ATUHUMIWA KUBAKA NA KUMPA UJAUZITO DADA YAKE

Polisi mkoani Kagera, wanamshikilia mkazi wa wilaya ya Misenyi mwenye umri wa miaka 19 kwa tuhuma za kumbaka dada yake  mwenye umri wa miaka 15 (majina yanahifadhiwa) na kumpa ujauzito.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Augustino Ollomi alisema binti huyo alitakiwa kujiunga na masomo ya sekondari katika Shule ya Sekondari Kagera ya wilayani Misenyi.
 Alisema wazazi wa watoto hao walimuona binti yao akiwa na mabadiliko ambayo yaliwashitua na kuchukua uamuzi wa kumpeleka katika Kituo cha Afya kupima ujazuzito.
 “Baada ya kufanyiwa vipimo iligundulika kuwa ana ujauzito wa miezi minne, ndipo wakaja kwetu kutoa taarifa na kwa sasa tumemkamata mtuhumiwa na muda wowote atafikishwa mahakamani.
 “Mtoto huyo amekiri mwenyewe baada ya kufanya naye mahojiano kuwa ni kaka yake aliyempatia ujauzito na kwamba alikuwa anambaka siku za nyuma,” alisema Kamanda Olomi.

No comments: