![]() |
Tawi hilo la mti lililochukua uhai wa mwanamke huyo mjamzito. |
Mwanamke mmoja mjamzito akifurahia siku nzuri kwenye benchi la bustani moja jijini New York amefariki dunia baada ya kuangukiwa na tawi la mti kichwani.
Mashuhuda waliojawa na hofu katika Bustani ya Kissena huko Flushing, Queens, wameelezea jinsi Yingyi Li, mwenye umri wa miaka 30, alivyominywa chini ya mti wa mwaloni, akimiminika damu nyingi kutoka kichwani.
Wapinzani wa Meya wa New York Michael Bloomberg wakawa wa kwanza kunyoosha vidole kwamba kifo hicho cha mwanamke huyo, aliyeelezewa kuwa na takribani miaka 30, hakiwezi kuitwa ajali sababu ni matokeo ya miaka kadhaa ya utunzaji mbovu wa miti ya zamani katika bustani kote jijini humo.
Hili ni tukio la 12 lililosababisha majeraha kwa kipindi cha zaidi ya wiki nane," alisema Geoffrey Croft, rais wa Wanasheria wa New York City Parks.
"Tumekuwa tukiliambia jiji kukagua kwa umakini miti yake, kutunza miti yake, na ni ukatili."
Mashuhuda walisema ilikuwa jioni tulivu katika Bustani ya Kissena ndipo Yingyi alipogongwa na mti.
Daktari mmoja wa dharura ambaye anadhaniwa alikuwa bustanini hapo alikimbialia eneo la tukio na haraka akamtoa na kumkimbiza hospitalini, lakini akatangazwa kufariki mara tu alipofikishwa hapo.
Haifahamiki Yingyi alikuwa na ujauzito wa muda gani au kilichoendelea kwa mtoto wake huyo aliyekuwa tumboni.
Sam Kim alisema mti huo wa mwaloni ulianguka ghafla bila tahadhari yoyote.
"Tulikuwa tumesimama mahali hapo, na ghafla tukasikia kitu kikianguka kwa sauti na kishindo kikubwa," alisema shuhuda.
"Hivyo marafiki zangu na mimi - tulikimbilia huko, na tulipofika pale, tulimwona msichana mmoja aliwa amelala huku sura yake ikitazama ardhini na damu ikitiririka kwa kasi kutoka kichwani kwake."
Mwanamke wa pili aliyekuwa amekaa kando ya Yingyi alipata majeraha kidogo. Alikataa kupatiwa matibabu.
No comments:
Post a Comment