Mabasi
mawili yamegongana uso kwa uso wilayani Sikonge mkoani Tabora na kuua abiria
13, wakiwemo madereva wa mabasi hayo na kujeruhi wengine 73.
Moja
ya mabasi hayo, lilikuwa likitokea mkoani Mwanza kwenda Mpanda na lingine
likitokea mkoani Mbeya kwenda Mwanza.
Taarifa
kutoka eneo la tukio, ilieleza kuwa mabasi hayo yalipata ajali hiyo jana saa
10.05 jioni katika eneo la Mlogoro, kilometa tatu kabla ya kuingia katika mji
wa Sikonge.
Mabasi
hayo moja linamilikiwa na Kampuni ya AM Investment Namba T 803 ATN, lililokuwa
likitokea Mwanza kwenda Mpanda.
Lingine
ni mali ya kampuni ya Sabena Namba T 110 ARV, lililokuwa likitokea Mbeya kwenda
jijini Mwanza.
Akizungumza
namwandishi kwa simu jana jioni, Kaimu Mganga wa Wilaya ya Sikonge, Dk John
Buswelu, alisema hospitali hiyo ilikuwa imeshapokea miili 13 ya abiria
waliokufa, huku mmoja ukiwa kiwiliwili bila kichwa.
Shuhuda
wa ajali hiyo aliyekuwa sehemu ya tukio, Suleimani Kambuzi alidai majeruhi
waliotolewa katika ajali hiyo, walikuwa zaidi ya 70. Alidai wengine walikuwa
wakiendelea kutolewa na kupelekwa hospitalini.
Mwandishi
alimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Suzan Kaganda, ambaye alikiri
kufahamu kutokea kwa ajali hiyo.
Aliongeza kuwa taarifa rasmi ataitoa leo.
Ajali
hiyo imetokea wakati Watanzania hawajasahau ajali iliyotokea wakati wa Sikukuu
ya Idd el Fitri mwezi uliopita, na kuua watu 17 katika eneo la Pandambili
wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
Ajali
hiyo ilihusisha basi la kampuni ya Moro Best, lenye namba za usajili T 258 AHV
lililokuwa likitoka Mpwapwa kwenda Dar es Salaam. Basi hilo liligongana uso kwa
uso na lori la mizigo, lenye namba za usajili T820 CKU -T 390 CKT, lililokuwa
likitokea Dar es Salaam kwenda Dodoma.
No comments:
Post a Comment