Monday, March 31, 2014

YASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMATATU...

WABUNGE SASA KUANZA KUPITIA RASIMU YA KATIBA, KANUNI ZAWEKWA KIPORO...

Wajumbe wa Bunge la Katiba.
Bunge Maalumu la Katiba linaendelea na kikao chake na miongoni mwa shughuli zinazotarajiwa kufanywa  kuanzia leo, ni kurekebisha baadhi ya kanuni za uendeshaji wake na kuanza kujadiliwa kwa ibara zilizopo ndani ya rasimu ya Katiba.

WATU 21 WAFARIKI, 10 WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA HIACE RUFIJI...

Watu 21 wamekufa na 10 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi dogo la abiria aina ya Hiace na lori.
Ajali hiyo ilitokea juzi katika kijiji cha Mkupuka kata ya Kibiti wilayani Rufiji mkoani Pwani.

WASSIRA ACHEKESHA WAOMBOLEZAJI KWENYE MSIBA WA RC TUPPA...

Stephen Wassira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira alisababisha kicheko kwa waombolezaji katika maziko ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Gabriel Tuppa baada ya kulalamikia masharti yanayoambatana na safari ya kwenda peponi.

YASEMAVYO MAGAZETI YA LEO...




SHIVJI AONYA BUNGE LIKIPITISHA SERIKALI TATU HAKUNA MUUNGANO...

Profesa Issa Shivji.
Gwiji wa masuala ya sheria za katiba nchini, Profesa Issa Shivji amewataka vijana kujiepusha na wanasiasa wenye uchu wa madaraka ambao kwa sasa wanang'ang'ania muungano wa serikali tatu ili kukidhi matakwa yao.

Sunday, March 30, 2014

HII NDIO AJALI YA TRENI ILIYOKATISHA MAISHA YA WATU WAWILI MPWAPWA...

Ajali ya kichwa cha treni kilichotumbukia mtoni na kusababisha watu wawili kupoteza maisha na wengine saba kujeruhiwa huku wengine hawajulikani walipo.

VYAMA VYA UPINZANI VYAUNDA UMOJA WAO WA KATIBA KUSHAWISHI WANANCHI...

Wajumbe wakifuatilia Bunge Maalumu la Katiba.
Baada ya kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ndani ya Bunge Maalum la Katiba, vyama vya siasa vya upinzani, vimeunda umoja wa aina hiyo nje ya bunge hilo (UKAWA-nje) na kupanga kuwashawishi wananchi nchi nzima kudai Katiba yenye kujali maslahi yao.

AJALI YATAFUNA MAISHA YA WANAWAKE 12 KWA MPIGO WAKIENDA MSIBANI...

Kamanda Robert Boaz.
Watu 14 wamefariki dunia na wengine 14 kujeruhiwa katika matukio tofauti yaliyohusisha ajali ya magari kugongana na wengine waliopoteza maisha baada ya kichwa cha treni kutumbukia mtoni.

BAKWATA YAUNGANA NA KIKWETE, NAO WAKATAA SERIKALI TATU...

Mufti Issa Shaaban Simba (kulia) akiteta jambo na Rais Jakaya Kikwete.
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA) limesema Waislamu wanataka Katiba itakayojali maslahi kwa wananchi wa pande zote mbili Bara na Visiwani na kuhakikisha Muungano unadumu.

YASEMAVYO MAGAZETI YA LEO....




Saturday, March 29, 2014

WAJUMBE WAKUBALIANA SUALA LA KURA KUPISHA MCHAKATO UENDELEE...

Wajumbe Bunge Maalum la Katiba wakipiga kura.
Hatimaye Bunge Maalumu la Katiba limemaliza mvutano wa Kanuni, hasa kuhusu kura ya wazi au ya siri katika kufanya uamuzi wa kupitisha ibara na sura za rasimu ya Katiba, kwa kuamua kura zote zitumike kwa kadri mjumbe mmoja mmoja atakavyoona inafaa.

MIKATABA YA MADINI KUREKEBISHWA MAENEO YA TOZO NA KODI...

Kazi ya uchimbaji madini ikiendelea huko Geita.
Serikali kwa kushirikiana na Kampuni kubwa za uwekezaji katika sekta ya madini nchini, imekubaliana kufanya marekebisho katika mikataba iliyosainiwa katika kodi na tozo.

ATAKA BUNGE MAALUMU LA KATIBA LIVUNJWE...

Mwenyekiti Samuel Sitta akisisitiza jambo.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta ameshauriwa kumuandikia barua Rais Jakaya Kikwete, kuomba kuvunjwa kwa bunge hilo linaloendelea mjini Dodoma endapo wajumbe wake watashindwa kuanza kujadili rasimu Jumatatu ijayo.

Friday, March 28, 2014

WAJUMBE BUNGE LA KATIBA WAANZA KUJUTIA MAMILIONI YA POSHO ZAO...

Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanajutia posho wanayoendelea kupata wakati bunge likivurugika mara kwa mara na kusababisha kuahirishwa, hivyo kuzua wasiwasi wa kutotekelezwa  malengo yaliyowapeleka. 

OFISA WA JWTZ AHUKUMIWA KIFUNGO JELA KWA KUGHUSHI...

Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam.
Mwanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Muhsin Kombo amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela baada ya kupatikana na hatia ya kughushi.

KURA YA SIRI, WAZI ZOTE KUTUMIKA KWA PAMOJA...

Hatimaye mvutano kuhusu kura gani itumike, kati ya wazi na siri kufanya uamuzi katika Bunge Maalumu la Katiba, umefikia tamati baada ya Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalumu, kuamua kura zote zitumike kufanya uamuzi mmoja.

BALOZI SEIF IDDI AKANUSHA KAULI YA MAALIM SEIF...

Balozi Seif Ali Iddi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Iddi ametaka wananchi visiwani humo kutotishika na kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad kwamba Wazanzibari wengi walitaka Muungano wa Mkataba.

MWILI WA ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA MARA KUAGWA LEO...

Askari wa FFU wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa John Tupa tayari kwa kusafirishwa.
Mwili wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa unaagwa leo katika ibada itakayofanyika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma.

JICHO LA TATU...


MABEHEWA 'TRENI YA MWAKYEMBE' YAANGUKA...

Mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia jana zimesababisha injini  ya treni kutoka Stesheni kwenda Ubungo Maziwa, kuacha njia na kusababisha mabehewa kuanguka.

Thursday, March 27, 2014

WATOTO WA KIKE WA KITANZANIA WASAFIRISHWA KWENDA KUFANYA UKAHABA CHINA...

Baadhi ya makahaba wenye umri mdogo wakiwa kwenye mawindo yao.
Watoto wa kike wenye umri wa hadi miaka 14 wanadaiwa kufanyishwa biashara ya ukahaba China kutokana na kusafirishwa na baadhi ya Watanzania wasio waaminifu.

MWALIMU WA KIKE ATIMULIWA KAZI KWA KUNOGEWA MAPENZI NA MWANAFUNZI WAKE...

Gary Ralston akiwa kwenye chumba alicholala na mwalimu wake huyo (picha ndogo kushoto) usiku mzima.
Mwalimu aliyeoolewa akiwa katikati ya kashfa ya ngono, amefutwa kabisa kwenye orodha ya walimu.

MAKABURI KUHAMISHWA KINYEREZI KUPISHA UJENZI WA BOMBA LA GESI...

Makaburi 47 yaliyopo katika eneo la Kanisa Katoliki Parokia ya Kinyerezi, Khanga jijini Dar es Salaam yatahamishwa kupisha ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mnazi Bay, Mtwara na Songosongo.

WENYE ASILI YA PEMBA 'WALIA' NA WANAOTAKA KUVUNJA MUUNGANO...

Baadhi ya wakazi wa kisiwa cha Pemba wakiwa katika shughuli zao za kila siku.
Mtandao wa Watanzania wenye asili ya Pemba waishio Bara (NEPPELTA), umehadharisha juu ya chokochoko na chuki zinazolenga kuvunja muungano na kusema ukivunjika, hautawaacha salama.

JICHO LA TATU...


WAFANYAKAZI WA MADUKA YA SHOPRITE WAENDELEA NA MGOMO WAO...

Wafanyakazi hao wakiwa na mabango wakati wakiendelea na mgomo wao huo.
Wafanyakazi wa Shoprite wameendelea kugoma kusisitiza mwajiri wao awapatie stahiki zao kabla hajaondoka nchini.

BUNGE MAALUMU LA KATIBA KUSITISHWA HADI MWAKANI, IKIWA...

Kikao cha Bunge Maalum la Katiba.
Kama mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba utaendelea kama linavyokwenda, uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu, unaweza kusogezwa mbele hadi mwakani.

Wednesday, March 26, 2014

RAIS KIKWETE AVUNJA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA...

Jaji Joseph Warioba.
Rais Jakaya Kikwete ameivunja Tume ya Mabadiliko ya Katiba, baada ya tume hiyo kumaliza kazi iliyopewa na kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Bunge Maalumu.

JICHO LA TATU...


AFARIKI DUNIA BAADA YA KULIPUKIWA NA PETROLI TARIME...

Uuzaji petroli kwenye vidumu.
Watu watatu wamekufa wilayani Tarime katika mazingira tofauti akiwemo anayeuza mafuta ya petroli kwa vidumu.

PAPAA MSOFFE NA WENZAKE WATAKIWA KUMWANDIKIA DPP...

Papaa Msoffe akiwa kwenye gari la polisi.
Mfanyabiashara maarufu Abubakar Marijan (50) 'Papaa Msoffe' na mwenzake Makongoro Nyerere wanaokabiliwa na kesi ya mauaji, wameshauriwa kuandika barua ya malalamiko kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kujua kwa nini jalada la kesi yao linacheleweshwa.

Monday, March 24, 2014

WANAOKOSOA HOTUBA YA RAIS KIKWETE NAO WAKOSOLEWA...

Rais Kikwete alipohutubia uzinduzi wa Bunge la Katiba.
Kitendo cha baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, kukosoa hatua ya Rais Jakaya Kikwete kutoa maoni yake kuhusu rasimu ya Katiba, kimekosolewa.

WATOTO WA KLERUU NA MWAMWINDI WAKUTANA KUMALIZA TOFAUTI ZAO...

Eva Kleruu (kushoto) na Amani Mwamwindi.
Miaka 43 tangu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Wilbert Kleruu alipouawa na mkulima, Said Mwamwindi, watoto wa kwanza wa familia hizo, wamekutana mwishoni mwa wiki kwa mara ya kwanza mjini Iringa kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kumaliza tofauti zao za kihistoria.

JICHO LA TATU...


WAJUMBE BUNGE LA KATIBA WATAKIWA KUACHA UBINAFSI, UCHOYO...

Kingunge Ngombale Mwiru akichangia katika semina hiyo.
Kutokana na kuongezeka mivutano na mpasuko miongoni mwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba,  imeshauriwa njia pekee ya kunusuru mchakato wa kuandikwa kwa Katiba mpya ni wajumbe kuacha ubinafsi, uchoyo na misimamo ya kisiasa badala yake wajenge maridhiano.

Sunday, March 23, 2014

HUYU NDIYE KIGOGO SERIKALINI ANAYEVURUGA VITA DHIDI YA MIHADHARATI...

Wakati Serikali ya Rais Jakaya Kikwete ikifanya kila linalowezekana kuhakikisha inapambana kwa dhati na biashara haramu ya dawa za kulevya, baadhi ya vigogo serikalini wametajwa kutaka kudhoofisha juhudi hizo kwa kukumbatia watuhumiwa waliokamatwa.