![]() |
| Kamanda Robert Boaz. |
Watu 14 wamefariki dunia na wengine 14 kujeruhiwa katika matukio tofauti yaliyohusisha ajali ya magari kugongana na wengine waliopoteza maisha baada ya kichwa cha treni kutumbukia mtoni.
Katika ajali ya gari wanawake 12 waliokuwa wanakwenda kwenye msiba wamefariki dunia papo hapo na wengine saba kujeruhiwa vibaya wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongwa kwa nyuma na kusababisha ajali hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 2:00 usiku, katika barabara kuu ya Moshi-Tanga eneo la Hedaru Tarafa ya Chome Suji, ambapo ajali na kuhusisha magari matatu.
Akieleza mazingira ya ajali hiyo, Kamanda Boaz alisema gari lenye namba za usajili T170 AKZ Toyota Hilux lilikuwa limebeba waombolezaji waliokuwa wakienda kwenye msiba wa mtu aliyefariki baada ya kusombwa na maji, kutokana na mvua kubwa iliyonyesha eneo la Hedaru.
Alifafanua kwamba gari la waombolezaji Toyota Hilux lilikuwa likitokea Hedaru kuelekea Majengo, liligongwa kwa nyuma na gari lenye namba T 299 aina ya Fuso lori lililokuwa likiendeshwa na dereva ambaye hakufahamika jina lililokuwa likitokea Moshi kuelekea Dar es Salaam.
Mara baada ya Toyota Hilux kugongwa nyuma liligongana tena uso kwa uso na gari lingine lenye namba T 737 AKW likiwa na tela namba T776 CCN aina ya Scania Lori, likiendeshwa na Gabriel Daudi (35) likitokea Dar es Salaam kuelekea mjini Moshi.
Baada ya ajali hiyo kutokea ilisababisha vifo vya watu 12 waliokuwa kwenye gari lenye namba T170 AKZ Toyota Hilux, wote wakiwa ni wanawake ambapo dereva wa gari hilo hakufahamika jina lake.
Kamanda Boaz aliwataja marehemu kuwa ni Stela John (45), Salma Kizoka (33), Merry Senzige (49) Neema Daniel (52), Rehema George (29), Sofia Mbike (51) na Mamarita Kalani (55). Wote wakiwa ni wakulima na wakazi wa Kongei-Hedaru.
Aliwataja wengine kuwa ni Mamakalan Stephano (55), Kolina Mmasa (55), Bahati Daudi (25), Farida Kiondo (24) na Maria John (33) wote wakiwa ni wakulima na wakazi pia wa Kongei-Hedaru.
Kamanda Boaz alisema katika majeruhi saba, kati yao watatu hali zao ni mbaya ambao ni Zubeda Mrindoko (42) Mipa Chedieli (29) na Zubeda Mlita (32 ) , ambapo wote wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo mjini Moshi.
Majeruhi wengine ni Joyce Kandogwe (29), Subira Juma (22), Ramadhani Msangi (31) na Adinani Rajabu (31) wote wakiwa ni wakazi wa Kongei-Hedaru, ambapo miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Same.
Kamanda Boaz alisema chanzo cha ajali hiyo ni utelezi wa udongo kujaa barabarani baada ya kusombwa na maji yaliyotokana na mvua , ambapo gari T170 AKZ Toyota Hilux lilipofika eneo hilo lilizima ghafla na gari T299 ANM Fuso lilikuwa nyuma na lilipojaribu kusimama liliteleza na kugonga kwa nyuma Toyota Hilux.
Alisema baada ya hapo gari zote mbili zilihamia upande wa kulia wa barabara na kugongana tena uso kwa uso na gari T 737 AKW lenye tela T776 CCN Scania na gari zote Toyota Hilux na Fuso zikaanguka upande wa kulia, ambapo Jeshi la Polisi limeanza jitihada za kuwasaka dereva wa Toyota Hilux na Fuso ili waweze kufikishwa mahakamani.
Kwa upande wa ajali ya kichwa cha treni kutumbukia mtoni kimesababisha watu wawili kupoteza maisha na wengine saba kujeruhiwa huku wengine hawajulikani walipo.
Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, David Misime alisema ajali hiyo ilitokea baada ya treni ya mizigo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Kigoma kupata ajali na kusombwa na mkondo wa maji katika eneo la Gulwe Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma. Tukio hilo lilitokea juzi saa 8:00 usiku.
Alisema kutokana na wingi na nguvu ya maji hayo yanayotokana na mvua zinazoendelea kunyesha ilifanya kichwa cha treni hiyo kutumbukia kwenye mto Mimo. Waliofariki dunia ni Felix Kalonga na mtu moja aliyefahamika kwa jina moja la Ismail.
Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Hassan Kitambo (89) mkazi wa Kidete, Ramadhani Kanenda (34) na Koplo Respic ambao wamelazwa Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa.
Wengine ni Reuben Ngasongwa (43) na Michael Lupatu (52), ambao wamehamishwa kutoka Hospitali ya Mpwapwa kupelekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Aidha Mohamed Salum na Koplo Mfaume walitibiwa na kuruhusiwa.
Kamanda Misime alisema jitihada zinaendelea kuwatafuta watu wanne ambao bado hawajulikani walipo.

No comments:
Post a Comment