Sunday, June 30, 2013

MZEE MANDELA AANDIKA WOSIA NA KUTAJA MAHALI ANAPOTAKA KUZIKWA...

KUSHOTO: Mzee Nelson Mandela. KULIA: Eneo walilozikwa mababu wa Mandela ambalo naye anataka akazikwe atakapofariki.
Mzee Nelson Mandela ameandika wosia kwenye karatasi moja ya ukubwa wa A4 ambamo ameagiza azikwe katika milima iliyojitenga nyumbani kwa mababu zake huko Qunu, imebainika.

WAPENZI WADONDOKA NA KUFA WAKATI WAKIFANYA MAPENZI DIRISHANI...

Wapelelezi wakifunika miili ya wapenzi hao eneo la tukio.
Wapenzi wameanguka na kufa baada ya dirisha walipokuwa wakifanyia mapenzi kufunguka ghafla nchini China.

WINNIE MANDELA AZUNGUMZIA HALI YA MUMEWE WA ZAMANI...

Winnie Mandela akizungumza na vyombo vya habari.
Nelson Mandela anaonesha 'maendeleo makubwa' katika afya yake tangu siku chache zilizopita, mkewe wa zamani alisema jana.

MWANAMKE ALIYEMKATA UUME MUMEWE AFUNGWA MAISHA GEREZANI...

Catherine Kieu.
Mwanamke mmoja wa California ambaye alituhumiwa kukata uume wa mumewe kabla ya kuutupa kwenye mashine ya kusagia taka amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

CHEKA TARATIBU...

Jamaa kaenda baa na mke wake wa ndoa. Wakati wakiendelea kupata vinywaji pale, ghafla akatokea changudoa mmoja na kwenda moja kwa moja kwa mke wa jamaa na kumnong'oneza sikioni: "Akulipe kabisa kabla hujaenda kulala naye, jamaa mgumu sana kulipa!!" Duh, kasheshe...

UVUMILIVU WAMSHINDA OBAMA, SASA AWAJIBU WAKENYA...

Rais Barack Obama.
Wakati Rais wa Marekani, Barack Obama amesema asingeweza kufanya ziara Kenya kutokana na Rais wake, Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Rutto kukabiliwa na mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC), pia amehadharisha Afrika kuhakikisha kuwa kampuni za kigeni zinaajiri wafanyakazi wazalendo ili wawekeze nchini mwao.

JICHO LA TATU...


MAITI AZIKWA MARA MBILI MWANZA...

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwili wa kijana umezikwa mara mbili,  baada ya maziko ya kwanza kufanywa na wanakijiji cha Mwalubungwe Kata ya Hungumalwa  Kwimba, Mwanza, baada ya kumuua wakidhani jambazi na kumzika bila nguo wala sanda.

Saturday, June 29, 2013

ALIYEMBAKA BIBI MSTAAFU MIAKA 16 ILIYOPITA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA...

KUSHOTO: Wendell Baker. KULIA: Hazel Backwell enzi za uhai wake.
Mtu aliyembaka mstaafu chumbani kwake miaka 16 iliyopita amehukumiwa kifungo cha maisha jela kufuatia kurejewa tena kwa hukumu chini ya sheria hatarishi.

KODI YA PETROLI YASHUSHWA, USHURU WA SIMU ZA MKONONI WAFUTWA...

Mfumo mpya wa Bunge kuanza na bajeti za kisekta na kumalizia na Bajeti ya Serikali pamoja na uundwaji wa Kamati ya Bajeti, umeonesha makali yake kiasi na kuilazimisha Serikali, kushusha kodi ya petroli na kufuta ushuru wa kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu.

OBAMA AWASILI AFRIKA KUSINI, KUTOKWENDA KUMTEMBELEA MZEE MANDELA...

Rais Barack Obama akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili nchini Afrika Kusini jana jioni.
Rais Barack Obama amewasili Afrika Kusini jana jioni, lakini sasa hatamtembelea kinara wa kupinga ubaguzi wa rangi, Mzee Nelson Mandela hospitalini alikolazwa mjini Pretoria katika kituo chake cha pili cha ziara yake ya nchi tatu za Afrika.

JICHO LA TATU...


PINDA AHITIMISHA BUNGE LA BAJETI KWA KUTOA ONYO KALI...

Mizengo Pinda.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, jana alihitimisha mjadala wa Bunge la 10 lililojadili na kupitisha Bajeti ya Serikali na bajeti za wizara mbalimbali, huku akisisitiza umuhimu wa kila mbunge kuwajibika kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani na utulivu.

MWANAUME ADAI KUISHI MIAKA MITANO BILA KULA CHAKULA...

Kirby de Lanerolle.
Mwanaume mmoja nchini Sri Lanka anadai ameweza kuishi bila kula chakula kwa miaka mitano iliyopita.
Ingawa wataalamu wanaamini wanadamu wanaweza tu kuishi kwa miezi miwili bila kula, Kirby de Lanerolle anasisitiza alikuwa akihitaji tu hewa safi kama kirutubisho.

Friday, June 28, 2013

WAGANGA WA JADI AFRIKA KUSINI WAMFANYIA TAMBIKO MZEE MANDELA...

Waganga wa Jadi nchini Afrika Kusini.
Sasa ni dhahiri kuwa maisha ya kiongozi wa zamani wa nchi hii, Nelson Mandela yamo hatarini kutokana na kwamba anaishi kwa msaada wa mashine, imethibitishwa na mmoja wa wazee wa ukoo wa kiongozi huyo.

JICHO LA TATU EXTRA...


SABABU ZA OBAMA KUTOKWENDA KENYA, NIGERIA ZAANIKWA...

Rais Barack Obama.
Rais Barack Obama amepongeza hatua zilizopigwa na Afrika katika kujenga demokrasia, imeelezwa kutoka Dakar, Senegal.

CHEKA TARATIBU...

Mke kamwomba mumewe pesa ya kununulia nyama kwakuwa aliitamani sana. Mume akamshika mkono mkewe na kwenda naye hadi kwenye kioo kisha akatoa Shilingi elfu tano na kusema:

UNENE ULIOKITHIRI WAMWOKOA BIBI ASIPANDISHWE KIZIMBANI...

Rita Astbury akionesha picha aliyopiga na wajukuu zake.
Mwanamke aliyenenepeana amekwepa kupandishwa kizimbani sababu maofisa waliamua kuwa kumtoa kwenye nyumba yake ingekuwa hatari.

MARAIS WA MAREKANI WAIBEBA TANZANIA...

Balozi Ombeni Sefue.
Tanzania imetajwa kuwa nchi pekee Afrika iliyobahatika kutembelewa na marais watatu wa Marekani wakiwa madarakani.

JICHO LA TATU...


Thursday, June 27, 2013

BINTI WA MIAKA 10 AFARIKI DUNIA SIKU CHACHE BAADA YA KUBAKWA NA WAVULANA WANNE...

Wanawake wakiandamana mitaani kulaani vikali vitendo vya ubakaji nchini humo.
Binti mmoja mwenye umri wa miaka 10 amefariki dunia siku chache baada ya kubakwa na kundi la wavulana wanne mjini Mumbai, polisi walisema jana.

FAMILIA YATOFAUTIANA MAHALI ATAKAPOZIKWA MZEE MANDELA...

Watu mbalimbali wakiendelea kuweka meseji za kumtakia afya njema Mzee Mandela pamoja na maua.
Suala la mahali atakakozikwa Rais wa zamani Nelson Mandela atakapofariki dunia, limesababisha tofauti ndani ya familia yake.

MWANAMKE ASHINDIA SODA KWA MIAKA 16 NA KUAMBULIA MARADHI YA MOYO...

Mwanamke mwenye umri wa miaka 31 ambaye alikimbizwa hospitali kutokana na matatizo ya moyo amewafichulia madaktari kwamba alikuwa akinywa soda tu tangu alipokuwa msichana mdogo.

CHEKA TARATIBU...

Daktari hospitali moja ya vichaa kawapa vipande vya sabuni wagonjwa wake wawasiliane na wapenzi wao.

MANDELA AFUMBUA MACHO NA KUTABASAMU ALIPOSIKIA ZIARA YA OBAMA AFRIKA KUSINI,,,

Mzee Nelson Mandela.
Mzee Nelson Mandela alifungua macho yake na kutabasamu pale alipoambiwa kuhusu ziara ijayo ya Barack Obama nchini Afrika Kusini, kwa mujibu wa binti yake.

WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI WALISHWA MIHADARATI KWENYE BARAFU...

Mojawapo ya aina za mihadarati.
Baadhi za chakula ikiwamo mikate na barafu zinazouzwa kwenye shule za msingi zinadaiwa kuwekwa dawa za kulevya hali inayosababisha watoto kuathirika.

NDEGE YENYE ABIRIA 325 YALIPUKA INJINI WAKATI IKIJIANDAA KURUKA...

Injini ya ndege hiyo ikiwaka moto wakati ikiwakwenye harakati za kuruka.
Hili ni tukio la kushangaza pale moja ya injini za ndege iliyobeba zaidi ya abiria 300 ilipolipuka wakati ikijiandaa kuruka.

JICHO LA TATU...


ZIARA YA BARACK OBAMA YAFUNGA BARABARA KADHAA DAR...

Ulinzi umeimarishwa katika mitaa ya Dar es Salaam huku baadhi ya barabara zikifungwa kwa kipindi maalumu kwa ajili ya ziara ya Rais Barack Obama wa Marekani nchini Julai 1 na 2.

Wednesday, June 26, 2013

UCHAGUZI WA MADIWANI ARUSHA SASA KUFANYIKA JULAI 14...

Jaji Damian Lubuva.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeahirisha tena uchaguzi wa madiwani kata nne za Arusha hadi Julai 14 kuruhusu kurejea utulivu baada ya mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa kampeni wa  Chadema ulioathiri uchaguzi huo wiki iliyopita.

WANASIASA WAICHIMBIA KABURI SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR...

Balozi Seif Ali Iddi.
Makamu wa Pili wa  Rais, Balozi Seif Ali Iddi amehadharisha kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa inaweza kumeguka iwapo viongozi wataendelea kutumia vibaya majukwaa ya kisiasa kutoa kauli za chuki na matusi na kukashifu Serikali kwa maslahi binafsi.

JICHO LA TATU...


OBAMA ABANWA KUMTEMBELEA MZEE MANDELA MAHUTUTI...

Mzee Nelson Mandela.
Ndugu wa karibu wa Rais wa zamani Nelson Mandela na machifu wa familia ya kifalme ya Abathembu jana asubuhi walikutana nyumbani kwake Qunu, Cape Mashariki.

Tuesday, June 25, 2013

ZAIDI YA ASILIMIA 50 YA WABUNGE WAIPITISHA BAJETI YA SERIKALI...


Dk William Mgimwa.

Bunge jana lilipitisha Bajeti ya Serikali ya Sh trilioni 18.2 kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa na wabunge wa Bunge hilo na kuiwezesha Serikali sasa kuanza kazi rasmi Julai mosi.

TAKUKURU YAOKOA SHILINGI BILIONI 3.2 ZA SERIKALI KWENYE MALIPO 'FEKI'...


George Mkuchika.

Serikali imefanikiwa kuokoa jumla ya Sh.bilioni 3.2 kutokana na  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kusimamisha malipo baada ya kuonekana kuwa si halali.

JICHO LA TATU...


TANZANIA YANG'ARA KWA AMANI DUNIANI...



Tanzania imeelezwa kuwa nchi yenye amani zaidi na utulivu mkubwa kuliko nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ikishikilia nafasi ya 55 duniani kati ya nchi 162 ambako utafiti kuhusu hali ya amani na usalama umefanyika.

Sunday, June 23, 2013

MPASUKO WAIBUKA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR...

Moja ya vikao vya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar imeanza kupata ufa kutokana na mawaziri kukosa umoja na kujitenga katika shughuli za Serikali na kushindwa kuwapa mapokezi viongozi wa kitaifa.

SAMWELI SITTA AAGWA RASMI KAMA SPIKA...

Samweli Sitta.
Bunge la Jamhuri ya Muungano juzi usiku lilimuaga aliyekuwa Spika, Samweli Sitta na kumsifu kwa kutetea maslahi ya watumishi wa Bunge na kuendesha Bunge la Spidi na Viwango.

HALI YA MANDELA TETE, ASHINDWA KUVUMBUA MACHO KWA SIKU KADHAA...

Mzee Nelson Mandela.
Mzee Nelson Mandela ameendelea kuwa katika hali mbaya hospitalini jana baada ya kubainika kwamba gari la wagonjwa lililombeba Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini kwenda hospitali limeharibika.

MREMA ASEMA WANASIASA NDIO CHANZO CHA VURUGU...

Augustine Mrema.
Wanasiasa wanaotafuta umaarufu kwa nguvu, wametajwa kuwa ndio chanzo cha vurugu mbalimbali nchini hivyo, wametakiwa kujifunza kutoka kwa wanasiasa wakongwe ambao licha ya kuwa na wafuasi wengi miaka ya nyuma, hawakuwahi kumwaga damu.

ASKOFU MKUDE ATAKA WASIOTAKA NCHI ITAWALIKE WABANWE...

Mhashamu Telesphor Mkude.
Siku chache baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutaka Serikali iachwe ifanye kazi yake katika kudhibiti vurugu zinazoibuka kila kukicha, Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude naye ameitaka Serikali kuwadhibiti wote wasiotaka nchi itawalike.

JICHO LA TATU...


MWANAFUNZI WA UDAKTARI ABAKWA NA KUNDI LA WANAUME AKITOKA KUJISOMEA...

Mwanafunzi wa udaktari mwenye miaka 22 amebakwa na kundi la wanaume watatu ambao walimnyaka kutoka eneo la chuo kikuu kimoja chenye sifa njema nchini India.

Saturday, June 22, 2013

MBUNGE MACHALI WA NCCR-MAGEUZI ASHAMBULIWA NA VIBAKA NJIANI...

Mbunge Moses Machali akiwa hoi kitandani baada ya kushambuliwa na vibaka jana.
Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali amesema alivamiwa na watu wanne ambao walimshambulia na kumjeruhi akiwa meta 30 kabla ya kufika nyumbani kwake.

JERAHA USONI KWA MTOTO LAIKOSESHA FAMILIA SAFARI YA NDEGE...

Jeraha usoni kwa mtoto huyo, Robyn lililoiponza familia hiyo kwenye ndege.
Familia moja imetupwa nje ya ndege waliyokuwa wasafirie kwenda kwao baada ya likizo sababu ya mpasuko kidogo kwenye uso wa binti yao ulikuwa kinyume cha tahadhari za kiafya na usalama.

NDEGE YENYE ABIRIA 218 YATUA KWA DHARURA BAADA YA TAA YA MAFUTA KUWAKA...

Chumba cha marubani.
Ndege Boeing 787 ya Shirika la United iliyokuwa ikiruka kutoka London kwenda Houston ililazimika kugeuza na kuelekea Newark, New Jersey, juzi sababu ya taa inayoashiria upungufu wa mafuta ya injini kuwaka, ikiwa ni ndege mpya ya pili ya Boeing kutua kwa dharura wiki hii.

MICHAEL JACKSON AWA MTU PEKEE DUNIANI KUKAA SIKU 60 BILA KULALA...

JUU: Dk Conrad Murray. CHINI: Catherine Jackson. KATIKATI: Michael Jackson. KULIA: Dk Charles Czeisler.
Michael Jackson alifikisha siku 60 bila kulala, na kumfanya awe mtu pekee kuwahi kufanya hivyo, mtaalamu wa usingizi amedai.

JICHO LA TATU...