Wednesday, July 31, 2013
Tuesday, July 30, 2013
WALIOMMWAGIA TINDIKALI MAMA NA WANAWE HUKU WAKICHEKA WAFUNGWA MIAKA 44 JELA...
![]() |
JUU: Yannick Ntesa. KATIKATI: Abdul Motin. CHINI: Ahad Miah. KULIA: Shule ya Msingi ya Upton Cross. |
Kundi moja ambalo lilikuwa likicheka huku wakimlowesha mwanamke mmoja kwa tindikali wakati mama huyo akiwasindikiza nyumbani watoto wake mapacha wenye miaka sita kutoka shuleni, wamehukumiwa kifungo cha jumla ya miaka 44 jela.
MKENYA AHUKUMIWA KIFO KWA KUSAIDIA MAHARAMIA WA SOMALIA KUTEKA, KUUA WATALII...
![]() |
KUSHOTO: Bi Judoth Tebbutt akiwa amedhoofu baada ya kuachiliwa huru. KULIA: Ali Babitu Kololo akivishwa pingu. |
Mfanyakazi wa hoteli moja jana alihukumiwa kifo nchini Kenya baada ya kutiwa hatiani kwa kusaidia kutekwa mtalii wa Uingereza, Bi Judoth Tebbutt wakati wa shambulio ambalo mume wa mtalii huyo alipigwa risasi na kufa.
Monday, July 29, 2013
Sunday, July 28, 2013
Saturday, July 27, 2013
Friday, July 26, 2013
JWTZ IKO TAYARI KWA VITA, NCHI ITAKAYOTHUBUTU ITAKIONA CHAMOTO...
![]() |
Rais Jakaya Kikwete akiweka silaha kama ishara ya kuwambuka mashujaa, jana. |
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete amewatoa hofu Watanzania akiwataka walale usingizi kwa kuwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wowote lipo tayari kulinda nchi kwa gharama yoyote.
Thursday, July 25, 2013
MWANAMKE ALIYESITISHA NDOA ADAI KATEKISTA ALIMSUKUMA KWENYE NGAZI ZA KANISA...
![]() |
Mwanamke huyo akiwa amevalia vazi lililozusha tafrani yote hiyo. Nyuma yake ni Kanisa la Mt. Peter, Dar es Salaam. |
Wakati mwanamke wa kivazi kilichositisha ndoa kanisani kwa dakika kadhaa akidai hakuwa na tatizo kuvaa vile, Katekista wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Peter, Yohane Maboko, amesisitiza kuwa alikiuka maadili ya Kanisa.
Wednesday, July 24, 2013
ASKARI KUTOKA ZANZIBAR WALIOUAWA DARFUR WAZIKWA...
![]() |
Askari wakiwa wamebeba moja ya majeneza yenye miili ya wanajeshi hao. |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein jana aliungana na viongozi mbalimbali wakiwemo wa vikosi vya ulinzi na usalama wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na wafiwa na wananchi katika maziko ya wanajeshi wa Zanzibar waliouawa Darfur, Sudan.
Tuesday, July 23, 2013
ASKARI SABA WA JWTZ WALIOUAWA DARFUR WALIPAMBANA KWA MASAA MAWILI...
![]() |
Baadhi ya askari wa JWTZ wakipita mbele ya miili ya wenzao waliouawa mjini Darfur, kutoa heshima zao za mwisho kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi, Dar es Salaam jana. |
![]() |
Majeneza yenye miili ya askari hao yakiwa yamepangwa tayari kwa zoezi la kutoa heshima za mwisho. |
Wanajeshi saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), waliouawa wakati wakilinda amani Darfur nchini Sudan, walipigana kwa saa mbili wakati wakijitetea kabla ya kufikwa na mauti.
WASEMA MISHAHARA MIPYA YA WATUMISHI WA NDANI HAITEKELEZEKI...
![]() |
Baadhi ya watumishi wa ndani wakiwa katika moja ya semina waliyoandaliwa. |
Baada ya Serikali kuweka kisheria mshahara wa kima cha chini kwa watumishi wa ndani, Chama cha Wafanyakazi wa Hifadhi, Hoteli, Majumbani, Huduma za Jamii na Ushauri (CHODAWU), kimeeleza kuwa utekelezaji wa sheria hiyo ni mgumu.
Subscribe to:
Posts (Atom)