Jumuiya ya Mabaharia nchini (JMT), imeiomba serikali
kufufua Shirika la Taifa la Wakala wa Meli Tanzania (Nasaco), ili kuwa na
chombo cha kitaifa kitakachosimamia maslahi ya nchi kwenye sekta hiyo na
kuondokana na ubadhirifu unaofanywa bandarini.
Hayo
yalisemwa jana Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Frank Chuma, wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utayari wao wa kufanya kazi kwenye
vyombo vya majini vya uchakataji, utafutaji na uchimbaji wa gesi baharini.
Alisema
ubadhirifu hauwezi kuisha bandarini kwa kuwa hakuna chombo cha kitaifa
kinachosimamia meli zote zinazoingia na kutoka, hivyo inakuwa vigumu kwa taifa
kuwa na takwimu halisi ya meli na idadi sahihi ya mizigo iliyobebwa na meli
hizo.
“Bandarini
kuna ubadhirifu mkubwa, na hauwezi kuisha iwapo Nasaco haitafufuliwa, hivi sasa
kila meli ina wakala wake ambaye ndiye anayejua mzigo uliobebwa ni kiasi gani
na wakati mwingine idadi ya uhakika haisemwi, lakini kama nchi ingekuwa na
chombo cha kusimamia meli zote, ni wazi kwamba hakuna ubadhirifu ungetokea,”
alisema Chuma.
Alisema
taarifa za upotevu wa makontena bandarini unaotokea hivi sasa sio jambo la
ajabu kwa sababu hakuna chombo cha kitaifa kinachokagua na kuhakiki idadi ya
makontena yaliyoingia nchini, jambo ambalo wakati Nasaco ilipokuwa ikifanya
kazi vitendo hivi vya upotevu wa makontena havikuwepo.
Chuma
alisema serikali iangalie upya jinsi ya kufufua Nasaco kwa sababu ni chombo
muhimu cha serikali kitakachodhibiti maslahi ya nchi na hivyo kuziba mianya ya
ubadhirifu na hivyo nchi kuwa na takwimu sahihi za idadi ya meli na mizigo
inayoingia na kutoka.
Akizungumzia
utayari wa mabaharia wa Kitanzania kufanya kazi kwenye meli na vyombo vya utafutaji,
uchimbaji, uzalishaji na usambazaji wa mafuta na gesi baharini, Chuma alisema
wako tayari sasa kufanya kazi hizo baada ya kukamilisha taratibu zote za
kisheria.
Alishukuru
kwamba kilio cha muda mrefu cha mabaharia wa kizalendo kutopewa nafasi kufanya
kazi kwenye meli na vyombo vya kutafuta mafuta na gesi, kimesikika.
“Sheria
za vyombo vya meli ziko wazi, ila zilipindishwa tu na baadhi ya watendaji ambao
kazi zinazopaswa kufanywa na mabaharia wa kizalendo pindi meli zinapotia nanga
kwenye bandari ya Tanzania, zilifanywa na wageni, na sasa tumepigania hilo na
tutahakikisha linatekelezwa,” alise
No comments:
Post a Comment