Tuesday, October 1, 2013

PAPA YOHANE PAULO II SASA KUTANGAZWA MTAKATIFU APRILI 27...

Papa Yohane Paulo II.
Papa Yohane Paulo II na Yohane XXIII watatangazwa kuwa watakatifu mnamo Aprili 27, mwaka ujao, Papa Francis ameamua wakati wa mkutano na makardinali.

Francis alitangaza Julai angewatakatifuza wawili kati ya mapapa wenye tija zaidi katika karne ya 20 kwa pamoja, akithibitisha muujiza uliofanywa na Yohane Paulo na kupinda kanuni za Vatican kwa kuamua kwamba Yohane XXIII hakuhitaji kufanya muujiza wowote.
Wachunguzi wamesema uamuzi huo kuwatakatifuza pamoja ulikuwa umelenga kuunganisha kanisa hilo, kutokana na kila papa kuwa na vitu vyake anavyoafiki na anavyopinga. Ni wazi Francis anashabikia vyote.
Katika kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha Yohane Paulo, Francis alisali kwenye sanamu za mapapa wote wawili - ishara kwamba anaona mwendelezo mkubwa binafsi na kiroho ndani yao.
Mapapa wote wametambuliwa kwa ukaribu na Halmashauri ya Pili ya Vatican, mikutano ya 1962-65 ambayo ililileta Kanisa Katoliki katika nyakati mpya, ishara kwamba Francis dhahiri anataka kutoa taarifa kuhusu wajibu wa halmashauri hiyo katika kuliunda kanisa hilo leo.
Kawaida, utakatifuzaji ulitarajiwa kufanyika Desemba 8 lakini mapapa wa Poland walilalamika kwamba ingekuwa vigumu kwa mahujaji wa Poland kwenda Vatican kwa basi kwenye barabara zenye ukungu na barafu.
Matokeo yake, Jumapili ya kwanza baada ya Pasaka ikachaguliwa badala yake - siku ya mafungo iliyoanzishwa na Yohane Paulo.
Yohane Paulo ndiye alimfanya Jorge Mario Bergoglio - Papa Francis wa sasa - kuwa kardinali.

No comments: