![]() |
| Feroz-un-Din Mir (kushoto) na Jiroemon Kimura. |
Mwanaume mmoja nchini India anadai ana umri wa miaka 141 - ambao utamfanya awe binadamu mzee zaidi duniani ambaye bado yuko hai.
Feroz-un-Din Mir, kutoka Kashmir, anasema anavyo vyeti vya serikali vinavyothibitisha kwamba alizaliwa Machi 10, 1872.
Wafanyakazi kutoka Guinness World Records wadhaniwa kuwa wanafanyia uchunguzi madai hao, ambayo yatamfanya awe mkubwa kwa miaka 26 zaidi ya Misao Okawa, mtu anayeshikilia rekodi hiyo kwa sasa akiwa na miaka 115.
Pia anaweza kumpita mwanamke wa Ufaransa, Jeanne Calment kama mtu mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kuishi. Calment alifariki mwaka 1997 akiwa na umri wa miaka 122.
Mir ameoa mwanamke mwenye miaka takribani 80, Misra, na alishawahi kuishi na wake wengine wanne, limeripoti jarida la Kashmir Life.
Anaweza kuendelea kutembea kwa msaada wa familia yake, amebakiwa na uwezo kidogo wa kuona, na anaweza kuzungumzia kuhusu maisha yake ya sasa kwa lugha yake ya asili ya Pahari.
Mir aliambatana na baba yake Matulli kuwa mfanyabiashara wa matunda na njugu na mara kwa mara alimsindikiza kwenda mji mkuu wa Pakistan, Karachi.
Katika miaka ya 1890, alioa mke wake wa kwanza na kuishi naye nchini Pakistan hadi mke huyo alipofariki mapema katika miaka ya 1900.
"Hakukuwa na mipaka kati ya India na Pakistan kwa wakati huo. Ilikuwa rahisi kwenda Muzaffarbad kuliko Srinagar," alilieleza jarida hilo.
"Nilikuwa najishughulisha na familia ya biashara mjini Karachi ambao walikuwa wakinunua nafaka kutoka kwangu. Nilichukua njugu kutoka Kashmir ambazo zilikuwa maarufu sana nchini Karachi."
Mara baada ya kuwa mjane, alirejea mahali alipozaliwa katika kijiji cha Bihjama kilichopo katika wilaya ya Uri, na kwenda kuoa zaidi ya mara nne.
Misra, mkewe wa tano, alilieleza Kashmir Life: "Uzoefu wake ni wa kidhalimu. Amekuwa akinisimulia simulizi za tetemeko la ardhi, ambalo liliyakumba maeneo ya Sopore na Pattan katika miaka ya 1880 na, wakati akiwa kwenye safari ya kibiashara kwenda Karachi, aliokoa maisha ya watu wengi mjini Gadiduptata.
"Ni shuhuda wa baadhi ya matukio muhimu katika historia kwenye karne iliyopita."
Baada ya tetemeko la ardhi, Mir alikuwa 'mwenye furaha mno' kukuta familia yake ikiwa hai na salama.
Mir pia alisema maisha yamekuwa magumu zaidi kufuatia maisha ya kisasa kutawaliwa zaidi na teknolojia iliyopiga hatua.
"Huku maisha yakianza kuwa rahisi, watu hawakuweza kuishi kwa urahisi na wenzao," alisema.
Mjukuu wake Abdul Rashid alisema afya ya Mir na kumbukumbu ziliathirika tangu alipofanyiwa upasuaji wa jicho miaka kumi iliyopita.
Alilieleza jarida hilo: "Tulikuwa tukisikiliza simulizi nyingi kutoka kwake wakati tulipokuwa vijana ambazo hatukuzikinai. Ni mtu wa kuvutia ambaye ameyaona maisha kwa ukaribu kabisa."
Kabla ya habari ya Mir kubainika, ilidhaniwa kwamba mtu wa mwisho kuwa aliishi katika karne ya 19 alikuwa Jiroemon Kimura, aliyezaliwa Aprili 19, 1897.
Kimura alifariki mwezi uliopita huko Kyotango, Japan, akiwa na umri wa miaka 116, akiacha watoto saba, wajukuu 14, vitukuu 25 na vilembwe 15.
Taji hilo la mtu mzee zaidi duniani anayeishi linashikiliwa na Misao Okawa mwenye umri wa miaka 115 anayeishi Osaka, Japan.

No comments:
Post a Comment