![]() |
| Dk John Pombe Magufuli. |
Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli ametoa siku saba kwa watu wenye nyumba kando ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuanzia Mwenge hadi Morocco, Dar es Salaam kubomoa kupisha upanuzi wa barabara.
Aidha, amesema atakayekaidi agizo hilo nyumba yake itabomolewa kwa lazima na ana ruhusa ya kwenda mahakamani kushitaki, kwani tayari wananchi 81 wameshalipwa fidia ili kupisha upanuzi huo.
Dk Magufuli alitoa agizo hilo mjini hapa jana, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya kuingia mikataba kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan.
Alimtaka Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick Mfugale kutekeleza jukumu la kubomoa nyumba hizo.
“Ukitaka kutoa jipu lazima damu itoke katika mipango yoyote barabara lazima ijengwe, Watanzania lazima waheshimu sheria na watu wachache wasiwe sababu za kuchelewesha ujenzi huo,” alionya.
Alisema wananchi hao walilipwa fidia mwaka jana na licha ya kupokea fidia hiyo, wengine wamejenga kuta kwa ndani.
Alisema mwaka 1997 walishitakiwa mahakamani walipobomoa nyumba 1,000 kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro na Serikali ilishinda kesi ile na kama wasingebomoa kungekuwa na msongamano mkubwa.
“Mfugale lazima ubebe ‘msalaba’ wa kubomoa, upo pale kutekeleza sheria, kwa kuwa ulitaka mwenyewe kazi hiyo… kama huwezi mniajiri mimi hiyo kazi, ili nipitishe hilo tingatinga kubomoa hizo nyumba kwani nitakuwa natekeleza sheria,” alisema.
Dk Magufuli alisema, Serikali haiwezi kusubiri kuona barabara zinachelewa huku wananchi wakihangaika na misongamano ya Dar es Salaam wakati wameshalipwa fidia.
Alisema wakazi hao wanatakiwa kufanya hivyo ili mkandarasi anayefanya kazi kutoka Mwenge hadi Tegeta aendelee mpaka Morocco ili barabara hiyo nayo ijengwe kwa njia nne.
Alisema barabara ya Morocco inatakiwa kukutana na inayojengwa na mradi wa mabasi yaendayo kasi.
Pia alisema mradi huo pia utaanzia Morocco hadi Kivukoni na Kimara ambao utakuwa wa zaidi ya kilometa 21 na kugharimu zaidi ya Sh. bilioni 288.8 na vituo saba vitajengwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia.
Alisema barabara hiyo inaendelea kujengwa, kwani kuna maeneo mengine yatakuwa na njia nne na pengine sita ambapo eneo la Faya kutakuwa na sita.
Alisema Japan imetoa fedha za upanuzi wa barabara kutoka Bendera Tatu hadi Kamata/Gerezani yenye urefu wa kilometa tatu ambapo kutajengwa nne na ya kupita kwa miguu ili kuunganisha daraja la treni kwenda bandarini.
Pia alisema kilometa 79.8 za barabara kwenda Maramba Mawili zitajengwa kwa kiwango cha lami. Alibainisha kuwa mazungumzo na Serikali ya China yanaendelea ili kupanua barabara ya Selander ili kupunguza msongamano.
“Baada ya miaka mitatu nadhani tatizo la msongamano wa magari Dar es Salaam litakuwa limepungua kwa kiasi kubwa,” alisema.
Alisema ili kutimiza azma hiyo, Serikali haiwezi kuendelea kuwasubiri watu wanaovunja sheria hivyo ni vema wananchi wa maeneo hayo wakaheshimu sheria watekeleze agizo hilo, wapishe ili mkandarasi aweze kuanza ujenzi huo ikiwa ni hatua ya kuleta maendeleo.
"Tunataka watu waheshimu sheria ili tujenge barabara tunaona watu wanafukuzwa kazi kwa kuchelewa kazini, ndoa zinavunjika kwa sababu tu ya foleni ni bora uvunje nyumba kuliko kukosa barabara,” alisema.

No comments:
Post a Comment