Thursday, March 27, 2014

WAFANYAKAZI WA MADUKA YA SHOPRITE WAENDELEA NA MGOMO WAO...

Wafanyakazi hao wakiwa na mabango wakati wakiendelea na mgomo wao huo.
Wafanyakazi wa Shoprite wameendelea kugoma kusisitiza mwajiri wao awapatie stahiki zao kabla hajaondoka nchini.

Miongoni mwa stahiki wanazozihitaji kutoka kwa mwajiri wao ni malipo ya likizo, matibabu, kiinua mgongo na mengine ambayo kwa muda mrefu walikuwa hawajapatiwa.
Akizungumza na mwandishi jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Wafanyakazi hao Bahati Kalolo alisema hadi  Aprili Mosi mwaka huu, kampuni hiyo itakuwa chini ya mwajiri mpya.
Alisema hofu yao si kupoteza kazi, bali ni kupoteza haki zao za msingi kama wafanyakazi.
Alisema kupitia Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) wamepeleka kesi Mahakama ya Kazi na Usuluhishi  wakitaka kupatiwa stahiki zao.
Mgomo huo ulianza juzi kwa kuwakutanisha wafanyakazi wa maduka yote ya Shoprite ya jijini ambayo ni Mlimani City, Pugu na Kamata.

No comments: