![]() |
Geraldo Ramos akiwa kajipumzisha nyumbani baada ya kutoka hospitali. |
Mwanaume mmoja mwenye miaka 64 ameelezea jinsi alivyopoteza fahamu baada ya kunywa kupita kiasi usiku mzima na kuzinduka akiwa hana uume wake.
Majirani wa Geraldo Ramos walidai kwamba alikuwa ameshambuliwa na mbwa wakati akiyumbayumba bila nguo maeneo ya Jamhuri ya Dominika huku akiwa amelewa chakari.
Lakini Ramos, mkazi wa Santiago, haamini maelezo yao ya matukio na hakubaliniani kabisa kuhusu jinsi alivyofikia kunyofolewa kiungo hicho.
Alikieleza kituo kimoja cha televisheni mjini humo kwamba anachokumbuka ni alipozinduka na kujikuta akiwa amepelekwa hospitalini kwa upasuaji wa dharura.
Mbwa huyo ambaye anasemekana kumshambulia hajaweza kupatikana, wala uume huo wa Ramos.
Ramos sasa analazimika kuvaa neli ya kuingiza uonevu katika mishipa mwilini na alirekodiwa nyumbani kwake akirejesha nguvu tena mwilini baada ya ugonjwa.
Anasema kwamba amejifunza kutokana na makosa - Ramos alikieleza kituo cha Noticias Sin kwamba analazimika kuacha ulevi kuanzia sasa.
Wakati simulizi za shambulio la mbwa huyo wa jirani yake linaweza kuonekana kushughulikiwa kwa mbali kidogo, si lote lisiloaminika.
Mwanaume mmoja aliyepooza mjini Arkansas alizinduka Julai na kukuta kwamba mbwa wake amekula moja ya korodani zake.
Mwanaume mmoja wa Brazili wakati huohuo alinyofolewa vidole vyake vya mguuni na mbwa wake wa kufugwa nyumbani.
Na inaonekana si mashambulio ya mbwa pekee ambayo wanaume wanatakiwa kuwa makini nayo - mwanaume mmoja alikimbizwa hospitali nchini Israeli baada ya nyoka kumng'ata kwenye uume wake wakati alipokuwa amekwenda chooni kujisaidia.
Kwa bahati nyoka huyo alikuwa wa jamii ile isiyokuwa na sumu kali na mwanaume huyo akapata majeraha kidogo.
No comments:
Post a Comment