Mama wakati akiandaa chakula mezani kamwagiza mwanae ampigie simu kumwita baba yake aliyekwenda matembezini. Baada ya kusubiri kwmuda bila majibu, mama akamuuliza mwanae: "Vipi, umempata baba yako? Kasemaje?" Mtoto akajibu: "Aah sijampata bado! Isitoshe simu yake anajibu mwanamke!" Mama kwa hasira akamwambia mwanae aache. Baada ya dakika chache mume akarejea nyumbani, ile anaingia tu wacha apate kipigo kutoka kwa mkewe. Mwishowe mume huku akichuruzika damu akahoji kulikoni. Mke akajibu: "Simu yako ulimwachia nani? Hebu mwanangu sema alivyokujibu yule mwanamke!" Mtoto akasema: "Alinijibu NAMBA UNAYOPIGA KWA SASA HAIPATIKANI!" Duh...

No comments:
Post a Comment