Monday, November 18, 2013

LORI LAGONGANA NA TOYOTA NOAH NA KUUA WATU SABA ENEO LA DAKAWA MOROGORO...

Morogoro.
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba watu saba wamethibitishwa kufariki dunia papo hapo muda mfupi uliopita katika ajali ya gari iliyotokea mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, ajali hiyo ilitokea eneo la Dakawa mkoani humo na kuhusisha magari aina ya Toyota Noah lililogongana uso kwa uso na lori la mizigo.
Katika ajali hiyo ambayo imethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, abiria wengine watano waliokuwamo kwenye Noah na mwingine kwenye lori walijeruhiwa.

No comments: