Saturday, November 30, 2013

JANJA YA WABUNGE KUJILIPA ZAIDI YAGUNDULIKA...

Kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano, mjini Dodoma.
Nchi masikini za Afrika ikiwamo Tanzania zinatumia fedha nyingi kulipa wabunge wakati utendaji kazi wa viongozi hao wa kisiasa ni mdogo na hauendani na marupurupu na mishahara minono wanayolipwa, utafiti  wa REPOA umebaini.

WASOMI WAAFIKI WALICHOFANYIWA AKINA ZITTO KABWE CHADEMA...

Viongozi wa Chadema wakishiriki katika moja ya kampeni za chama hicho.
Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa Chadema (Chaso) Mkoa wa Dar es Salaam, umeunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho wa kuwavua madaraka aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na wenzake wawili wakisema Kamati hiyo imefuata misingi ya Katiba ya Chama.

JICHO LA TATU...


ACHOKA KULEA MAMA MKWE NA KUAMUA KUMUUA SINGIDA...

Kamanda Geofrey Kamwela.
Watu wawili wamekufa katika matukio tofauti mkoani hapa, likiwamo la kikongwe kupigwa fimbo kichwani na mkwewe aliyedai kuchoka kumlea.

Friday, November 29, 2013

WAFUASI WA KAMBI MBILI ZA UCHAGUZI WAIBUKA CHADEMA...

Baadhi ya wafuasi wa Chadema katika moja ya mikutano ya chama hicho.
Baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kufunga mjadala wa mgogoro unaoendelea ndani ya chama hicho, agizo hilo limeonekana kufuatwa vema na wajumbe wa Kamati Kuu, lakini limewafungua wajumbe wa Baraza Kuu, Mkutano Mkuu na taasisi za chama hicho.

JICHO LA TATU...


POLISI SASA KUTUMIKA KUFUNGA VYUO 'BUBU' VYA UFUNDI...

Philipo Mulugo.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amesema ataanza kutumia Jeshi la Polisi, kufunga vyuo vyote vinavyoendeshwa bila ithibati ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte).

TUME YA MABADILIKO YA KATIBA YAONGEZEWA SIKU 14...

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, imeongezwa siku 14 kuanzia Desemba 16 ili iweze kukamilisha kazi yake, imeelezwa.

Thursday, November 28, 2013

KESI YA MAUAJI DHIDI YA PAPAA MSOFE HADI DESEMBA 11...

Marijan Abubakar  ‘Papaa Msofe’.
Kesi ya tuhuma za mauaji inayomkabili mfanyabiashara maarufu, Marijan Abubakar  ‘Papaa Msofe’ na mwenzake, imeahirishwa hadi Desemba 11 mwaka huu, kutokana na Wakili wa upande wa mashitaka kutokuwepo.

JICHO LA TATU...


UANACHAMA WA ZITTO KABWE SASA WAIPASUA KICHWA CHADEMA...

Kabwe Zitto.
Uanachama wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe umetajwa kuwa ‘kaa la moto’ kwa uongozi wa chama hicho hata kabla ya kiongozi huyo kujibu mashitaka 11 yanayomkabili ili kunusuru uanachama wake.

MWANDISHI WA HABARI MKONGWE AFARIKI DUNIA...

Marehemu Dunia Mzobora.
Mhariri Mwandamizi wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, Dunia Mzobora amefariki dunia.

Wednesday, November 27, 2013

ALIYEJIFANYA NI ASKARI USALAMA BARABARANI APANDISHWA KIZIMBANI...

James Hassan.
Kesi ya mkazi wa Dar es Salaam aliyejifanya askari wa usalama barabarani, James Hassan (45) imeanza kusikilizwa  katika Mahakama ya Wilaya  ya Ilala kufuatia kukamilika kwa upelelezi.

MAMIA WAJITOKEZA DAR KUMZIKA MWANAFUNZI ALIYEUAWA NCHINI KENYA...

Jeneza lenye mwili wa Jerry Mruma likishushwa kaburini wakati wa mazishi kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam jana.
Waziri mstaafu Cleopa Msuya jana aliongoza mamia ya watu waliojitokeza jijini Dar es Salaam katika maziko ya mwanafunzi wa kitanzania aliyeuawa  Nairobi, Kenya, Jerry Mruma (23).

JICHO LA TATU...


HATUA DHIDI YA ZITTO NA WENZAKE NI KAMA ILE YA AKINA CHACHA WANGWE...

John Mnyika akiteta jambo na Tundu Lissu wakati Chadema ilipokuwa ikitolea ufafanuzi hatua dhidi ya Zitto Kabwe na wenzake, mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam jana.
Hatua iliyochukuliwa na Chadema dhidi ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe na Mjumbe wa zamani wa Kamati Kuu, Dk Kitilla Mkumbo, haitofautiani na waliyochukuliwa Katibu Mkuu wa zamani, Dk Aman Kabourou na Makamu Mwenyekiti wa zamani, Chacha Wangwe.

Tuesday, November 26, 2013

INAUZWA HARAKA SANA...


CHADEMA KUTOLEA UFAFANUZI LEO SUALA LA AKINA ZITTO KABWE...

Kabwe Zitto akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi juzi. Kushoto ni Dk. Kitilla Mkumbo.
Baadhi ya wasomi wameitaka Chadema kutumia vikao vyake  kutafakari mgogoro unaoendelea baina ya viongozi wake na kutoa uamuzi ambao utakijenga zaidi.

MWILI WA MANAFUNZI ALIYEUAWA KENYA WAWASILI, KUZIKWA LEO KINONDONI...

Marehemu Jerry Mruma.
Mwili wa mwanafunzi Mtanzania Jerry Mruma (23) aliyeuawa Nairobi nchini Kenya, umewasili nchini jana na kupokelewa na ndugu, jamaa na marafiki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

JICHO LA TATU...


SHULE TATU ZA SEKONDARI ZAFUNGWA KWA UKOSEFU WA CHAKULA...

Wanafunzi wakijipatia chakula shuleni.
Shule  za  sekondari  tatu  za  bweni  mjini Sumbawanga zimelazimika kufungwa kutokana na  wanafunzi  kukosa chakula  baada  ya  wazabuni  kuzira  kuwasambazia  tangu  mapema  mwezi uliopita.

Monday, November 25, 2013

ZITTO KABWE ASISITIZA HATOKI CHADEMA, AASHIRIA KUGOMBEA UENYEKITI MWAKANI...

Kabwe Zitto alipokuwa akielezea msimamo wake mbele ya waandishi wa habari jana Dar es Salaam.
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Kabwe Zitto, amesisitiza kwamba hatoki katika chama hicho, huku akitoa ishara kwamba ‘atamkabili’ Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe, katika uchaguzi mkuu wa chama hicho mwakani.

JICHO LA TATU...


MFANYABIASHARA AJIPIGA RISASI AKISHINIKIZA KURUDIANA NA MKE ALIYEMTALIKI...

Mfanyabiashara maarufu mjini Tabora, Hakimu Hamdun,  mkazi  wa kata ya  Kanyenye anashikiliwa Polisi akituhumiwa kujaribu kujiua kwa kujipiga risasi kutokana na wivu wa mapenzi. 

Sunday, November 24, 2013

HUU NDIO WARAKA ULIOMPONZA ZITTO KABWE NA WENZAKE CHADEMA...

Zitto Kabwe.
Juzi uongozi wa juu wa Chadema ulichukua hatua kali za kuwavua madaraka ndani ya chama hicho vigogo wake watatu, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe; Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitilla Mkumbo na Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.
Kikubwa kilichosababisha hatua hiyo kuchukuliwa ni waraka ufuatao:

JICHO LA TATU...


BINTI AUAWA KWA MPENZI WAKE AKISUBIRIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE...

Mwanafunzi aliyehitimu kidato cha nne mwaka huu, Sharifa Abdallah (18) ameuawa kwa kuchomwa kisu shingoni na mbavuni chumbani kwa mvulana aliyedai  kuwa mpenzi wake maeneo ya Kimara Golani, Dar es Salaam.

Saturday, November 23, 2013

MAOMBI YA TANESCO KUPANDISHA BEI YA UMEME YAPOKEWA NDIVYO SIVYO...

Maombi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ya kupandisha bei ya umeme, yamepokewa kwa hisia tofauti za kuungwa mkono na pia kupingwa.

JICHO LA TATU...


HIKI NDICHO ALICHOSEMA NGUGI WA THIONG'O KUHUSU VIONGOZI WA AFRIKA...

Profesa Ngugi wa Thiong’o.
Mwanazuoni mkongwe na mwanafasihi wa lugha za Kiafrika aliyebobea duniani, Profesa Ngugi wa Thiong’o amesema si viongozi wa serikali za Afrika pekee waliotekwa na fikra za kigeni, bali hata wasomi wa karne ya sasa ni majemedari wanaopigana vita katika kambi ya adui.

ZITTO KABWE NA WENZAKE WAVULIWA MADARAKA YOTE CHADEMA...

Kabwe Zitto.
Sasa ni dhahiri kwamba Chadema inameguka na kubaki vipande, kutokana na uamuzi uliochukuliwa jana na Kamati Kuu yake kuwavua rasmi madaraka vigogo wake watatu.

Friday, November 22, 2013

OMBI LA BABU SEYA, PAPII KOCHA LATUPILIWA MBALI, SASA 'KUFIA' JELA...

Nguza Viking 'Babu Seya' (kushoto) na mwanawe Johnson 'Papii Kocha'.
Ndugu na jamaa wakilia kwa uchungu mahakamani mara baada ya hukumu kutolewa jana.
Mahakama ya Rufani Tanzania, imetupilia mbali ombi la mwanamuziki maarufu nchini mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Nguza Viking 'Babu Seya' na mwanawe Johnson 'Papii Kocha', na kuamuru waendelee kutumikia kifungo cha maisha jela.

WANNE WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KUJIUNGA KUNDI LA AL-SHABAAB...

Wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab.
Watu wanne wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka ya kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la Al Shabaab.

JICHO LA TATU...


SIKU 10 ZA MGAWO WA UMEME ZAPUNGUZWA NA KUFIKIA TANO...

Miundombinu ya umeme.
Makali ya mgawo wa umeme yameanza kupungua baada ya asilimia 80 ya gesi kutoka kisima cha Songosongo, kuanza kuzalisha umeme.

Thursday, November 21, 2013

MSICHANA ALIYEUZA BIKRA YAKE PAUNI 485,000, SASA AAMUA KUINADI UPYA...

Catarina Migliorini.
Mwanafunzi mmoja nchini Brazil ambaye aliuza bikra yake kwa Pauni za Uingereza 485,000 bado anaendelea kuinadi tena kwenye mnada mtandaoni, akidai mapatano ya awali hayakuwahi kukamilika.

BABU SEYA, PAPII KOCHA KUSOTA JELA AMA KUACHIWA LEO...

Papii Kocha na Babu Seya wakiwapungia jamaa zao nje ya Mahakama ya Rufani, Dar es Salaam.
Hatma ya mwanamuziki maarufu nchini mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanawe Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ itajulikana leo katika Mahakama ya Rufani Kanda ya  Dar es Salaam.

JICHO LA TATU...


KILIO CHA WAKULIMA CHAMPONZA WAZIRI WA FEDHA...

Dk William Mgimwa.
Baada ya CCM kusema itamwomba Rais Jakaya Kikwete aruhusu baadhi ya mawaziri wake wafike mbele ya Kamati Kuu ya chama hicho kuhojiwa, wimbi hilo sasa limemkumba Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa.

KAMATI NANE ZA BUNGE KWENDA MAFUNZONI NG'AMBO...

Kikao cha Bunge mjini Dodoma.
Kamati nane za Bunge zinatarajiwa kwenda nje ya nchi kwa ziara za kikazi na mafunzo, huku zingine nane zikiendelea na shughuli mbalimbali nchini ikiwamo kutembelea miradi.

Wednesday, November 20, 2013

AUA WANAFAMILIA NA KISHA KUJIUA KWA RISASI DAR...

Kamanda Marietha Minangi.
Watu wawili wameuawa papo hapo baada ya mtu anayefahamika kwa jina la Gabriel Munisi kuvamia familia moja na kuwapiga risasi na kisha kujifyatulia risasi naye kufa hapo hapo kutokana na wivu wa mapenzi.

JICHO LA TATU...


WAFANYABIASHARA WASISITIZIWA KUNUNUA MASHINE ZA RISITI...

Baadhi ya wafanyabiashara wa Kariakoo waliofunga maduka yao kugomea mashine za risiti juzi.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesisitiza wafanyabiashara kununua mashine za kutolea stakabadhi za ununuzi zilizotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kuwezesha Serikali kupata  fedha zinazotokana na kodi zinazokusanywa.

PROFESA MWALUKO WA ST. JOHN'S UNIVERSITY AFARIKI DUNIA...

Jengo la Utawala la St. John's University, Dodoma ambako Prof. Mwaluko alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana (St John’s) cha mjini Dodoma, Profesa Gabriel Mwaluko, amefariki dunia jana nchini India alikokuwa amekwenda kwa ajili ya matibabu.

Tuesday, November 19, 2013

CHEKA TARATIBU...

Nesi mmoja aliachiwa maagizo na ndugu wa mgonjwa kwamba ikifika Saa 8, ampatie mgonjwa chakula. Kabla ya muda huo, yule nesi akala yeye kile chakula.

MAWAZIRI WATATU WAZEMBE SERIKALI YA CCM KUWAJIBISHWA...

Nape Nnauye.
Mawaziri watatu wanatakiwa kuwajibishwa kutokana na kushindwa kutatua kero za wananchi, imeelezwa.

JICHO LA TATU...


MASHINE ZA RISITI (EFD) SASA KUUZWA KILA AINA KWA BEI YAKE...

Serikali imesema imezungumza na wasambazaji wa mashine za kutolea risiti za elektroniki (EfDs) ili kila aina iuzwe kwa bei yake.

BAJETI YA SERIKALI YAPIGWA JEKI DOLA ZA MAREKANI MILIONI 560...

Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alipokuwa akisoma Bajeti ya Serikali bungeni Dodoma.
Washirika wa  Maendeleo nchini  wamesema licha ya Tanzania kupata  mafanikio katika sekta kadhaa imeonesha kutofanya vizuri katika elimu, maji na nishati, ambako maendeleo bado yanakwenda taratibu.