![]() |
| Baadhi ya watu wakiwa hawaamini kilichotokea baada ya mlipuko wa bomu Arusha. |
Yamesemwa mengi kuhusu tukio la kulipuliwa bomu mjini Arusha lililoua watu wawili na kujeruhi wengine zaidi ya 70. Binafsi, nimemsikia Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi akieleza bungeni kile alichodai ndicho kilichotokea.
Pia nimemsikia, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, anayesema tukio lile limefanywa na Chadema. Nina uhakika makada hawa wa CCM hawaelezi ukweli hasa Nape anayedai kuwa wafuasi wa Chadema ndiyo waliomtorosha mtuhumiwa.
Napenda kupingana na Nape kwa asilimia 100 kwa sababu nilikuwepo na nilishuhudia kila kitu. Napenda kumueleza mwanachama mwenzangu huyu, kwamba tunaweza kuichukia Chadema, lakini kuwasingizia kila kitu vikiwamo vile ambavyo tumevifanya sisi wenyewe, ni dhambi isiyosameheka mbele ya Mwenyezi Mungu na tunalipeleka taifa pabaya.
Katika hili, Chadema hawawezi kufanya njama za kutupa bomu katika mkutano wao wenyewe. Njama hizi zimefanywa na CCM. Na hii siyo mara ya kwanza kwa CCM kufanya njama zinazofanana na hizi, hasa pale kinapoona kinashindwa uchaguzi. Rejea matukio kama haya huko Zanzibar. Ukweli wa tukio hili ni kama ifuatavyo:
Mimi nilikuwa takribani mita nane kutoka mahali ambako bomu hilo lilitua. Ilikuwa majira ya saa 11:50 jioni, muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kumaliza kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara. Aliposhuka tu kutoka kwenye jukwaa ndipo bomu lilipotupwa na kujeruhi makumi ya raia.
Mbowe alishuka kwenye jukwaa kuu majira ya saa 11:40 na kisha kuamuru viongozi wenzake wote waliokuwapo jukwaani, akiwamo mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, kushuka ili kuanza kazi ya kukusanya “sadaka.”
Michango ya sadaka ililenga kusaidia gharama za uchaguzi kwa kuwalipia chakula na vinywaji mawakala wa Chadema waliopangwa kusimamia uchaguzi.
Kwa wanaofahamu jiogrofia ya uwanja wa Soweto, jukwaa kuu lilikuwa upande wa Mashariki, likiangalia upande wa Mgharibi ambako watu walikuwa wamekaa. Nyuma ya jukwaa kuu kulikuwa na gari ya matangazo na ndiko kwenye barabara.
Ng’ambo ya barabara, kuna makazi ya watu – (Kota) za Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Mbele ya nyumba hizo za AICC kuna kichaka cha Maua ya Bogavilia.
Bomu lililoteketeza maisha ya watu wawili na kujeruhi wengine wengi, lilirushwa kutoka Kaskazini Mashariki mwa uwanja wa Soweto, eneo ambalo mkutano ulifanyika. Bomu hili lilielekezwa mahali ambako Mbowe na Lema walikuwapo. Wote wawili walikuwa katikati ya watu wakikusanya “sadaka.”
Askari wa jeshi la polisi waliokuwapo uwanjani, walikuwa upande wa Kusini Magharibi mwa uwanja na jukwaa kuu. Bomu liliporushwa lilipita juu yetu likiwa limefungwa na kitu cheusi kama Soksi au Nailoni.
Kabla ya bomu hilo kutua chini na kulipuka, binafsi nilipoona likipita juu, nilidhani ndege aina ya Popo. Nilidhani ndege huyo alikuwa ametoka kwenye mti uliopo jirani na eneo ambalo jukwaa lilikuwapo. Baada ya mlipuko na watu kuanza kukimbia huku na kule, ndipo polisi walipoanza kurusha risasi hovyo kuelekea jukwaa kuu na baadhi ya risasi zilipiga watu na zingine kutoboa tanki la mafuta ya gari la matangazo la Chadema. Baada ya wananchi kuona polisi hawamkamati mtuhumiwa – ambaye wananchi walimuona akirusha bomu hilo – walianza kumfuata na kutaka kumkamata wao wenyewe. Lakini ghafla polisi walianza kufyatua risasi hovyo na mabomu ya machozi.
Kitendo hicho kiliwaudhi wananchi ndipo walipoamua kujihami kwa kurusha mawe. Hiyo ilikuwa takribani dakika 10 baada ya bomu kutupwa. Baadaye polisi walifanikiwa kukimbia na “mtuhumiwa wao.”
Baada ya Polisi kukimbia wananchi wakaamua kuchukua majeruhi kuwapeleka hospitali. Katika harakati zao za kumtorosha mtuhumiwa Polisi hawakukumbuka kuchukua hata majeruhi mmoja, pamoja na kwamba walikuwapo eneo la tukio.
Askari wa jeshi la polisi walirejea tena uwanja wa Soweto, zaidi ya dakika 45 baada ya bomu kupigwa. Huu ndiyo ukweli na siyo maelezo ya William Lukuvi, anayedai kuwa Chadema ndiyo walimtorosha mtuhumiwa.
Mawazo yangu mimi ni kuwa bomu la Soweto linakamilisha mpango uliokusudiwa wa kuvuruga uchaguzi ili kutoa nafasi kwa CCM kujipanga. Nape analijua hili. Mimi ninalijua hili na baadhi ya viongozi wanalijua hili.
Hili linaweza kuthibitishwa na hatua ya polisi kushindwa kumkamata mtuhumiwa, wakati walikuwa wamejazana uwanjani. Walivyofyatua risasi za moto na mabomu ya machozi kutawanya watu, wakati walipaswa kutuliza watu na kuwasaidia majeruhi.
Nape anasema Chadema ndiyo iliyohusika na mlipuko huu. Anasema eti wamefanya hivyo kwa sababu wameogopa kushindwa uchaguzi. Lakini Nape hebu tuwe wakweli kidogo: Mbona vurugu na mauaji yanatokea kule ambako CCM kinazidiwa; na siyo kule ambako Chadema wamekuwa wakizidiwa?
Lakini kuna jingine hapa linaloonekana. Wakati Nape anataja Chadema kuwa ndiyo wahusika, serikali ya chama chake inasema, haifahamu aliyehusika na mlipuko huo. Tayari imedai kutenga kiasi cha Sh. 100 milioni kwa yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa wahusika.
Hii ni tamthilia nyingine ambayo serikali inataka kuicheza. Ni kama ilivyofanya kwa wahusika wa utekaji, utesaji na ung’oaji meno na kucha na kisha kumtupa kwenye msitu wa Mabwepande, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka.
Mpaka sasa, serikali inasema haiwafahamu waliomteka Ulimboka, zaidi ya raia mmoja wa Kenya, Joshua Mulundi.
Serikali inasema haijaweza pia kumfahamu aliyemteka na kumtesa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda. Yaelekea pia serikali haimfahamu aliyeamrisha kurushwa bomu lililochukua maisha ya mwandishi wa habari, Daud Mwangosi.
Mimi nafahamu kuwa Nape anawajua wote hawa. Kwake yeye wahusika ni Chadema.
Kauli ya Nape ina maana tatu kubwa: Kwanza, kwamba yeye ni zaidi ya vyombo vya ulinzi na usalama vikiwamo Polisi na Usalama wa Taifa (TISS), yaani yeye katika uchunguzi ni baabukubwa. Tayari amefanya uchunguzi na amefahamu mhusika mkuu wa tukio lile la kishetani lililochukua uhai wa raia wawili na kujeruhi makumi wengine.
Pili, Nape amethibitisha kwamba aliyehusika na mlipuko ule ni mtu kutoka vyombo vya ulinzi na usalama. Hivyo kauli ya serikali ya kutenga Sh. 100 milioni kusaka mlipuaji ni geresha tu. Na kwamba huu ndiyo msingi wa yeye kuanza poropaganda za kudai Chadema ndiyo wanaohusika na mlipuko huo.
Tatu, Nape ameonyesha jinsi anavyoshindwa kuchagua maneno ya kusema – kipi kisemwe wapi na kipi kiachwe. Kwa kusingizia Chadema katika hili, hakisaidii hata chama chake.
Hata kama ingekuwa ni Chadema kilichohusika na mlipuko ule, bado ukweli ni kuwa serikali ilipaswa kulinda raia wake. Hatua ya serikali kusema, haifahamu mlipuaji, huku yeye akidai ni Chadema, basi serikali hiyo haipaswi kuendelea kuwapo.
Na Watanzania wanafahamu kuwa kitendo cha Nape kushabikia mauaji, hakiwezi kukubarika. Ni kinyume na ustawi wa taifa letu.
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere amewahi kusema mara nyingi kuwa upumbavu ni kipaji. Mtu anaweza kuzaliwa nacho na aweza kufa nacho. Ni tofauti na mtu mjinga. Huyu mjinga anaweza kueleweshwa na ujinga wake ukafutika.
Tunaomfahamu Nape tunajua jinsi alivyo “mpuuzi.” Jinsi alivyo kibaraka. Ndiyo maana tumeanza kujua kuwa kelele zote alizokuwa akipiga huko nyuma – hadi kujiapiza kwa mabaya na hata kumuapiza Rais Kikwete, zililenga kutafuta madaraka.
Nakumbuka moja ya kauli zake Nape aliyowahi kuniambia wakati ule alipokuwa mbioni kutaka kuhama nchi kwa sababu mgombea wa CCM Jakaya Kikwete alipopitishwa na chama chake kugombea urais. Nitaeleza nitalieleza hili siku ikifika.
Lakini kama Rais Kikwete analitakia mema taifa hili na anapenda kuondoka madarakani kwa heshima, ajihadhari mno na wanasiasa vinyonga aina ya Nape. Vinginevyo, kuna siku Nape anayesingizia Chadema haya, atageuka na kumsingizia Kikwete, chama chake na familia yake. Tuombe Mungu asifike huko.

No comments:
Post a Comment