lukuvi, ameongoza mamia ya waombolezaji katika maziko ya Grace Mbowe (57), ambaye ni dada wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

JICHO LA TATU...


CCM YAMKANA MWENYEKITI WAKE JUMUIYA YA WAZAZI...

Abdallah Bulembo (kushoto) na Nape Nnauye.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeikana kauli ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo na kusema kauli ya  mwenyekiti huyo ni yake mwenyewe wala si msimamo wa chama.

Friday, October 4, 2013

SALUNI YA BM KINONDONI YASHEREHEKEA MIAKA 11 TANGU KUANZISHWA KWAKE...

Mandhari ya Saluni ya BM kwa nje.
Saluni ya BM Hair and Beauty Clinic leo imeadhimisha miaka 11 tangu ilipoanzishwa rasmi mwaka 2002 Kinondoni Manyanya, Dar es Salaam.

TUKIFANYIA KAZI MANENO YA MCHUNGAJI MSIGWA NCHI ITASONGA MBELE...


 
Baada ya kumsikia Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chadema, Mchungaji Peter Msigwa, tutumie maoni yako kama ifuatavyo. Bofya hapa chini katika neno COMMENTS.

AL-SHABAAB WAITISHA KENYA, WASEMA NAIROBI ITATIRIRISHA MITO YA DAMU...

Wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab.
Kikundi cha Al Shabaab kimetishia kumwaga damu zaidi Kenya kwa kufanya mashambulizi mapya na safari hii wanatamba kupiga patakapouma zaidi.

MWANAMKE AJIFICHA USO MIAKA 19 BAADA YA KUOTA NDEVU KIAJABU...

Agustina Dorman katika picha tofauti, na kulia akiwa na mwanae wa miaka mitatu.
Mwanamke mmoja ambaye alianza kuchipuka nywele nyeusi usoni kwa miaka 19 baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza anasema hataki tena kuficha ndevu zake.

JICHO LA TATU...


VIBAKA WARUKA UKUTA NA KUIBA NYUMBANI KWA MKUU WA WILAYA...

Senyi Ngaga.
Wezi wameruka ukuta wa makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Senyi Ngaga, kuvunja banda la kufugia na kuchukua mifugo yote iliyokuwemo.

WANASIASA WAIPA WAKATI MGUMU TUME YA MABADILIKO YA KATIBA...

Jaji Joseph Warioba.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewaambia wanasiasa wajadili  rasimu iliyotolewa badala ya kujadili Tume au wajumbe wake.

Thursday, October 3, 2013

WATANZANIA HAWAAMINIKI KIMATAIFA, WADAIWA KUPENDA 'MICHONGO'...

Balozi Ombeni Sefue.
Kuporomoka kwa maadili ya Mtanzania, kumetajwa kuporomosha hadhi ya Mtanzania ndani na nje ya nchi, na sasa wawekezaji wanaogopa kuwaajiri.

JICHO LA TATU...


CHAMA CHA WALIMU TANZANIA CHAGAWANYIKA MAKUNDI MANNE...

Ezekiah Oluoch.
Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kinakabiliwa na mgogoro wa ndani kwa ndani, ambapo sasa kuna makundi manne ya walimu, yaliyojitambulisha kutaka kujitoa ndani ya chama hicho na kuunda chama kingine.

Wednesday, October 2, 2013

MBUNGE GODBLESS LEMA AFUTIWA KESI YA UCHOCHEZI...

Godbless Lema.
Mbunge wa Arusha, Godbless Lema  imefutiwa   kesi   ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili baada ya upande wa mashtaka kusema hauna nia ya kuendelea na kesi mahakamani hapo.

OPERESHENI KIMBUNGA YANASA SILAHA ZA KIVITA, MABOMU YA KUTUPA KWA MKONO...

Baadhi ya silaha.
Operesheni Kimbunga inayoendelea kwa awamu ya pili, imebaini hifadhi haramu ya silaha za kivita, katika kijiji bandia cha wahamiaji haramu cha Nyamgali kutoka Burundi, kilichokuwa wilayani Kasulu.

MWANANCHI YAONYWA KUCHAPISHA GAZETI MTANDAONI...

Mtandao wa gazeti la Mwananchi.
Serikali imeitaka Kampuni ya New Habari 2006, kuacha kuchapisha gazeti la Rai kila siku na kampuni ya Mwananchi kuacha kuchapisha gazeti la Mwananchi kwenye mtandao.

MAGAIDI WALIWATOROKA ASKARI WESTGATE MALL KUPITIA KWENYE MTARO...

Askari wa Kenya wakijipanga kupambana na magaidi hao katika jengo la Westgate Shopping Mall.
Inahofiwa kuwa baadhi ya magaidi wa kundi la al Shabaab, ambao walivamia maduka katika jengo la Westgate walitoroka kwa kutumia mtaro mkubwa wa maji machafu ulioko chini ya ardhi.

JICHO LA TATU...


UPELELEZI KESI YA UCHOCHEZI DHIDI YA SHEKHE PONDA WAKAMILIKA...

Shekhe Ponda Issa Ponda.
Upande wa mashitaka katika kesi ya uchochezi inayomkabili Katibu wa Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Shekhe Ponda Issa Ponda, umedai kuwa upelelezi umekamilika.

Tuesday, October 1, 2013

WAKATOLIKI WAANZA MWEZI WA ROZALI TAKATIFU LEO....

Waumini wa Kikristo wa Kanisa Katoliki duniani kote leo wanaanza rasmi mwezi wa Rozali Takatifu kuanzi Oktoba 1 hadi Oktoba 31, mwaka huu.

KILA MTEJA KULIPA DENI LA KODI YA SIMU YA MKONONI SHILINGI 3,000...

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekiri kuziandikia waraka kampuni za simu nchini kuzitaka zianze kukata kodi mpya ya laini mara moja kuanzia mwezi huu.

MFADHILI WA AL-SHABAAB KENYA ASEMA BAADA YA WESTGATE, SASA NI UINGEREZA...

Abubaker Shariff Ahmed 'Makaburi' wakati wa mahojiano juzi.
Mhubiri kisirani anayetafutwa kwa kuajiri wauaji kwenye kundi ambalo liliua mamia ya wananchi katika jengo la Westgate Shopping Mall mjini Nairobi ametahadharisha jana kwamba Uingereza ilikuwa kusudio linalofuata.

BOSI MPYA APANGUA MAOFISA WA IDARA YA UHAMIAJI...

Sylvester Ambokile.
Idara ya Uhamiaji imefanya mabadiliko makubwa katika safu za maofisa wake wa mikoa, wilaya na wafawidhi wa vituo nchini.

MKENYA 'ALIYEMTEKA' DK ULIMBOKA ATOZWA FAINI SHILINGI 1,000...

Dk Steven Ulimboka akiwa hospitalini mara baada ya kushambuliwa.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya Sh 1,000, raia wa Kenya, Joshua Muhindi baada ya kupatikana na hatia ya kutoa taarifa za uongo kwa Ofisa wa Polisi.

KESI YA SHEKHE PONDA KUENDELEA KUSIKILIZWA LEO...

Shekhe Ponda Issa Ponda.
Kesi inayomkabili Katibu wa Taasisi na Jumuiya ya Kiislamu Tanzania,  Shekhe Ponda Issa Ponda, inatarajia kuendelea kusikilizwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro.

JICHO LA TATU...


MVUA YAZUA KIZAAZAA JIJINI DAR ES SALAAM, NI MSONGAMANO MTINDO MMOJA...

Msongamano katikati ya jiji la Dar es Salaam kama unavyoonekana pichani.
Mvua iliyonyesha jijini  Dar es Salaam jana kwa nyakati tofauti, kwa kiasi kikubwa imesababisha foleni ya magari katika maeneo mengi na  kuleta usumbufu kwa  watumiaji wa barabara hususani wenye magari.

PAPA YOHANE PAULO II SASA KUTANGAZWA MTAKATIFU APRILI 27...

Papa Yohane Paulo II.
Papa Yohane Paulo II na Yohane XXIII watatangazwa kuwa watakatifu mnamo Aprili 27, mwaka ujao, Papa Francis ameamua wakati wa mkutano na makardinali.