Wednesday, February 29, 2012
CHEKA TARATIBU...
Kulikuwa wa jamaa mmoja kwenye wodi ya vichaa Mirembe, Dodoma. Kila siku jamaa huyo alikuwa akitega sikio lake ukutani mithili ya mtu amayesikiliza kitu. Dokta aliyekuwa akiwahudumia alikuwa akiona tabia hii kila siku. Akaanza kufuatilia kwa karibu kila mara na kumkuta hivyo. Siku moja Dokta akaamua kuingia ndani na kwenda moja kwa moja kwenye ule ukuta na kutega sikio lake huku yule jamaa akimtazama kwa makini. Dokta akamgeukia yule jamaa na kusema, "Mbona sisikii chochote?" Ndipo yule jamaa akamjibu, "Kwa muda mrefu sasa hali iko hivyo hivyo." Duh!
UNAWATEGA MADEREVA WENZAKO...
Lori likiwa limeharibika kwenye kona zilizoko maeneo ya viwanja vya Gymkhana, Posta Dar es Salaam leo asubuhi kiasi cha kuhatarisha usalama wa watumiaji wengine wa barabara hiyo. (Picha na ziro99blog)
HATARI LAKINI SALAMA...
Mwendesha baiskeli ya miguu mitatu maarufu kama Guta akiendesha kwenye barabara ya Kinondoni jambo ambalo ni hatari kwa usalama wake kutokana na kasi ya magari yanayopita njia hiyo nyakati za asubuhi. (Picha na ziro99blog)
MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA...
Usemi wa "Mbuyu ulianza kama Mchicha" unaweza kuleta maana kama inavyoonekana pichani. Taka hizi zikiwa vimetelekezwa kwenye kituo cha daladala Mwananyamala Komakoma jambo ambalo linaashiria kama hatua za haraka hazitachukuliwa basi katika siku chache zijazo tunaweza kushuhudia dampo kubwa kituoni hapo. Zilianza chache na sasa ndio kama hivyo. (Picha na ziro99blog).
WABONGO SASA TUMEFIKIA HAPA
Viroba vilivyojaa uchafu vikiwa vimetelekezwa kando ya barabara maeneo ya Wabongo wenye "Maisha Bora" Mikocheni Regent, Dar es Salaam kama vilivyokutwa leo asubuhi. (Picha na ziro99blog)
Tuesday, February 28, 2012
MATUNDA YA DALADALA KUKATISHA "RUTI"
Abiria wakisubiri usafiri kwenye kituo cha Mwananyamala Komakoma, Dar es Salaam leo asubuhi. Kumekuwa na tatizo la usafiri kwa wakazi wa maeneo ya Mwananyamala kwenda mjini kutokana na tabia iliyozuka hivi karibuni ya daladala kukatisha safari na mengi kati yao kugeuzia Kinondoni kwa Manyanya. (Picha na ziro99blog).
FOLENI LEO ASUBUHI...
Hapa foleni hii ilikuwa maeneo ya Kinondoni Makaburini, Dar es Salaam mishale ya saa 1:35 asubuhi. (Picha na ziro99blog)
Barabara ya Bagamoyo maeneo ya St. Peter's hali ya foleni asubuhi hii ilikuwa hivi. Hii ilikuwa mishale ya saa 1:40 asubuhi. (Picha na ziro99blog)
Barabara ya Bagamoyo maeneo ya St. Peter's hali ya foleni asubuhi hii ilikuwa hivi. Hii ilikuwa mishale ya saa 1:40 asubuhi. (Picha na ziro99blog)
CHEKA TARATIBU...
Jamaa kaenda kupata kilaji na mkewe kwenye baa moja maeneo ya Kinondoni kwa Manyanya. Baada ya kinywaji kukolea mitaa ya saa nane za usiku, jamaa kamchukua mkewe kurudi nyumbani. Walipofika mlangoni jamaa katoa funguo na kutaka kufungua mlango. Muda ukazidi kwenda huku jamaa akihangaika kutumbukiza ufunguo kwenye tundu mlangoni. Ndipo mkewe akaamua kutaka kumsaidia zoezi hilo. Weeee! Jamaa akageuka na kumfokea, "Unachotakiwa kufanya hapa ni kushikilia nyumba isicheze-cheze." Mh, kweli ulevi noma!!
MTENGENEZAJI KATUNI ZA "BERENSTAIN BEARS" AFARIKI
Mtunzi wa nguli wa vitabu vya watoto na mtengenezaji wa katuni za Berenstain Bears, Jan Berenstain amefariki dunia akiwa na miaka 88 baada ya kupata maradhi ya kupooza mwili, imeeleza familia yake.
Jan na mumewe, Stan Berenstain walibuni na kutengeneza katuni za familia ya Bear (Mama Bear, Papa Bear, Brother Bear and Sister Bear ) mwaka 1962 pale walipoweza kuchapisha kitabu chao cha kwanza "The Big Honey Hunt."
Tangu hapo, waliweza kuchapisha hadithi na visa zaidi ya 300 zinazohusu katuni hizo.
Kwa mujibu wa mtoto wake wa kiume, Jan alisumbuliwa na maradhi ya kupooza ghafla na siku iliyofuata akafariki dunia.
Mumewe, Stan alifariki dunia mwaka 2005 akiwa na umri wa miaka 82.
Marehemu ameacha watoto wa kiume kadhaa na wajukuu wanne.
Mungu ailaze roho ya marehemu Jan mahali pema peponi, Amen.
Jan na mumewe, Stan Berenstain walibuni na kutengeneza katuni za familia ya Bear (Mama Bear, Papa Bear, Brother Bear and Sister Bear ) mwaka 1962 pale walipoweza kuchapisha kitabu chao cha kwanza "The Big Honey Hunt."
Tangu hapo, waliweza kuchapisha hadithi na visa zaidi ya 300 zinazohusu katuni hizo.
Kwa mujibu wa mtoto wake wa kiume, Jan alisumbuliwa na maradhi ya kupooza ghafla na siku iliyofuata akafariki dunia.
Mumewe, Stan alifariki dunia mwaka 2005 akiwa na umri wa miaka 82.
Marehemu ameacha watoto wa kiume kadhaa na wajukuu wanne.
Mungu ailaze roho ya marehemu Jan mahali pema peponi, Amen.
Monday, February 27, 2012
LIVERPOOL MABINGWA KOMBE LA CARLING
Liverpool jana ilifanikiwa kutwaa Ubingwa wa Kombe la Carling kwa kuinyonyoa Cardiff kwa mikwaju ya penalti 3-2 baada ya kutoka sare ya 2-2 katika muda wa nyongeza kwenye mechi kali ya fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Wembley.
CHEKA TARATIBU...
Jamaa kaingia kwenye mgahawa huko Gabon siku moja baada ya fainali za Kombe ka Mataifa ya Afrika. Meza ya pembeni kamkuta mshambuliaji wa Ivory Coast, Didier Drogba akipata kifungua kinywa kwa kutumia bakuli. Jamaa akauliza, "Drogba mbona unatumia bakuli?" Drogba akajibu, "Mshamba nini, we hujui kwamba KIKOMBE wamechukua Zambia?" Duh!
PAMOJA NA KUWEKA ULINZI MKALI...
Mapaparazi hawakukubali mpaka wakapata picha ya mwili wa Whitney Houston ukiwa ndani ya jeneza tayari kwa waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho. Nani alipiga picha hii? Bado ni kitendawili.
WHITNEY ALIFIA HUMU!
Picha iliyopigwa muda mfupi baada ya polisi kuondoa mwili wa Whitney ikionyesha bafu likiwa bado na maji kwenye Hoteli ya Beverly Hilton. Vinaonekana vitu mbalimbali kwa ndani yake kama taulo (kushoto), chanuo (chini) na mafuta ya kulainisha ngozi (katikati).
CHUMBA ALICHOFIA WHITNEY CHAPATA MTEJA!
Chumba ambamo alifia mwanamuziki Whitney Houston. Wahusika wameeleza kwamba wanaendelea 'kula vichwa" kwenye chumba hicho ambacho hupangishwa kwa Pauni 375 kwa usiku mmoja. Kwa sasa tayari kimepata mtu.
FAMILIA YA WHITNEY YAPATA PIGO TENA!!
Vyanzo vya habari vilivyo karibu na familia hiyo vimesema familia sasa imechanganyikiwa mno na kwamba hawafahamu ni kwa jinsi gani picha hizo zimepatikana kutokana na ulinzi mkali uliowekwa kwenye shughuli nzima ya mazishi ya Whitney.
Familia hiyo inahisi kwamba picha hizo zimepigwa na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni iliyosimamia mazishi hayo, lakini hawafahamu ni nani hasa atakuwa amewahujumu ikizingatiwa kwamba ilikubalika mazishi hayo yawe siri.
Vyanzo vya habari vimesema kwamba Mama wa Whitney, Cissy, amelichukulia suala hilo kwa uzito wa juu.
Pamoja na kushtushwa huko, imefahamika kwamba familia hiyo haitachunguza tukio hilo wala kuchukua hatua zozote za kisheria.
Lakini, mmiliki wa kampuni iliyosimamia mazishi hayo amekanusha vikali kuhusika kwa namna yoyote ile ama mfanyakazi wake kuhusika na picha hizo au kuharibu shughuli hiyo. (Kutoka Mtandaoni)
Sunday, February 26, 2012
ARSENAL YAIMONG'ONYOA TOTTENHAM 5-2
Mtambo wa mabao na Nahodha wa Arsenal, Robin van Persie (10) akiifungia timu yake bao kwenye mechi ya Ligi Kuu ya soka England dhidi ya "Wabishi" Tottenham Hotspurs leo Jumapili kwenye Uwanja wa Emirates. Arsenal ilishinda mabao 5-2.
EXTRA BONGO KAZINI
Wanenguaji wa Extra Bongo wakionyesha umahiri wao wa kucheza miondoko ya Kizigo katika onyesho la usiku wa kuamkia Jumapili. Wa pili kulia ni kiongozi wa wacheza shoo, Super Nyamwela. (Picha na ziro99blog)
EXTRA BONGO KAZINI
Jenerali Banza Stone akishambulia jukwaa katika onyesho la bendi ya Extra Bongo kwenye ukumbi wa Meeda, Sinza Mori usiku wa kuamkia leo Jumapili. (Picha na ziro99blog)
EXTRA BONGO KAZINI
Kiongozi wa bendi ya Extra Bongo "Next Level - Wazee wa Kizigo", Kamarade Ally Choki (katikati) akiongoza safu ya waimbaji wa bendi hiyo katika onyesho la bendi hiyo usiku wa kuamkia leo Jumapili kwenye ukumbi wa Meeda, Sinza Mori. (Picha na ziro99blog)
Saturday, February 25, 2012
Friday, February 24, 2012
Thursday, February 23, 2012
Wednesday, February 22, 2012
Monday, February 20, 2012
Sunday, February 19, 2012
BOBBY APIGWA STOP MAZISHI YA WHITNEY
Bobby Brown akiondoka kwa hasira baada ya kuzuiwa kanisani.
IMEELEZWA kwamba Bobby Brown amezuiliwa kuhudhuria mazishi ya Whitney Houston baada ya kuzusha malumbano na familia ya Houston kutaka aruhusiwe kuambatana na jamaa zake tisa kwenye misa ya kumwombea marehemu Newark, New Jersey.
Bobby alionekana akiingia kanisani mapema leo, lakini baada ya muda mfupi alitoka na kutokomea.
Vyanzo vya habari zilieleza kwamba Bobby alialikwa kuhudhuria pamoja na wapambe wawili, lakini badala yake aliambatana na msafara wa watu tisa. Baada ya kuzuiliwa, Bobby alionekana kuhamaki kabla ya kuamua kutoka nje na kuondoka.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, inasemekana Bobby alitaka kukaa pembeni ya binti yake Bobbi Kristina, lakini watu wa familia ya Houston wakamdhibiti kabisa na kushindwa azma yake hiyo.
Imeelezwa katika sakata hilo, Mchungaji Jesse Jackson alijaribu bila mafanikio kusawazisha mambo kati ya pande hizo mbili lakini ikashindikana.
HABARI ZILIZOTUFIKIA PUNDE...
Mchungaji Al Sharpton akielezea tukio hilo alisema, "Hakuna baya alilofanya bali kuonyesha upendo na heshima kwa Whitney. Napenda sasa watu wasimwandame tena Bobby, wamwache".
Baadaye Bobby alitoa kauli kwa kusema, "mimi na wanangu tulialikwa kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mke wangu Whitney Houston. Tulikaa chini ya ulinzi na katika hali isiyoeleweka tukatakiwa kuhama zaidi ya mara tatu".
Aliendelea, "Sijui kwanini walinzi walitufanyia hivyo na kututaka tutulie hapo hapo. Walinzi walinidhibiti nisimsogelee binti yangu Bobbi Kristina, na ili kuepusha shari nikaamua kwenda kubusu jeneza la aliyekuwa mke wangu na kisha kuondoka zangu".
Saturday, February 18, 2012
UJENZI WA BARABARA YA BAGAMOYO
Ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo umeshika kasi kama mafundi hawa walivyokutwa na 'wazururaji' wetu eneo la Mbezi jirani la Kambi ya Jeshi Lugalo, Dar es Salaam mchana huu. (Picha na ziro99blog)
UNAPOM-BIPU ISRAEL!
Mwendesha bodaboda akiendesha katikati ya barabara kama alivyonaswa na 'wazururaji' wa ziro99blog eneo la Manzese Darajani, Dar es Salaam mchana wa leo. Kumekuwa na ripoti za vifo vingi vya watumiaji wa usafiri huu lakini vingi vimekuwa vikitokana na uendeshaji mbovu na kutozingatia sheria za usalama barabarani. Kama una lolote tuma kwa: ziro99blog@gmail.com
Subscribe to:
Posts (Atom)