Bobby Brown akiondoka kwa hasira baada ya kuzuiwa kanisani.
IMEELEZWA kwamba Bobby Brown amezuiliwa kuhudhuria mazishi ya Whitney Houston baada ya kuzusha malumbano na familia ya Houston kutaka aruhusiwe kuambatana na jamaa zake tisa kwenye misa ya kumwombea marehemu Newark, New Jersey.
Bobby alionekana akiingia kanisani mapema leo, lakini baada ya muda mfupi alitoka na kutokomea.
Vyanzo vya habari zilieleza kwamba Bobby alialikwa kuhudhuria pamoja na wapambe wawili, lakini badala yake aliambatana na msafara wa watu tisa. Baada ya kuzuiliwa, Bobby alionekana kuhamaki kabla ya kuamua kutoka nje na kuondoka.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, inasemekana Bobby alitaka kukaa pembeni ya binti yake Bobbi Kristina, lakini watu wa familia ya Houston wakamdhibiti kabisa na kushindwa azma yake hiyo.
Imeelezwa katika sakata hilo, Mchungaji Jesse Jackson alijaribu bila mafanikio kusawazisha mambo kati ya pande hizo mbili lakini ikashindikana.
HABARI ZILIZOTUFIKIA PUNDE...
Mchungaji Al Sharpton akielezea tukio hilo alisema, "Hakuna baya alilofanya bali kuonyesha upendo na heshima kwa Whitney. Napenda sasa watu wasimwandame tena Bobby, wamwache".
Baadaye Bobby alitoa kauli kwa kusema, "mimi na wanangu tulialikwa kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mke wangu Whitney Houston. Tulikaa chini ya ulinzi na katika hali isiyoeleweka tukatakiwa kuhama zaidi ya mara tatu".
Aliendelea, "Sijui kwanini walinzi walitufanyia hivyo na kututaka tutulie hapo hapo. Walinzi walinidhibiti nisimsogelee binti yangu Bobbi Kristina, na ili kuepusha shari nikaamua kwenda kubusu jeneza la aliyekuwa mke wangu na kisha kuondoka zangu".
No comments:
Post a Comment