![]() |
| Mandhari ya Zanzibar. |
Baadhi ya wajumbe wa mabaraza ya Katiba, wamepinga muundo wa Muungano wa serikali tatu kwa hoja kadhaa, ukiwamo uwezekano wa muundo huo kuzorotesha Muungano na umoja wa kitaifa.
Wengine wamedai kuwa muundo huo, utavunja heshima ya waasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, hayati Shekhe Abeid Amani Karume na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Akizungumza katika mkutano wa Baraza ya Katiba Mkoa wa Kaskazini Unguja jana, Mjumbe wa Baraza hilo kutoka kata ya Mahonda, Mohamed Mwindadi Haji, alielezea wasiwasi wake wa kuwepo urasimu mkubwa wa uendeshaji wa mambo ya Muungano, katika muundo wa serikali tatu.
Alisema hivi sasa upo muundo wa serikali mbili, lakini bado kuna matatizo yanayotokana na Muungano na kuhoji itakuwaje kama mchakato wa serikali tatu ukianza.
“Mimi napinga muundo wa serikali tatu ambao naona utasababisha urasimu mkubwa zaidi na kuzorotesha Muungano wenyewe...bora tubaki katika serikali mbili,” alisema.
Mjumbe wa kata ya Donge, Salum Suleiman Ameir, alisema muungano wa serikali mbili, ndio uliopata baraka na ridhaa kutoka kwa waasisi wa Muungano baada ya kuufanyia utafiti na kujua faida zake.
“Kama tunataka radhi za viongozi wetu waasisi wa Muungano huu, basi turudi katika makubaliano yetu ya asili ya Muungano wa serikali mbili ambao ndio ulijenga Taifa la Tanzania kuwa moja,” alisema.
Mjumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Kati, Unguja, Sada Abdi, alitaka mfumo wa serikali mbili uendelee, huku akisisitiza kero za Muungano zipatiwe ufumbuzi haraka.
Alisema mfumo wa serikali mbili umepata mafanikio makubwa pamoja na kujenga uhusiano mzuri wa wananchi wa pande mbili za Muungano, na kuwa na Taifa lenye nguvu na upendo na mshikamano kwa watu wake, hivyo ni bora kuendelea na mfumo huo.
“Mimi napendekeza kuendelea kwa mfumo wa serikali mbili uliopo sasa, ambao unahitaji kufanyiwa marekebisho tu zaidi katika kuzipatia ufumbuzi kero za Muungano,” alisema.
Alipinga kuondoshwa kwa viti maalumu vya wanawake katika Rasimu ya Katiba, kwa madai kwamba kutapunguza idadi ya wabunge wanawake na kutoa mwanya kwa mfumo dume kuendelea kuota mizizi na kutawala.
Mjumbe wa wilaya ya Kaskazini B, Zingwezingwe Kombo Baraka, alipinga mfumo wa serikali tatu akisema ni gharama kwa walipa kodi.
“Mfumo wa Serikali tatu utabebesha majukumu mengi wananchi wa Tanzania, kutokana na Taifa kuwa na uchumi tegemezi zaidi,” alisema.
Mjumbe wa wilaya ya Kati Unguja, Arada Ali Abdallah, alitaka Katiba iweke ukomo wa muda wa umri wa urais, akipendekeza anayefikia miaka 70, asiruhusiwe kugombea nafasi hiyo ya juu ya uongozi.
“Katiba mpya iweke ukomo wa kugombea urais, mtu anapofika miaka 70, asiruhusiwe kugombea,” alisema Arada.
Mjumbe wa wilaya ya Kati Unguja, Zainab Khamis Shomari alitaka Katiba itambue rasmi usawa wa binadamu bila kubagua kati ya mwanamke na mwanamume.
Shomari alisema wanawake sasa wanatakiwa kutambuliwa rasmi na kuondokana na ubaguzi katika majukumu na ajira.
“Tunataka wanawake watambuliwe rasmi katika Katiba mpya...tumeshuhudia vitendo vya ubaguzi kwa wanawake na kushindwa kupiga hatua ya maendeleo zikiwamo nafasi za kugombea uongozi,” alisema.
Alitaka Katiba mpya ibainishe na kupiga marufuku ajira za watoto ambazo zimekuwa zikidumaza maendeleo ya jamii, kwa kukosa fursa mbalimbali ikiwamo elimu.
Katika mikutano ya mabaraza ya Katiba iliyofanyika mikoa ya Kusini na Kaskazini Unguja, wanawake walijitokeza kwa wingi na kuchangia rasimu hiyo.
Mmoja wao, Fatma Haji Juma alisema walihamasika vya kutosha kuchangia rasimu na kutoa mapendekezo yao ili kuboresha Katiba iwe na maslahi ya wananchi.
Mikutano ya Baraza la Katiba mkoa wa Kusini na Kaskazini Unguja, ilisimamiwa na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Awadh Ali Said na Mwantumu Malale na Katibu, Asaa Rashid.

No comments:
Post a Comment