Serikali imekataa viwango vya nauli mpya
vilivyopendekezwa na Kampuni ya Uda Rapid Transit (UDA-RT), itakayotoa huduma
ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam.
Kaya 2,857 wilayani Kilosa zimekosa makazi kutokana na
nyumba 379 kubomoka na nyingine 997 kuzingirwa na maji yaliyotokana na mafuriko
yaliyokumba wilaya hiyo ya Mkoa wa Morogoro.
Mawaziri walioteuliwa na kuapishwa na
Rais John Magufuli kabla ya kula kiapo cha ubunge, wanaruhusiwa kushiriki shughuli
za Bunge kama wabunge wateule.
Polisi mkoani Kagera, wanamshikilia mkazi wa wilaya ya
Misenyi mwenye umri wa miaka 19 kwa tuhuma za kumbaka dada yakemwenye umri wa miaka 15 (majina yanahifadhiwa)
na kumpa ujauzito.
Watu
wanane akiwemo Msaidiziwa Mkuu wa Jeshi
la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Gerald Ryobapamoja na familia yake,wamekufa maji baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kusombwa na maji katika mkondo mpana wa mto unaotenganisha Kibaigwa
na Pandambili, mkoani Dodoma.
Jumuiya ya Mabaharia nchini (JMT), imeiomba serikali
kufufua Shirika la Taifa la Wakala wa Meli Tanzania (Nasaco), ili kuwa na
chombo cha kitaifa kitakachosimamia maslahi ya nchi kwenye sekta hiyo na
kuondokana na ubadhirifu unaofanywa bandarini.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam,
Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete anaendelea vizuri na anaweza kuruhusiwa wiki ijayo.
Msichana mwenye umri wa miaka 15 amekamatwa kwa tuhuma za
kumuua mama yake mzazi na rafiki wa kiume wa mama huyo kwa kile alichodai
kubakwa na mwanaume huyo, polisi wamesema.
Tanzania’s new President John Pombe Magufuli has been a big hit among social
media pundits in the East Africa owing to his tough stance on corruption and
government official excesses.