Saturday, June 22, 2013

MWIGULU NCHEMA ASEMA CCM HAIEPUKI LAWAMA MLIPUKO WA BOMU ARUSHA...

Mwigulu Nchemba.
Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakina namna ya kujivua lawama katika tukio la bomu la kurushwa kwa mkono, kutupwa katikati ya wafuasi wa Chadema, Arusha na kusababisha mauaji.

Friday, June 21, 2013

NASSARI AWASHUKURU MBATIA NA NYALANDU KWA MSAADA WA MATIBABU...

Joshua Nassari.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema) amekanusha kutoroka hospitalini jijini Arusha na badala yake ameshukuru Naibu Waziri na Mbunge kwa kumhangaikia.

GEORGE BUSH AJA DAR KUJADILI KUINUA WANAWAKE DUNIANI...

George W. Bush.
Rais mstaafu wa Marekani, George W. Bush na mkewe, Laura, wanatarajiwa kuwasili nchini mwezi ujao ambapo watahutubia kongamano litakalojadili wajibu wa wake za marais katika kuinua wanawake duniani.

CHEKA TARATIBU...

Jamaa kapiga magoti kuwasilisha maombi yake kwa Mungu na mambo yakawa hivi. Jamaa: "Ee Mungu baba, naomba unipatie gari kubwa na wasichana kibao pembeni yangu." Mungu: "Ni hayo tu?" Jamaa: "Ndiyo!" Baada ya siku chache jamaa akapata kazi ya kuendesha basi la shule moja ya wasichana!! Kasheshe...

HATIMAYE MBOWE NA LEMA WAJISALIMISHA POLISI, WATOA MAELEZO...

Freeman Mbowe (kushoto) na Godbless Lema.
Baada ya utata wa siku kadhaa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) wamejisalimisha Polisi na kutoa maelezo yao.

MTOTO AFANYIWA UPASUAJI KUONDOA MIGUU MIWILI YA ZIADA...

Mtoto Andrew Palismwe baada ya upasuaji huo.
Mtoto wa miezi miwili wa kiume nchini Namibia amefanyiwa upasuaji wa aina yake baada ya kuwa amezaliwa akiwa na miguu minne.

JICHO LA TATU...


SERIKALI YACHARUKIA WASIOTII SHERIA BILA SHURUTI...

Mizengo Pinda.
Serikali imechoka na vurugu ambapo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ametangaza rasmi kwamba inafahamu zinasababishwa na wanasiasa na wafuasi wao na kuonya kwamba wakikaidi amri ya kuacha fujo nguvu za ziada zitaendelea kutumika.

Thursday, June 20, 2013

MTOTO ALIYEJERUHIWA MLIPUKO WA BOMU ARUSHA NAYE AFARIKI DUNIA...

Mtoto Fahad Jamal alipotembelewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi kwenye chumba cha ICU siku chache zilizopita.
Mtoto Fahad Jamal (7) ambaye hali yake ilikuwa mbaya na kulazwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Selian kufuatia kujeruhiwa na bomu katika mkutano wa Chadema Arusha, amefariki dunia juzi saa saba mchana hospitalini hapo.

TANESCO YAIWEKA NJIAPANDA BAJETI YA SERIKALI 2013/14...

Moja ya mitambo ya umeme ya Tanesco.
Matumizi ya Shirika la Umeme (Tanesco) kwa mwaka ujao wa fedha yameiweka Serikali njia panda hasa baada ya kutakiwa kutafuta fedha hizo nje ya bajeti.

CHEKA TARATIBU...

Daladala moja imepakia abiria kibao wakiwamo wazungu wawili. Ukafika wakati kondakta anataka kuwadai nauli. Hapo ikawa kivumbi lugha! Kondakta: "Oyaa, dereva waambie hao wazungu wako wanipe nauli." Dereva: "Waambie mwenyewe, mie leo nasumbuliwa na jino. Linauma ile mbaya!" Kasheshe…

MAONESHO YA SABASABA MWAKA HUU KWA TIKETI ZA KIELEKRTONIKI...

Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wakiwa katika harakati za kuingia kwenye Viwanja vya Sabasaba.
Kwa mara ya kwanza katika kudhibiti mapato na kuondoa usumbufu kwa wananchi, tiketi za kuingia katika Maonesho ya 37 ya Kibiashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) mwaka huu zitakatwa kwa mfumo wa kielektroniki.

JICHO LA TATU...


IDDI SIMBA NA WENZAKE WAACHIWA HURU KESI YA KUFUJA MABILIONI UDA...

Iddi Simba.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru vigogo wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi na kulisababishia shirika hilo hasara ya Sh bilioni 8.4.

Wednesday, June 19, 2013

MBUNGE WA CCM ACHEKELEA SERIKALI KUKAMUA WANANCHI...

Ally Keissy Mohamed.
Wakati wabunge mbalimbali pamoja na Kamati ya Bunge ya Bajeti, wakipendekeza baadhi ya kodi kuondolewa,  Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy Mohamed (CCM) ameitaka Serikali iwakamue vilivyo wananchi.

MAHAKAMA YA RUFAA YAITA JALADA LA KESI YA LWAKATARE...

Wilfred Lwakatare (kushoto) na wenzake wakifuatilia kesi yao mahakamani.
Mahakama ya Rufaa Dar es Salaam imeita majalada ya kesi ya Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema Wilfred Lwakatare na mwenzake Ludovick Joseph kwa ajili ya kufanya marejeo ya uamuzi wa Mahakama Kuu uliowafutia washitakiwa hao mashitaka ya ugaidi.

CHEKA TARATIBU...

Dokta katika hospitali ya vichaa kamkuta kichaa mmoja akichungulia chini ya gari lake. Kwa akili ya haraka Dokta akafurahi sana akiamini kichaa yule kapona. Dokta akamfuata na kumuuliza: "Unafanya nini chini ya gari langu?" Kichaa akajibu: "Natazama kama ni jike au dume!" Kasheshe...

MAGUFULI ASISITIZA BOMOABOMOA DAR HAIEPUKIKI...

Dk John Pombe Magufuli.
Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli ametoa siku saba kwa watu wenye nyumba kando ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuanzia Mwenge hadi Morocco, Dar es Salaam kubomoa kupisha upanuzi wa barabara.

CCM YAOMBWA IRUHUSU WANACHAMA WAKE KUJITANGAZA URAIS...

Frederick Sumaye.
Vuguvugu la Uchaguzi Mkuu wa 2015 linazidi kupamba moto ambapo juzi aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye, ameomba CCM itoe ruhusa mapema kwa wanaowania urais kuanza kutangaza nia lakini bila kukampeni.

POLISI YAKARIBISHA USHAHIDI WA MBOWE NA LEMA...

Mmoja wa mejeruhi wa bomu katika mkutano wa Chadema, Arusha hivi karibuni alipotembelewa na Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal (kulia).
Wakati ikibainika kwamba bomu lililorushwa na kulipuka Arusha limetengenezwa China, Polisi imewataka viongozi wa Chadema kuwasilisha ushahidi ulionao wa mtu aliyelirusha.

JICHO LA TATU...


SHUHUDA ASIMULIA KILICHOTOKEA BOMU MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA...

Baadhi ya watu wakiwa hawaamini kilichotokea baada ya mlipuko wa bomu Arusha.
Yamesemwa mengi kuhusu tukio la kulipuliwa bomu mjini Arusha lililoua watu wawili na kujeruhi wengine zaidi ya 70. Binafsi, nimemsikia Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi akieleza bungeni kile alichodai ndicho kilichotokea.

Tuesday, June 18, 2013

"ANAYETUHUMIWA KURUSHA BOMU MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA ATOROSHWA"...

Baadhi ya majeruhi wa mlipuko huo wa bomu wakipatiwa matibabu hospitalini.
Mtu asiyefahamika aliyerusha bomu kwa mkono katika mkutano wa kampeni za uchaguzi wa madiwani wa Chadema katika kata ya Soweto mkoani Arusha, imebainika aliandaliwa mazingira ya kutoroka ili asikamatwe na mkono wa sheria.

MBUNGE NASSARI ASIMULIA MKONG'OTO ALIOPATA...

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akiwa kitandani hospitalini.
Akielezea kupigwa kwake, Mbunge Joshua Nassari akizungumza na Mbowe  na Nyalandu hospitalini hapo,  alisema alikuwa kwenye kata yake ya uchaguzi lakini ghafla alizingirwa na watu zaidi ya 30.

JICHO LA TATU...


ALIYEDAI ABIRIA WOTE KWENYE NDEGE WAMELISHWA SUMU ADHIBITIWA...

Ndege ya United Airlines inayofanya safari zake Newark imebeba abiria ambaye alidhibitiwa baada ya kudai kwamba kila mtu kwenye ndege hiyo amelishwa sumu.

KODI ZA PETROLI NA MISHAHARA ZATAKIWA KUSHUSHWA...

Wabunge wakiendelea na kikao mjini Dodoma.
Mjadala wa Bajeti ya Serikali ulianza jana kwa taarifa ya Kamati ya Bunge ya Bajeti, ambayo imetaka baadhi ya kodi zilizopendekezwa na Serikali kuongezwa katika mafuta ya petroli, zishushwe au kubaki kama ilivyokuwa katika mwaka huu wa fedha.

CHEKA TARATIBU...

Mwanafunzi kapanda kwenye daladala. Cha kushangaza yule mwanafunzi badala ya kukaa kwenye kiti muda wote akawa akitembea kwenda mbele na kurudi nyuma.

CCM YASHINDA VITI VYA UDIWANI KATIKA KATA 16 KATI YA 22...

Nape Nnauye.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda katika kata 16 kati ya 22 kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika nchini juzi.

Monday, June 17, 2013

BINTI AMCHINJA KICHWA BABA YAKE BAADA YA KUBAKWA...

Baadhi ya wanakijiji wakiwa wameweka ulinzi mkali kuzuia binti huyo asikamatwe na polisi.
Binti mmoja amekata kichwa cha baba yake na kukitenganisha na kiwiliwili kwa kutumia panga baada ya baba huyo kumbaka kwenye nyumba yao iliyoko katika milima ya Papua New Guinea.