![]() |
| Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alipokuwa akisoma Bajeti ya Serikali bungeni Dodoma. |
Hata hivyo, wamesema Tanzania ni mpokeaji mkubwa wa misaada inayoelekezwa katika bajeti duniani na katika mwaka wa fedha 20013/14 washirika hao wameahidi kusaidia dola milioni 560 za Marekani na wameanza na dola milioni 290.2.
Katika bajeti ya mwaka 2012/13 walichangia bajeti kwa dola milioni 584 zaidi ya milioni 495 walizopanga kutoa awali.
Balozi wa Sweden nchini, Lennarth Hjelmaker ambaye pia ni Mwenyekiti wa washirika hao, alisema hayo Dar es Salaam jana katika mkutano wa mwaka wa kupitia bajeti na kuongeza kuwa hadi sasa bajeti ya Tanzania inakwenda kulingana na matarajio.
Kuhusu sekta ambazo maendeleo yao hayajafikiwa, alisema sekta ya elimu ufaulu wa sekondari na msingi umeshuka na uwiano wa walimu na wanafunzi haujafikiwa kwa kiwango stahiki.
Kwenye sekta ya maji nusu ya wakazi vijijini wanakosa maji safi na salama, huku kwenye nishati ikiwa na maendeleo kidogo ya kujenga na kuboresha zaidi miundombinu yenye kutoa uhakika wa upatikanaji wa nishati hiyo kwa wananchi.
“Leo tumekutana kupitia na kutathmini bajeti ili kuchanganua yaliyofikiwa na kujua changamoto zinazokabili na kutafuta namna ya kupambana nazo,” alisema Lennarth na kuongeza kuwa bajeti ya Tanzania huchangiwa na washirika wa maendeleo 12.
Alisema wanatarajia msaada unaotolewa kuelekezwa zaidi katika mpango wa matokeo makubwa sasa ambao lengo lake ni kufikia mafanikio katika sekta za nishati ya gesi asilia, maji, elimu, usafirishaji na ushirikishwaji wa rasilimali.
Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum alisema ili kufikia panapotakiwa lazima kuwe na mifumo ambayo ni pamoja na kujitathmini.
“Ni kweli kuna maeneo ambayo hayajafanya vizuri, kwa mfano eneo la elimu, Serikali imejitahidi sana katika ujenzi wa madarasa lakini zipo changamoto kama za vitabu na madawati na mengine ambayo yanahitaji ushirikiano wa wadau,” alisema Saada na kuongeza kuwa ndiyo maana sekta hizo zimeingizwa katika mpango wa Matokeo Makubwa Sasa.
Kuhusu umasikini alisema uchumi unakua kwa kasi kwa asilimia saba lakini umasikini umekuwa ukipungua kwa asilimia mbili serikali itaelekeza nguvu zaidi katika maeneo ya kuzalisha ajira kwa walio wengi.

No comments:
Post a Comment