Wednesday, November 20, 2013

PROFESA MWALUKO WA ST. JOHN'S UNIVERSITY AFARIKI DUNIA...

Jengo la Utawala la St. John's University, Dodoma ambako Prof. Mwaluko alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana (St John’s) cha mjini Dodoma, Profesa Gabriel Mwaluko, amefariki dunia jana nchini India alikokuwa amekwenda kwa ajili ya matibabu.

Profesa Mwaluko ambaye alikuwa akisumbuliwa na kansa ya koo alifariki wakati akiendelea kupatiwa matibabu.
Ofisa Uhusiano wa chuo hicho, Meshack Karim alithibitisha kutokea kwa kifo hicho.
Profesa Mwaluko ambaye ni daktari kitaaluma, amekuwa Makamu Mkuu wa chuo hicho kwa muda wa miaka miwili sasa.
Kutokana na kifo hicho, mahafali ya chuo hicho yalikuwa yafanyike Jumamosi wiki hii yameahirishwa hadi Desemba 14, mwaka huu na hakutakuwa na masomo kwa siku mbili mfululizo,  jana na leo.
Alisema utaratibu wa kuurejesha mwili wa marehemu kutoka India unafanyika nyumbani kwake Kisasa, barabara ya Dar es Salaam mjini Dodoma.

No comments: