Wednesday, August 7, 2013

MJAMZITO AFA KWA KUANGUKIWA NA MTI AKIPUNGA UPEPO BUSTANINI...

Tawi hilo la mti lililochukua uhai wa mwanamke huyo mjamzito.
Mwanamke mmoja mjamzito akifurahia siku nzuri kwenye benchi la bustani moja jijini New York amefariki dunia baada ya kuangukiwa na tawi la mti kichwani.

Tuesday, August 6, 2013

JOHN TENDWA ASTAAFU RASMI USAJILI WA VYAMA VYA SIASA...

John Tendwa.
Baada ya misukosuko ya kisiasa ya hapa na pale na hasa kulalamikiwa na baadhi ya vyama vya siasa nchini, hatimaye Msajili wa Vyama hivyo, John Tendwa amestaafu utumishi wa umma.

ZANZIBAR WAIKATAA KODI YA LAINI ZA SIMU, SMZ YADAI HAIKUSHIRIKISHWA...

Mzozo wa kodi ya laini za simu, unaotarajiwa kumalizwa   katika mkutano ujao wa Bunge, umefikia mwisho Zanzibar, baada ya wawakilishi kuikataa rasmi.

JICHO LA TATU...


MAKADA WATANO WA CHADEMA WAFUTIWA MASHITAKA YA UGAIDI...

Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora, imefuta mashitaka ya ugaidi yaliyokuwa yakikabili makada watano wa Chadema na kubakiza mashitaka ya kummwagia tindikali kada wa CCM, Igunga, Musa Tesha.

Monday, August 5, 2013

WANAFUNZI 9,000 WAKATALIWA KUJIUNGA NA VYUO VYA ELIMU YA JUU...

Jengo la Nkrumah lililoko Chuo Kikuu cha Dar es Salaam eneo la Mlimani.
Wanafunzi 8,805 walioomba kujiunga na masomo ya shahada ya kwanza katika vyuo vya elimu ya juu nchini, kwa mwaka wa masomo 2013/2014, wamekataliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

ALIYEKUWA AUAWE KESHOKUTWA AKUTWA KAJINYONGA JELA...

Billy Slagle.
Muuaji anayekabiliwa na adhabu ya kifo Jumatano ya wiki hii, amekutwa amenyongwa kwenye selo yake Jumapili, Ohio alikokuwa akisubiria kutekelezwa kwa hukumu yake ya kifo, maofisa wa gereza wamesema.

JICHO LA TATU...


WASICHANA WA SHULE WAISHI KWA HOFU YA KUBAKWA SUMBAWANGA...

Bweni la wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bomalang'ombe iliyoko wilayani Kilolo, mkoa wa Iringa. Ukosefu wa mabweni madhubuti kumekuwa kukichangia vitendo vya kubakwa kwa wanafunzi wa kike.
Wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari Mzindakaya kijijini Kaengesa, wameelezea vitendo hatari wanavyokabiliwa navyo vya kubakwa na kudhalilishwa kijinsia mara kwa mara, kutokana na kukosa uwezo wa kuishi katika mabweni kwa usalama.

Sunday, August 4, 2013

AZINDUKA KWENYE ULEVI NA KUKUTA UUME WAKE UMENYOFOLEWA NA MBWA...

Geraldo Ramos akiwa kajipumzisha nyumbani baada ya kutoka hospitali.
Mwanaume mmoja mwenye miaka 64 ameelezea jinsi alivyopoteza fahamu baada ya kunywa kupita kiasi usiku mzima na kuzinduka akiwa hana uume wake.

MWALIMU WA KIKE KORTINI KWA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA MWANAFUNZI WAKE...

Warnick (kulia) alihitimu kwenye shule hiyohiyo (pichani) aliyokuja kufundisha.
Mwalimu mmoja mwenye miaka 22 huko New Jersey amekamatwa Ijumaa kwa tuhuma za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mmoja wa wanafunzi wake wa kiume mwenye miaka 15 katika Sekondari ya Juu ya Wall Township, ambako ni mwalimu wa Kiingereza wa Darasa la 9.

JICHO LA TATU...


AWA MTU WA KWANZA DUNIANI KUTEMBELEA NCHI 201 KWA MIAKA MINNE BILA KUPANDA NDEGE...

Graham Hughes akiinua juu shampeni kushangilia kukamilisha ziara yake Sudani ya Kusini.
Imememchukua Graham Hughes takribani miaka minne kutembelea mataifa 201 na kuwa mtu wa kwanza kuzunguka dunia bila kupanda ndege.

Saturday, August 3, 2013

BIASHARA YA MAFUTA YA UBUYU SASA YADODA...

Wasindikaji wa mafuta ya ubuyu mkoani Dodoma wamesimamisha uzalishaji kutokana na ukosefu wa wateja baada ya Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA), kutamka kuwa mafuta hayo ni hatari kiafya.

MATUSI NA KEJELI ZA KAGAME ZAMDUWAZA RAIS KIKWETE...

Rais Paul Kagame (kushoto) na Rais Jakaya Kikwete.
Baada ya kushambuliwa kwa kejeli na Rwanda, Rais Jakaya Kikwete amevunja ukimya na kueleza kushangazwa na kauli hizo na maneno yasiyofaa yanayotolewa na viongozi wa nchi hiyo dhidi yake na Tanzania.

JICHO LA TATU...


MWAROBAINI WA KUPAMBANA NA UJAMBAZI WAPATIKANA...

Baadhi ya silaha zilizokamatwa na polisi kwenye moja ya matukio ya ujambazi hapa nchini.
Jeshi la Polisi nchini katika kupambana na uhalifu limekuja na mbinu mpya ya kutambua wahalifu kwa kutumia gari maalumu ambalo lina uwezo wa kuchukua taarifa, alama za vidole na picha katika matukio ya uhalifu na kuzihariri.

Friday, August 2, 2013

CHAMA CHA RAIS MUGABE CHAZOA VITI LUKUKI VYA UBUNGE ZIMBABWE...

Habari zilizopatikana muda mfupi uliopita zinasema, Robert Mugabe ameshinda theluthi mbili ya viti vyote vya ubunge katika uchaguzi uliofanyika wiki hii nchini Zimbabwe - ambao makundi mawili makubwa ya waangalizi kutoka Afrika  yamethibitisha 'huru na wa amani'.

MKURUGENZI WA MASHITAKA AFAFANUA KESI DHIDI YA PINDA...

Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Eliezer Feleshi, amesema haoni mantiki yoyote au uhalali wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), kumshitaki Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

UCHAGUZI MKUU ZIMBABWE NI KICHEKESHO KIKUBWA...

Rais Robert Mugabe (kushoto) na Morgan Tsvangirai.
Wakati upinzani nchini ukidai kuwa uchaguzi uliofanyika juzi ulikuwa kichekesho kikubwa, chama tawala kimedai kuwa mgombea wake, kiongozi mkongwe Robert Mugabe, amepata ushindi wa kishindo.

JELA SASA YANUKIA KWA SHEKHE PONDA...

Shekhe Ponda Issa Ponda.
Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu, Shekhe Ponda Issa Ponda, yuko hatarini kufutiwa kifungo cha nje, iwapo Polisi itathibitishia Mahakama iliyomtia hatiani, kuwa ametenda kosa akiwa chini ya uangalizi wa kimahakama.

MNENGUAJI AJINGUNDUA KUWA MJAMZITO WA KUJIFUNGUA BAADA YA KUFIKA HOSPITALI...

Mtoto wa mnenguaji huyo, Jack Arthur.
Mnenguaji mmoja ambaye alipelekwa hospitali na mama yake wakati alipoanza kusumbuliwa na maumivu ya tumbo alipatwa na mshituko kugundua alikuwa leba na karibu kujifungua mtoto.

JICHO LA TATU...


MREMBO SHINDANO LA MISS AFRICA AUAWA KWA KUCHOMWA VISU...

Lina Keza (kulia). Nyuma yake ni jengo yalikofanyika mauaji hayo.
Mrembo chipukizi amekutwa amekufa kwa kuchomwa kwa visu huku binti yake wa miaka mitatu 'akilia pembeni yake kwenye dimbwi la damu', wamesema marafiki jana.

Thursday, August 1, 2013

SERIKALI YAFANYA UPYA UTAFITI KUHUSU MAFUTA YA UBUYU...

Moja ya aina za bidhaa za mafuta ya ubuyu.
Utata wa kauli kuhusu usalama wa mafuta ya ubuyu, umesababisha Serikali kuyafanyia utafiti na hivi karibuni itatoa tamko la kumaliza gumzo hilo.

MAMA ASIMULIA MACHUNGU YA KUISHI GEREZANI NA BINTI YAKE WA MIEZI MINANE...

Khadija Shah akiwa na binti yake, Malaika.
Mwanamke mmoja wa Uingereza anayetuhumiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin amezungumzia maumivu yake makali katika malezi ya binti yake mdogo ndani ya selo katika gereza nchini Pakistan.

TBS YAZINYANG'ANYA KAMPUNI 48 LESENI ZA ALAMA ZA UBORA...

Maji ya kunywa ya chupa.
Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limesitisha leseni za alama za ubora ya TBS, katika bidhaa za kampuni 48, zikiwamo za maji ya kunywa, magodoro, taulo za wanawake, mvinyo na vifaa vya magari.

JICHO LA TATU...


MWANAMKE ALIYEKUWA AKINYWA UNITI 350 ZA POMBE KWA WIKI AISHIA HOSPITALI AKIPUMULIA MASHINE...

Patricia Murphy (katikati) kabla ya kuangukia kwenye ulevi na kulia akiwa amelazwa hospitalini.
Kiasi cha juu kabisa cha pombe kilichopendekezwa kutumiwa kwa wanawake ni kati ya uniti mbili na tatu kwa siku, na kisizidi uniti 14 kwa wiki.

SHEKHE PONDA ASAKWA NA POLISI ZANZIBAR KWA KUHATARISHA AMANI...

Shekhe Ponda Issa Ponda.
Polisi Zanzibar inamsaka Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Shekhe Ponda Issa Ponda, kwa tuhuma za kuendesha mihadhara ya kidini katika misikiti kisiwani hapa, yenye kuashiria uvunjifu wa amani.