![]() |
| Rais Jakaya Kikwete akiweka silaha kama ishara ya kuwambuka mashujaa, jana. |
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete amewatoa hofu Watanzania akiwataka walale usingizi kwa kuwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wowote lipo tayari kulinda nchi kwa gharama yoyote.
Aidha, amesema Serikali haitakubali hata mara moja, mtu aichezee amani ya Tanzania na Dola iko tayari kuilinda na kuitetea nchi na akaonya tena, kwamba hakuna atakayejaribu kuvuruga nchi, apone.
Kikwete alisema hayo jana katika kambi ya Kaboya, wilayani Muleba, Kagera wakati akihutubia wananchi kwenye maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Mashujaa na kutangazwa moja kwa moja na televisheni ya Taifa (TBC).
Maadhimisho hayo ni kumbukumbu ya wanajeshi waliokufa katika Vita ya Kagera mwishoni mwa miaka ya sabini baada ya majeshi ya Nduli Iddi Amini wa Uganda kuvamia nchi na kuchukua sehemu ya ardhi ya Tanzania.
Akisisitiza alichozungumza Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange alipomkaribisha kusalimu wananchi katika sherehe hizo kuwa Jeshi lipo imara saa 24 kulinda wananchi, Rais Kikwete alitaka Watanzania wasiwe na hofu.
“Hamhitaji kauli zaidi ya hii (ya Mwamunyange), laleni usingizi, msisikilize maneno ya mitaani, Jeshi liko salama na imara, atakayejaribu, atakiona cha mtema kuni...Jeshi wakati wowote, saa yoyote, tupo tayari kuilinda nchi yetu,” alisema Kikwete na kuongeza.
“Tutailinda, tutaitetea, hatutakubali mtu aichezee, hatuna nchi nyingine, ni hii hii, hakuna atakayepona anayetaka kuchezea nchi yetu”.
Akizungumzia kuhusu kuenzi mashujaa waliobaki waliopigana vita, Rais Kikwete alisema ingawa hakuna uwezo wa kuwaridhisha kwa namna ya mahitaji yao, Serikali kamwe haitaacha wateseke, itaendelea kuwaenzi kwa kuwa walijitoa muhanga kwa nchi yao.
“Wenzetu walijitoa muhanga kwa ajili yetu, kuhakikisha usalama wa nchi kuna gharama zake, Taifa haliwezi kuwasahau, Serikali itaendelea kuwajali, wapo mashujaa wenzetu waliokwenda Msumbiji, baadhi nao walelala, waliobaki tutaendelea kuwajali,” alisisitiza Kikwete.
Aligusia ukaidi wa Amini na majeshi yake alipovamia nchi mwaka 1978, akisema baada ya kuingia Kagera na kubadili ramani na kudai Mto Kagera ndio mpaka, aliharibu mali nyingi na Amiri Jeshi Mkuu wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere alimwamuru aondoke akakataa, ndipo akavamiwa na kushindwa vibaya.
“Ili kumwonesha kuwa uwezo tunao, Mwalimu Nyerere aliamuru pamoja na kumtoa katika ardhi yetu, aondoke kabisa madarakani na pia majeshi yetu yaliingia Uganda eneo la Masaka na Mbarara kushambulia ili wapate uchungu wa kujenga kama waliotupatia sisi,” alifafanua Rais Kikwete akidhihirisha kwa mifano, uwezo wa Jeshi la Tanzania.
Rais Kikwete awali pamoja na kumkaribisha Jenerali Mwamunyange kusalimia wananchi, pia alikaribisha viongozi wengine wa ngazi za juu waliohudhuria sherehe hizo kuwasalimia wananchi akiwamo Makamu wa Rais wa Muungano, Dk Mohamed Gharib Bilal na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na ambao wote walisisitiza kuilinda amani ya nchi.
Wengine waliohudhuria na kusalimu wananchi ni pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.
Rais Kikwete alitumia nafasi hiyo pia kutaka wabunge wa majimbo mawili ya Muleba, Charles Mwijage wa Kaskazini na Profesa Anna Tibaijuka wa Kusini, ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kueleza matatizo yanayokabili wananchi wa eneo hilo.
Mwijage (CCM) alisema miongoni mwa changamoto kubwa katika eneo hilo ni utata wa mpaka wa kambi hiyo ya Jeshi ya Kaboya kutojulikana na kusababisha uhusiano mbaya kati ya wakazi wa eneo hilo na Jeshi, kwa kuwa wanashindwa kujua walime mpaka wapi.
Mbunge huyo alisema pia kuwa ujenzi wa madaraja mawili likiwamo la Kishala na mradi wa kuvua samaki ambao Serikali iliwezesha mtu kwenda kujifunza Vietnam na China, ni mambo yanayowatatiza wananchi wa jimbo hilo.
Akijibu changamoto hizo, Kikwete alitaka watendaji wa wilaya na mamlaka husika kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa na kuwambia wakikwama wamweleze, kwa kuwa yeye ndiye mtoa fedha za miradi ya wananchi.
Kuhusu umeme vijijini, Kikwete alisema umeme utafika ulikoahidiwa, alimwita Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fabian Massawe kuwaeleza wananchi ulikofikia na Massawe alisema tayari umeanza katika vijiji kadhaa na Muleba utafika kama ulivyoahidiwa kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

No comments:
Post a Comment